Starlink yawasilisha maombi ya leseni kwa TCRA. Je, safari hii watatoboa? Ushindani wa gharama na ubora wa internet utakuwaje?

Haya mkuu, wenye JF yao wameunganisha mada yako na huna la kuwafanya 😂
 
Ije tuu, natumia zaidi ya 250,000 ya bundle Airtel kila mwezi na mtandao wao uko ovyo.
 
Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo? Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga
hata zisipopungua, bora kutumia internet yao ambapo una uhakika wa faragha wa mambo yako kuliko hawa kenge wa sasa
 
Inabidi wawanyooshe na hawa voda uchwara
 
Ndio hapo kwenye simu yako itakuwa inasoma 100Mbps.. hadi 220 Mbps..
Sasa kuna Mtanzania gn anayeweza kufanya shughuli ipi itakayomfanya kifaa chake kionyeshe 100mbps?
Mm tangu nimenunua simu n mara moja tuu niliona 11mbps kwenye simu yangu na hapo nilikuwa nadownload movie kupitia wifi yenye speed ya 70mbps, ila mara nyingi kwenye hy hy wifi hua nachezea kwenye 6mbps
 
kununua vifaa ni KSH 88K = 1.7M

hiyo 130k ni basic plan😂

kuna mkenya nilimsikia anasema bora zuku tu
Hapana Sio kweli..

Kununua Vifaa Ni KSH 27K (Kwa Rate ya Sasa hivi ya 20= 540,000/= TSH)

Na Basic Plan ni 4000 KSH ambayo ni sawa na Tsh 80k
Na Unlimited Ni 6500 KSH ambayo ni Hiyo 130k TSH..

Ushahidi hapa Chini Japo nilitoka Kenya Juzi kati bei Unaweza Ukapata kwa Bei ya Chini zaidi ya Hapo kama Wewe Ni Mjanja mjanja wa Kanairo pale..

CC: mshamba_hachekwi
Vincenzo Jr


 
nenda website yao uone

au ingia youtube kuna wakenya kibao wame-review
Ipo hivi ndugu Kuna min kit na hard kit normal kwa rate ya pesa ya kibongo ni 936,000 Tsh (Kidishi) - Unaweza connect device 235, na inashika umbali wa mita 297.

Hii ni Min kit
560,000 Tsh (Kidishi) - Unaweza connect device 128, na inashika umbali wa mita 112. Na inaweza kupungua ikija kwa pesa ya kibongo hii zote nimetoa kwenye website Yao ya starlink Kenya
 
hapo itafaa

niliona May wanasema 88k itakua wamepunguza

na hua wana toa punguzo la 55% mara nyingine, mseleleko upo
 
Bei rafiki sana hii mda si mrefu naivuta kwenye la casa yangu hapa kigamboni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…