Ukifuatilia wachangiaji wengi, Kuna tatizo mahala nchi hii.
Ifikie hatua Watanzania tujue nini tunataka kwa wakati gani, aliyofanya Nyerere kwa wakati wake yalikua sahihi kwa wakati huo, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Maguful pia.
Tunatakiwa kujua tunataka nini kwa sisi kujikwamua lakini kutwa nzima watu wanalinganisha serikali zilizopita, unafikiri Kuna Rais atakaa Ikulu na kutulia? Atakua anafanya kama anashindana na mtangulizi wake ilihali alitakiwa kupeleka Tanzania mbele bila kujali nani alifanya nini.
Matokeo yake tunadumaa na kuamini maendeleo ni kumzidi mtangulizi wako.
Tuanze kuilinganisha Tanzania na nchi zilizoendelea, tuangalie mataifa ya ulaya, China na Marekani yako wapi, wanapiga hatua gani za kimaendeleo.
Haya Magenge yetu ni hovyo na yanakua kama laana kizazi hadi kizazi.
Kweli mtu anakaa na kusema fulani kaleta maendeleo sio kama fulani, Tanzania ina maendeleo? Shuwain.