Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Mkuu Sexless , kwanza nikushukuru kwa imani yako kwangu, ni kweli hayo yote yako ndani ya uwezo wangu, na kiukweli sijakwama popote bali ni mipangilio tuu!.

Hili halihitaji uchunguzi, ile ilikuwa ni ajali tuu, ila eneo la Pandambili ni very notorious kwa ajali za ajabu ajabu, sio ajali ya Wangwe tuu , hata Salome Mbatia alipatia ajali eneo hilo hilo na kupoteza maisha!. Mimi mwenyewe nilipatia ajali eneo hilo hilo, nikaponea tundu la sindano!

this is valid

this is valid but very dangerous undertaking

I knows about this, its not true.

Ni ukoo wa kifalme wa Dubai

Hii inaingilia the right to privacy, kama hatukuuliza kwa Nyerere, Mwinyi, Ben, JK na.JPM, why Samia?.

Kuna issues kuhusu asili ya JPM niliiulizia ...

P
Kwahiyo hapa umeshafanya uchunguzi na haya nfo majibu.
 
Huyo bwana ndiye aliyekuwa mhimiri wa kashfa ya Loliondo kabla ya kutolewa Wizara ya Utalii na kupelekwa kuwa RC Singida. Hivi siku hizi yuko wapi huyo Mgumia?


RIP Katabaro.....Namkumbuka sana jinsi alivyokuwa mwandishi mzuri sana na asiye na woga.

Wadau naomba pia mkumbuke jamaa mmoja anaitwa Anthony Ngaiza ambaye aliwahi kuwa editor wa Family Mirror kwenye miaka ya 1992/93 kabla ya kuhamia MCT. Tunahitaji kweli kuwakumbuka hawa jamaa!
 
Nafikiri watu wengi mnakumbuka yule mwandishi wa habari miaka ya themanini na tisini marehemu stan Katabaro,alikuwa ni mwandishi mahiri kwa miaka ya leo hana tofauti na Saed Kubenea,Johnson Mbwambo,nauliza kifo chake kilisababishwa na nini hasa?wanaokumbuka watujuze
UTAWALA WA MWINYI NDO ULIMWONDOA KUTOKANA NA KASHFA YA LOLIONDO. WATOTO WENGI HAWAJUI. HAYA MAMBO.
 
Alikufa ghafla!

Kumfananisha Kubenea na Stan, ni kumpandisha tuu chati Kubenea, Stan alikuwa akiandika investigative journalism kwenye developing story, Kubenea anaandika udaku kwenye medani za siasa, sio uchunguzi in a really sense ya uchuguzi.

Waliotaka kufuata nyanyo za Katabalo, ni This Day na Kulikoni, walioanza, wakati wakifuatilia story ya Rada.
Kubenea ni kweli hawezi vaa viatu vya Stan Katabalo. Stan alikuwa msomi na mwenye misimamo hasa. Kubenea ni mbabaishaji tu.
 
Da! umenikumbusha mbali. ktk makala zake za mwisho aliwahi kuandika kuwa, "Najua nitakufa na kalamu yangu ndio inaniua,lakini ktk vizazi vijavyo watatamani kuona fuvu langu ili atathmini ubongo wangu umekaaje." na kweli leo yametimia...mwana jf amekumbuka mzimu wake... RIP Katabalo
 
Mkuu enzi hizo kulikuwa na heshima ya taaluma zote. Stan Katabalo na Mfanyakazi waliji tofautisha sana kwenye uandishi wake. Mkono wa kifo chake yupo pia Abrahaman Kinana akina JK, Ndolanga and the likes kwa Loliondo Gate.

Mimi naomba tumkumbuke kila tukikumbuka kama mwandishi JASIRI ambaye labda kama hakuwa wa kwanza basi mmoja wa wawili bora.

Nawakumbusha tu miaka ya 60 alitokea mwandishi na mtangazaji mwingine (Marehemu Melek Kangero) alimkosoa sana Mwl. Nyerere akapata life Ban ya ajira kwenye ofisi yo yote ndani na nje ya Tanganyika.

