Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haitawezekana aisee. Serikali haitaki kulegeza maisha ya wananchi.Afadhali, hawa wanaotulima bei za bando wapate ushindani, walegeze kidogo ...
Ushindani utoke wapi wakati kuna bei elekezi ? Unajua watu hatujui tatizo (ugonjwa) hivyo lawama tunapelekea kwingine na tunachodhani ni tiba kumbe sio TIBA..., Tiba ni kuondoa Serikali na TCRA iachane kabisa na hii mitandao yenyewe ijivinjari kwenye free market...Labda ataleta ushindani maana hii mitandao ya simu bando bei kubwa alafu speed mwendo wa kobe
Starlink inalenga wateja wa kati na wakubwa labda sababu kuu gharama za kulipia kwa mwezi kama unavyojuwa wa Tz wengi na wakujiunga na vifurushi vya alfu alfu na mtu anazima na kuwasha data chafya. Ila wale wenye kuweka Wi-Fi majumbani hapo litakuja bei na quality vitaamua. Kwa sisi wateja option zikiwa nyingi nafuu kwetu.Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo?
Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga,
View attachment 3152628
Meanwhile hivi ndivyo voda na wenzake walivyo sasa hivi
=====
Baada ya muda mrefu wa Watanzania kuhoji kwanini Tanzania hatujaruhusu uwepo wa Internet ya Starlink kutoka kwa tajiri Elon Musk, hatimaye leo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo kuonesha Kampuni hiyo imeomba kupatiwa leseni ya Kitaifa ya Miundombinu na Leseni ya Kitaifa ya Huduma ya Mifumo Tumizi.
Kwa muda mrefu Wananchi wamekuwa wakihoji kwanini Tanzania hatuna huduma hii na hasa ukizingatia kwa wenzetu majirani wanayo; Je, kwanini Tanzania hatupati huduma ya starlink nini shida?
Wakati hapa kwetu kumekuwa na kususua kupokea huduma hii wananchi wakihoji kwanini: Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?
Katika moja ya fafanuzi zake, aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti, hivyo ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.
Na haya yalikuwa majibu ya Nape, kuwa serikali haikuwa imeweka vikwazo vyovyote ila bwana Elon hakuwa na mpango wa kuanzicha huduma hiyo nchini: Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania
Hata hivyo, Februari mwaka huu, akiwa bado Waziri, Nape Nnauye alisema Kampuni hiyo inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa huduma nchini. Aliongeza kuwa ikishatimiza taratibu zote itaanza kutoa huduma na kwamba Serikali inasubiri wakamilishe tu taratibu hizo.
Sasa hivi Kampuni hiyo imeomba leseni tena na TCRA kwa sasa imeweka wazi kabisa uombaji huo tofauti na awali ambapo haikuwa wazi. Sasa maswali ya kujiuliza ni
- Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo? Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga
- Je, sasa hivi amekubali kujenga ofisi au ile ilikuwa janja janja ya kipindi kile?
🌜Kama Wana vigezo watapewa leseni pasi na shaka
Duuuh kama installation cost ni 1.7m basi bora tukamuliwe tu na hawa ma-CARTEL.kununua vifaa ni KSH 88K = 1.7M
hiyo 130k ni basic plan😂
kuna mkenya nilimsikia anasema bora zuku tu
Jerry kawaita Bwana yule alieenguliwa aliwatimuani kweli au ukajanja tu
Sasa sijui mvua likishuka huko na wingu litanda bado unapata link?Star link wana offer internet yao kupitia kit zao kama Router na sio direct kwenye simu kama mitandao ya simu
Washushe bei tu mbona tuna ma bus, SGR na ndege na watu wanapanda zote.Itakuwa mbinde! Huenda Wabunge na Mawaziri ni shareholders wa mitandao yetu ya simu-Tigo,Voda,nk
Sasa waje kukubali itakuwa mbinde maana itaathiri mitandao hiyo na mapato yatashuka.
Mbona hata hapa unapata kit laki 3 unlimited mpaka laki kwenye hii mitandao yetu.Sio ghali sana hapo tu Kenya imeenea Kila Kona kit Yao yote ni laki tatu tu Unlimited kwa mwezi 135,000 (Nyumbani)
▪️Unlimited lite kwa mwezi 83,000 (Nyumbani one location)
▪️GB 50 kwa mwezi - 30,000
Starlink atakusaidia nyumbani lakini sio kwenye simu ukiwa nje huko na mishemishe zako.Ije tuu, natumia zaidi ya 250,000 ya bundle Airtel kila mwezi na mtandao wao uko ovyo.
Elon MuskSijaelewa hapo kampuni ya Starlink Satellite Tanzania ina hisa 1%, who owns the rest?
Kwa sasa bado sijaona kama Starlink itakuwa feasible kwa sisi wazee wa kukaa majumbani masaa machache..Starlink atakusaidia nyumbani lakini sio kwenye simu ukiwa nje huko na mishemishe zako.
Mishemishe zote za kazi nafanyia nyumbani, nikitoka nje bundle la simu linatosha kwa matumizi tuu madogo madogo ya kawaidaStarlink atakusaidia nyumbani lakini sio kwenye simu ukiwa nje huko na mishemishe zako.