Nina week nzima hapa Kahama, nimezunguka maeneo kadhaaa, ni AIBU kwa eneo kama hili lenye mapato makubwa kushindwa kabisa kujenga stand hata moja yenye hadhi.
Inayoitwa stand kuu ni kama zizi la kitimoto, Yaani Mvua kidogo pamejaa tope, Wana Choo ni kichafu na Huduma suni, Yaani unakutana na UTI mlangoni.
Kuna stand inaitwa Dodoma, iko barabara ya kuelekea Wilaya ya Ushetu, hapa sidhani kama kuna hata Choo, na imagine kuna Watu wako getini wanakusanya mapato.
Stand ya TATU iko katikati ya mji, haiko mbali Sana na Ile inayoitwa stand kuu, hapa napo ni uchochoro umegeuzwa kuitwa stand, hapana shading wala hata waiting lounges.
Kahama ilivyokua na mawe wameshindwa hata kumwaga kokoto (changarawe) kupunguza vumbi na tope....
Stand imejaa takataka Tu na kuna wamama wanauza chakula hapo. Hizi stand ukumbuke zinahudumia Mabasi ya Bukoba, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kigoma, Arusha, Dodoma, Dar , na Wilaya nyingine za jirani
View attachment 3286040View attachment 3286041View attachment 3286042View attachment 3286043View attachment 3286042
Tanzania mmerogwa nyie Sio bure aiseee