Nakumbuka wakati niko mdogo ingawa nilikuwa najua kusoma na kuandika wakati huo,kulikuwa na kashfa moja kubwa sana iliyoitingisha nchi,kashfa ya loliondo,kipindi hicho kuna mwandishi mmoja alikuwa anaitwa Stan Katabalo,nadhani alikuwa anaandikia gazeti la Mfanyakazi au.....kwa baadhi yenu huyu jamvini aidha mlikuwa wadogo sana au bado kuzaliwa lakini natumai wapo wengi waliokuwa wakubwa na walikuwa wanafuatilia kisa hiki kitakatifu,huyu jamaa mwandishi Stan Katabalo alikuwa anapambana na system na mbaya zaidi alikuwa peke yake katika kutetea masilahi ya nchi yetu,nakumbuka watu kama Ndolanga na wenzake.
Pamoja na Rais wa kipindi kile walikuwa wanahusika sana kwenye ile kashfa ya Loliondo,huyu jamaa mwandishi shujaa huyu alikuja kufa katika mazingira ya ajabu sana na mpaka leo sijasikia hata akienziwa,inauma sana...huyu jamaa alikuwa si tu shujaa bali alifungua njia kwenye tasnia nzima ya investigative journalism hapa nchini,hivi kwanini isianzishwe hata tuzo kwa jina lake?najua kuna watu na viongozi hatapenda kuusoma huu uzi kwa sababu kombe lilishafunikwa na mwanaharamu alishapita but huyu mtu anadeserve heshima ya pekee sana katika suala hili,kwa sababu hizi kashfa zote mnazoziona leo zikiwemo Richmond,IPTL,ESCROW
Sio kwamba zimeanza jana au juzi katika nchi hii,ni tangu kipindi hichoo cha Mwinyi sema tu watu hawakuwa makini kama ilivyo sasa na matokeo yake kwa wale waliokuwa conscious kama Stan Katabalo waliishia kupotezwa kusikojulikana,REST IN PEACE STAN KATABALO, HAKIKA WEWE ULIKUWA JABALI NA MZALENDO HALISI WA NCHI HII.