MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nadhani ni wakati sahihi kwa watanzania wote waliowahi kumlaumu Nape kuhusu kampuni ya Starlink kumuomba msamaha na kuungama makosa yao. Hawakufanya vyema. Pamoja na mapungufu yake ni kuwa Mheshimiwa Nape aliona mbali katika hili.
Ndani ya muda mfupi sana wananchi wa Zambia wameshaanza kulalamika na kuitupia lawama kampuni ya Starlink kuhusu huduma zao za internet. Mheshimiwa Nape alivyosema Starlink wawe na ofisi ndani ya Tanzania alikuwa sahihi 100%. Leo hii wazambia wanalalamikia kupigwa na watu wa kati wanapotaka huduma ya internet za Starlink kutokana na wao kutokuwa na ofisi. Dish & Router ambazo ukiagiza ni $500 kuna wahuni wanauza $1000 huku kifurushi cha mwezi kikiwa $110.. ni maumivu makali. Pia wananchi wamelalamikia usumbufu wa kuagiza Starlink kit moja kwa moja kutoka USA ambapo huchukua hadi wiki 4 kuwafikia huku vikiwa bei ghali sana kuliko matarajio ya wengi.
Baadhi ya wananchi wameenda mbali kwa kudai Starlink sio ya mwananchi wa kawaida. Itawanufaisha wafanyabiashara tu. Kitu pekee ambacho kwa pamoja tunakubali ni kasi ya internet ya Starlink. Haina mpinzani. 120 Mbps ni kubwa sana. Nchi ya Rwanda inayosifika kwa kasi ya internet ina 50 Mbps tu. Kimsingi biashara na beberu haimjali mwananchi wa kipato cha chini. Kuna mwananchi mmoja kauziwa Stalink Kit kwa kwacha 21500.
USHAURI KWA NAPE; Ninamsihi akae chini na timu yake na kushusha bei za vifurushi. Sioni sababu yoyote kwa nchi yetu yenye watumiaji wengi wa internet kuuza vifurushi kwa bei ya kupaa. Hadi leo hii hakuna utetezi wowote wenye maana uliowahi kutolewa na Nape zaidi ya kusema internet kwa Tanzania ni bei rahisi kulinganisha na nchi zingine. Ni UTETEZI WA KITOTO SANA. Kuhusu ni kuwa Starlink hawana namna ya kuikwepa Tanzania. Hii nchi ina biashara kubwa ya internet kuliko majirani zetu. Starlink lazima atarudi tena au kimyakimya anaendelea na mazungumzo ili afanye biashara hapa.