Sikia nikwambie mkuu maisha ya shule Mimi nayajua Tena zaidi ya unavodhani ...
Shule kubwa kama hizo ,zinawalimu wakubwa Sana wenye uzoefu wa hali ya juu ,na wanakuwa na connection na walimu wengine zaidi ..
Wanaotunga mitihani ni walimu kutoka kanda mbalimbali ,na wabobevu ,hutoa maswali na mwisho wa siku mtihani kitungwa ...
Utake usitake ,upende usipende hizi shule zinamazingira Safi ,walimu Safi ,lakini wananunua mitihani week kadhaa kabla ya pepar ,.....
Fuatilia mitihani wanayofuanya week mbili kabla ya mtihan pre -necta ,ready for necta ,hio ndio mitihan inayotolewa imejaa maswali yanayotoka necta ...
Sio kwamba wanasoviwa siku ya mtihan hapana ,wanafanya maswali yatakayotoka necta week kabla na walimu wanasisitiza kuyakalili ,....
Kama Kuna swali gumu ambalo linasahaulika ,basi mwalimu ataliimba darasana kila siku na mwisho wa siku wanalikuta necta ....
A inaanzia 81-100 ,bro mtihan wa physics , mathematics , biology , chemistry kwa watoto wote 97 wapate A ,???????? Hawa wa kibongo kabisa ? Woteeeee ? ....
Aiseee ,Mimi nakataa hayo matokeo ...hao watoto uwezo wao wa kawaida tu ,sio wa kupata huo ufaulu wote ,kwa kusema sijui walimu Bora ,mazingira Bora ,...