St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

St kayumba za dar earl2000 darasa la sita kwenda la saba kulikua na utaratibu wa kushindana kwenye mitihani inashirikisha shule nyingi,bwana ulikua ukifeli hizo stick zake balaa[emoji2][emoji2]mda wa kwenda mnashangilia makelele mpk mnafika
 
Maisha ndugu yangu.....hapo kutoka nyumbani mbaka shule ni km9 kichwani umebeba mzigo wa kuni kwa ajili ya kwenda kupikia uji na kujikinga na baridi, mgongoni begi na mkononi fagio na jembe..kwa maisha hayo lazima ngozi ikose Nuru na ukomae.
SAFI SANA, najua hayo mambo kama maana kunakipindi unajipaka mafuta ya kula, ugoko unang'aa utadhani tubelight.
Pamoja na hayo kwangu maisha yale ndio yalikuwa best na yenye furaha sana,,,
 
Asbh tution jion tution hahahhaa nimechapwa sana table[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kitu pekee nachokumbuka ni kwambaaaa..kubebeshwa kote kuni,mbolea,jembe,fagio,kwenda kafanya kazi om kwa mwalimu nk. Nlitoka kama nlivyoingia yan ckuambulia chochote akilini..cjui walikua wanafundisha kikorea
 
SAFI SANA, najua hayo mambo kama maana kunakipindi unajipaka mafuta ya kula, ugoko unang'aa utadhani tubelight.
Pamoja na hayo kwangu maisha yale ndio yalikuwa best na yenye furaha sana,,,
Yani yalikuwa maisha fulani yaliyokamilika, mtu mnakaa wote miaka 7 pamoja halafu sababu ya utoto tulikuwa tumesharidhika na hayo maisha na tuliona kawaida hakukuwa na mtu aliekuwa akiyachukulia maisha serious kihivyo ili ayabadirshe....kiukweli kipindi hiko pamoja na changamoto zote lakini Furaha na Upendo vilitawala.
 
Kingine kipindi cha masika ule muda Wa kuridi mvua ikianza kunyesha ilikuwa bonge LA raaahaaaa tukikuta kidimbwi tu tunakigeuza bwawa aisee basi hapo ni kuogelea na kupiga mbizi kwenye maji ya ugoko
upload_2017-4-23_15-52-40.png
 
Aseee....!
Shule ni kwetu ilikuwa kila alhamis unapikwa uji Wa mchele na wapishi ni ss wanafinzi
Huu uji Wa mchele mi naupenda sana kwahiyo nilikuwa kila unapopikwa nilipenda niwe mmoja Wa wapishi ili niufaidi vizuri kule kule jikoni
Kingine kipindi cha masika ule muda Wa kuridi mvua ikianza kunyesha ilikuwa bonge LA raaahaaaa tukikuta kidimbwi tu tunakigeuza bwawa aisee basi hapo ni kuogelea na kupiga mbizi kwenye maji ya ugoko
Jioni tunakuwa na kazi ya kuanika daftali kwenye moto
Da, nna mengi ya kuelezea aisee ...
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kuanika daftari kwenye moto hiyo hatari likiwaka je [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahahahaa hapo unajiona mjanja sana, alafu hujulikani.
Hapo umetupia kamptula moja ina kiuno size 28 halafu imefungwa na kamba ya kiatu cha mshua umekwapua asubuhiiii.....kiatu hakijui brush...kinajiosha chenyewe kipindi cha mvua....umejipaka mafuta ya rays au yale ya kupikia...unang'aa kama kitumbua
 
Back
Top Bottom