Starehe visiwani ndani ya kisiwa cha Ukerewe, ule ni ulimwengu mwingine

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Wanasema tembea uone
Ilikuwa mwaka 2017, nikifika visiwani Ukerewe nikiwa na project ya UNDP, aisee nilijifunza na kuona maajabu ambayo sikuyatarajia

Ukerewe ni Moja ya wilaya za
mkoa wa Mwanza
Ukewe ni kisiwa ndani kisiwa hicho Kuna visiwa vingine zaidi ya 20

Nilitembelea baadhi ya visiwa kama Goziba, Ghana, Siza, Ukara, Bwiro n.k

Niligundua kule watu wanaishi na watu wanatumia pesa na pesa ipo ya kutosha

Shughuli kuu kule ni uvuvi na kula bata

Starehe zote zipo,

Hakuna doria, yaani serikali hawafiki, hakuna wizi, ujambazi wala tatizo lolote,

Kule ni amani na bata tu

Kuna matajiri wanapiga pesa nyingi, unakuta mtu anamiliki mitimbwi zaidi ya 100 amewapa vijana ni kuingia ziwani na kutoka na samaki kupima na kula bata

Ukiambiwa warembo, hawa ndo wamejaa huko yani utake Mganda , Mnyarwanda, kabila zote zipo
Ni wewe tu kujilia unachotaka

Beer zinanywewa full time

Asubuhi ni ugali na sato, kule chakula huulizi ukikuta msosi unakula tu

Kingine kwenye hivo visiwa mtu akifa Huwa hawaziki wanadhani kwamba kisiwa kitajaa makaburi wakose pa kuishi badala yake huwa wanatupa mwili ziwani na bila shaka kuwa chakula cha mamba na Sangara

Visiwani hasa huko Ukara watu hufuga mamba, na mamba anaheshimika na ni mifugo ya watu

Chatu, ni marufuku kumuua Chatu
Wanaamini Chatu hana madhara na Kwa kuwa hana sumu na ni kiumbe mzuri, kwaiyo visiwani utapishana na Chatu ila hana shida yoyote
Chatu wa visiwani hula sana mbwa na kondoo

Biashara zipo zote
Biashara zinakesha, kule visiwani Kuna maduka makubwa tu

Nawaasa vijana maisha sio mpaka Dar es salaam ukipeleka bidhaa zako visiwani Ukerewe utapata ukwasi usio wa kawaida

Fika Ukerewe visiwani uone maajabu
 
Story zako Zina kahawa nyingi.


Hiki ni kisiwa cha Goziba kipo mkoa wa Kagera. Hao watafiti wako wa UNDP nina mashaka nao, askari wa hapo wanatoka Kagera sio mwanza kwa maana ya ukerewe. Nina mashaka na taarifs yako kuwa hakuna doria kama askari wapo.





Punguza uongo ktk maandiko yako mengi unayoandika. Yana uongo mwingi usio na maana
 
Ana story nyingi za kusikia na sio uhalisia wake. Kifupi Hana taarifa kamili kuhusu hiko kisiwa na huo mradi labda alishiliki akiwa ngara na sio ukerewe.
Mnapenda ubishi
Yaani me nisipajue Ukerewe na nimekuweponkwa miaka miwili dogo
 
Nakazia,anajua huko kafika yeye tu
 
Huwa natamani kufika Namagondo na sehemu zingine zilizorejelewa katika kazi nyingi za Euphrase Kezilahabi. Dhana ya uduara, ukatikati na ukitovu pamoja na maji zinabeba mhimili mkuu wa falsafa ya Kezilahabi kuhusu maisha; na zote zinatokana na mazingira ya kisiwani Ukerewe alikokulia.

Siku moja nitafanya utalii wa ndani huko!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…