Watawala wetu watateseka sana na ukandamizaji wa Fikra
 
Nakumbuka wakati niko mdogo ingawa nilikuwa najua kusoma na kuandika wakati huo,kulikuwa na kashfa moja kubwa sana iliyoitingisha nchi,kashfa ya loliondo,kipindi hicho kuna mwandishi mmoja alikuwa anaitwa Stan Katabalo,nadhani alikuwa anaandikia gazeti la Mfanyakazi au.....kwa baadhi yenu huyu jamvini aidha mlikuwa wadogo sana au bado kuzaliwa lakini natumai wapo wengi waliokuwa wakubwa na walikuwa wanafuatilia kisa hiki kitakatifu,huyu jamaa mwandishi Stan Katabalo alikuwa anapambana na system na mbaya zaidi alikuwa peke yake katika kutetea masilahi ya nchi yetu,nakumbuka watu kama Ndolanga na wenzake.

Pamoja na Rais wa kipindi kile walikuwa wanahusika sana kwenye ile kashfa ya Loliondo,huyu jamaa mwandishi shujaa huyu alikuja kufa katika mazingira ya ajabu sana na mpaka leo sijasikia hata akienziwa,inauma sana...huyu jamaa alikuwa si tu shujaa bali alifungua njia kwenye tasnia nzima ya investigative journalism hapa nchini,hivi kwanini isianzishwe hata tuzo kwa jina lake?najua kuna watu na viongozi hatapenda kuusoma huu uzi kwa sababu kombe lilishafunikwa na mwanaharamu alishapita but huyu mtu anadeserve heshima ya pekee sana katika suala hili,kwa sababu hizi kashfa zote mnazoziona leo zikiwemo Richmond,IPTL,ESCROW

Sio kwamba zimeanza jana au juzi katika nchi hii,ni tangu kipindi hichoo cha Mwinyi sema tu watu hawakuwa makini kama ilivyo sasa na matokeo yake kwa wale waliokuwa conscious kama Stan Katabalo waliishia kupotezwa kusikojulikana,REST IN PEACE STAN KATABALO, HAKIKA WEWE ULIKUWA JABALI NA MZALENDO HALISI WA NCHI HII.
Umeandika vitu muhimu
 
Nafikiri watu wengi mnakumbuka yule mwandishi wa habari miaka ya themanini na tisini marehemu stan Katabaro,alikuwa ni mwandishi mahiri kwa miaka ya leo hana tofauti na Saed Kubenea,Johnson Mbwambo,nauliza kifo chake kilisababishwa na nini hasa?wanaokumbuka watujuze
Alikuwa kama si mmiliki basi mwandishi wa gazeti la Motomoto. Misukosuko ilimuanzia baada ya kuandika habari kuu mbili kama ifuatavyo;

1. Zanzibar yajiunga na OIC
Hapa Zenji walijiunga bila kushirikishwa Tz bara. Lakini kama kawa, walianza kukana na mwisho ikaja onekana ni kweli. Jamaa akapotezwa

2. Loliondo yauzwa kwa waarabu
Ukiingia kwa Loliondo huku ukiwa na simu, inakukaribisha uarabuni. Yaani upo TZ lakini unakaribishwa uarabuni. Hii iliashilia kwamba Loliondo imeuzwa. Kama kawa, serikali ilikana. Lakini ikaja onekana ni kweli. Jamaa akapotezwa

Mwisho wa siku, gazeti lake likafungiwa milele na yeye "kuuwawa" kimiujiza..!!
 
Alikuwa kama si mmiliki basi mwandishi wa gazeti la Motomoto. Misukosuko ilimuanzia baada ya kuandika habari kuu mbili kama ifuatavyo;

1. Zanzibar yajiunga na OIC
Hapa Zenji walijiunga bila kushirikishwa Tz bara. Lakini kama kawa, walianza kukana na mwisho ikaja onekana ni kweli. Jamaa akapotezwa

2. Loliondo yauzwa kwa waarabu
Ukiingia kwa Loliondo huku ukiwa na simu, inakukaribisha uarabuni. Yaani upo TZ lakini unakaribishwa uarabuni. Hii iliashilia kwamba Loliondo imeuzwa. Kama kawa, serikali ilikana. Lakini ikaja onekana ni kweli. Jamaa akapotezwa
Dah mwamba alikuwa mwamba kweli, Watu kama hawa inabidi wakumbukwe
 
Back
Top Bottom