Starlink yawasilisha maombi ya leseni kwa TCRA. Je, safari hii watatoboa? Ushindani wa gharama na ubora wa internet utakuwaje?

Labda ataleta ushindani maana hii mitandao ya simu bando bei kubwa alafu speed mwendo wa kobe
Ushindani utoke wapi wakati kuna bei elekezi ? Unajua watu hatujui tatizo (ugonjwa) hivyo lawama tunapelekea kwingine na tunachodhani ni tiba kumbe sio TIBA..., Tiba ni kuondoa Serikali na TCRA iachane kabisa na hii mitandao yenyewe ijivinjari kwenye free market...

 
Starlink inalenga wateja wa kati na wakubwa labda sababu kuu gharama za kulipia kwa mwezi kama unavyojuwa wa Tz wengi na wakujiunga na vifurushi vya alfu alfu na mtu anazima na kuwasha data chafya. Ila wale wenye kuweka Wi-Fi majumbani hapo litakuja bei na quality vitaamua. Kwa sisi wateja option zikiwa nyingi nafuu kwetu.
 
Star link wana offer internet yao kupitia kit zao kama Router na sio direct kwenye simu kama mitandao ya simu
Sasa sijui mvua likishuka huko na wingu litanda bado unapata link?
 
Itakuwa mbinde! Huenda Wabunge na Mawaziri ni shareholders wa mitandao yetu ya simu-Tigo,Voda,nk
Sasa waje kukubali itakuwa mbinde maana itaathiri mitandao hiyo na mapato yatashuka.
Washushe bei tu mbona tuna ma bus, SGR na ndege na watu wanapanda zote.
 
Sio ghali sana hapo tu Kenya imeenea Kila Kona kit Yao yote ni laki tatu tu Unlimited kwa mwezi 135,000 (Nyumbani)

▪️Unlimited lite kwa mwezi 83,000 (Nyumbani one location)

▪️GB 50 kwa mwezi - 30,000
Mbona hata hapa unapata kit laki 3 unlimited mpaka laki kwenye hii mitandao yetu.
 
Starlink atakusaidia nyumbani lakini sio kwenye simu ukiwa nje huko na mishemishe zako.
Kwa sasa bado sijaona kama Starlink itakuwa feasible kwa sisi wazee wa kukaa majumbani masaa machache..

Binafsi nitaendelea kukomaa na Airtel Router.

 
Sidhani kama itakuwa na unafuu wowote kwa sababu mamlaka ya mawasiliano ina sheria ngumu sana za kuongoza hawa watoa huduma, rejea mitandao ya simu hakuna kifurushi cha tofauti kati ya mtandao na mtandao watumaji wanacho bakiwa nacho ni kuchagua mtandao unao wafikia kwa ufasaha ila kwenye garama vyote vinafanana.
So hata hawa Starlink kodi na sera zetu za regulation zita wabana wata kuwa na tofauti kidogo mno ambayo kwa hesabu za chap hazina unafuu wowote. Muda ni msema kweli tutakuja tembelea huu uzi na wakilisha wadau.
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo la kukaribisha maoni ya wananchi kuhusu maombi ya leseni ya kampuni ya Starlink inayotoa huduma za mawasiliano ya intaneti.

Hatua hiyo inaashiria kuwa Starlink ambayo inamiliki na bilionea namba moja duniani, Elon Musk, huenda ikaanza kutoa huduma hapa nchini endapo wananchi wataridhia ipewe leseni.

Najiuliza kipindi vodacom, na mita dao mingine wanakuja mliombwa maoni?


Mkipandishaga bei za vifurushi huwa mnawaomba wananchi maoni?

Ni lini ambapo muwekezaji alikua wananchi wakaombwa maoni kwanza?

 
Starlink atakusaidia nyumbani lakini sio kwenye simu ukiwa nje huko na mishemishe zako.
Mishemishe zote za kazi nafanyia nyumbani, nikitoka nje bundle la simu linatosha kwa matumizi tuu madogo madogo ya kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…