St. Francis Mbeya kuna siri gani?

NO!! NO!! NO!! NO!!

BIG BIG NO!!!
 

Unaweza kuta ndio bwana Supika aliyetoka
 
Nimegundua Kuna kizazi Cha wapumbavu sana. Sisi tulikuwa shule ya serikali michepuo miwili wakati inaanza na jumla tulikuwa 82.

My friend mwaka 2001 hiyo, hakuna aliyetoka na div 3 na wote tuliingia University na Leo tuna mawaziri wawili na makatibu wakuu pamoja na Senior Managers kibao.

Wengine Mahakamani ni Jaji mmoja na mahakimu kadhaa, so msishangae huo ufaulu nyie mpo busy kucheza viduku. Pale st Francis ni shuleshule tu, ukikutwa na simu ni nyumbani huwa hakuna majadiliano, ukipungua wastani ni nyumbani.

Shule mnaenda mnashikana na mademu mtaweza kusoma kweli? Unaenda shule una daftari unaandika nyimbo eti unataka kuwa Kama diamond sasa unasoma ili iwe nini?

Someni vijana
 
Let's assume wanafunzi 2000 wameenda kwa interview ya kujiunga form one pale st Francis girls alafu wanafanya wrritten na oral interview baada ya hapo wanachagua wanafunzi timamu 120 pekee walopata kuanzia wastan wa 95 iv na kila wanavoingia kidato kingne wanachuja na kufukuza wasiofika viwango vya wastan wao unafikir hawawez kupata one ya7?? Inawezekana tena hata bila kuiba hata Mzumbe Kibaha kilakala iliboru tabora boys zingefanya ivo zingekuwa top kuzid hata hz za private⛷🏇🚴‍♂️
 
Kizazi cha wapumbavu?? Kwaiyo nyie ndo mlikuwa intelligent kuliko wengne wote??@@ i previously had the same mentality like u but now ........
 
Ndugu PainKiller nafikiri kuna kitu haukijui

Binafsi ni moja kati ya watu ambao nilibahatika kuajiriwa na kufundisha moja kati ya shule ambayo ipo top ten hapo inaitwa Bright Future Girls ipo Mbondole - Serikali ya Mtaa Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam mwaka jana 2021

Kiukweli hakuna kitu kinachoitwa kununua mitihani au kufanya siku kadha nyuma kabla ya mtihani wa mwisho, Hakuna kitu kama hicho.

Shule zina mikakati asee, picha linaanza Vijana wanapoanza kidato cha kwanza wanachujwa haswaaa, yaan kijana haanzi kidato cha kwanza ikiwa anaonekana wa kawaida bali she've to be very bright.

Wakishaanza kidato cha kwanza ni mchujo mpaka anaingia kidato cha nne, Ratiba zao zipo very tight mpaka Vijana wanalalamika muda mwingine kwa kukosa muda wa kujisomea kwasababu ni wanafanya mitihani kila wiki

Yaan kiukweli siwezi zungumza yote ila ilikua inafikia kipindi tunafundisha ikifika mwezi wa tano unajua kabisa hapa nna uhakika wa division one za single digit ngapi kwahiyo mpaka wanaingia NECTA Mwalimu unaji commit kabisa kwamba division one zote

Motisha kwa Walimu baada ya Vijana kufaulu ni kubwa ni wewe tuu na idadi ya A's zako
 
Aliyefaulu kiukweli bila kuiba mtihani ni huyo wa Ilboru, kipindi nimeenda advance level darasa letu lilikuwa na hao waliotoka st Francis na kila mtu aliwaogopa chakushangaza mtihani wa kwanza marks walizopata ni tofauti na hizo one zao. Huko private ni business kwa kwenda mbele na solving za paper kwa ajili ya kupata A za kutosha wakati zikija kitaa inputs yake ni zero kabisa
 
Bahati mbaya tukiwapokea vyuoni tunakutana na different story

Ukija makazini ndio usiseme
 
Mkuu punguza uongo,
Hiyo shule ada ni kawaida tu haeana ada kubwa
Hawanunui mtihani.
 
.
 
Wanapewa vitabu! Wanasoma kwa mikakati,wala hakuna cha kuiba mitihani umekutana na sampuli chache!
Nimesoma nao pia Alevel,
Na wengi wako mbali wanapasua anga tu!
 
Wala sio leo tu, miaka nenda rudi wao ndio wanakimbiza! Kuna mwaka wasichana wote top 10 walitoka pale
 
Hiyo shule haijaanza kufaulisha leo, ndani ya shule kuna sehemu wanaubao ambao unaonyesha nafasi waliyoshika kila mwaka kitaifa kuanzia mwaka 1997 kama sijakosea. Nimepeleka dogo hapo anasoma, shida huwa kupita kwenye interview tu na masister wako very strict.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…