Star Tv wameingia vitani dhidi ya awamu ya sita? Habari ya SSH kuzindua uingiaji maji Stiglers ilirushwa ya mwisho, Alloyce Nyanda atumika

Kwa hiyo ulipewa kazi ya kufuatilia vituo vyote? Wewe ni nani hasa huko?
 
Mkuu umejipa kazi nzito sana. Sijasoma post yako yote ila nahoji uliwezaje kutazama taarifa kwenye tv stesheni zooote kwa wakati mmoja?
Au ndio kazi yako kufatilia haya mambo haya
 
Diallo hataki kujipendekeza tena kwa CCM, kwani anakumbuka awamu ya 5 ilivyomyumbisha.
 
Kikubwa walirusha! Achana na mambo ya kuwa mwishoni au ya kwanza.
Ukienda huko huo unakuwa ni umbea bin ushakunanku!
 
Ndio ndio ndugu mkereketwa......!!! Wananchi hawataki maji wanataka Umeme tulivu.....!! Naona unatafuta ugali wa tumbo lako kwa nguvu kiasi cha kuhatarisha maisha ya watu.....!!!
All in all kikubwa pumzi
 
Hongera Sana Startv kuthubutu kuwa huru. Hizi channel za kusifu tu na kuvisha vilemba (flattery) zinatia kichefu chefu.
 
unahakika au umbea tu?
 
Kwamba ALOYCE NYANDA ndo mmiliki wa star Hadi ajipangie habari ipi itoke,

Acha kusagia watu kunguni.
 
Mimi ningekipongeza hicho kituo maana kama wote wangerusha mwanzoni waliochelewa kuangalia taarifa za habari wasingeipata hiyo habari
 
Nilikuwa naangalia star tv, lakini habari za vibaka wa Geita zikawa na umuhimu kuliko mradi huo wa kihistoria

WANANCHI WAKOSA AMANI GEITA
Habari hii ya mauaji ya kusikitisha walinzi kuchinjwa kujitokeza mara kwa mara ni habari iliyowagusa sana wananchi Geita, Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla. Na raia wanajiuliza vyombo vya dola vimeshindwa kabisa kukomesha mauaji haya ya raia

Mkoa wa Geita ulisemekana kushamiri kwa mauaji ya walinzi huku sababu ya mauaji hayo zikiwa hazijulikani. Hata hivyo, baadaye yalikoma, lakini sasa ni kama yamerejea tena baada ya walinzi watatu kuuawa.
Source : Global TV Online
 
Kwani ilikua lazima hiyo taarifa irushwe ya kwanza au kuna sheria gani ya vyombo vya habari inawalazimu kutoa taarifa za ssh ndio ziwe za kwanza
 
Umeuliza Sababu ni NINI??
 
Mkuu chukua pumzi, una tatizo.
 
Tunakushukuru kwa kutufungua macho, kumbe Star TV siyo bendera fuata upepo, naanza kuipa kipaumbele.
 
Huu no uzandiki na uchonganishi kumchonganisha Samia na Dialo. Kila kituo cha TV kina editorial independence yake, hivyo huku ni kuingilia editorial independence ya Sta TV kulazimisha habari ya Samia lazima iwe ya kwanza.. Tukio lilikuwa live tv zote hivyo sio lazima ku lead na old news. Star TV has all the right to run the newe kwenye segment yoyote or even not to run it al all. Enzi za Blaza, niliwahi kuuliza, Magufuli kutawala kurasa za mbele za magazeti, Je anastahili hata kama hazina impact, au wahariri wanajipendekeza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…