Starlink yawasilisha maombi ya leseni kwa TCRA. Je, safari hii watatoboa? Ushindani wa gharama na ubora wa internet utakuwaje?

Lazima watapelekwa kwenye rates zetu. Kuna taasisi moja iliundwa kwa ushirika na nchi za Ulaya, walikuwa na mpango wa kulipa mishahara minono kama ya Ulaya. Wizara ya fedha ikakataa, ikataka walipwe kwa ngazi za Tanzania. The same happened kwa TBL wakati inabinafsishwa kwa ubia.

Last time walipewa sharti wawe na ofisi Tanzania, may be mambo ya kodi, na kufanikisha udukuzi
Vigumu Sana Kumdukua Elon musk
 
Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo?

Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga,

View attachment 3152628
Meanwhile hivi ndivyo voda na wenzake walivyo sasa hivi​

=====

Baada ya muda mrefu wa Watanzania kuhoji kwanini Tanzania hatujaruhusu uwepo wa Internet ya Starlink kutoka kwa tajiri Elon Musk, hatimaye leo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo kuonesha Kampuni hiyo imeomba kupatiwa leseni ya Kitaifa ya Miundombinu na Leseni ya Kitaifa ya Huduma ya Mifumo Tumizi.

Kwa muda mrefu Wananchi wamekuwa wakihoji kwanini Tanzania hatuna huduma hii na hasa ukizingatia kwa wenzetu majirani wanayo; Je, kwanini Tanzania hatupati huduma ya starlink nini shida?

Wakati hapa kwetu kumekuwa na kususua kupokea huduma hii wananchi wakihoji kwanini: Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?

Katika moja ya fafanuzi zake, aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti, hivyo ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.

Na haya yalikuwa majibu ya Nape, kuwa serikali haikuwa imeweka vikwazo vyovyote ila bwana Elon hakuwa na mpango wa kuanzicha huduma hiyo nchini: Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania

Hata hivyo, Februari mwaka huu, akiwa bado Waziri, Nape Nnauye alisema Kampuni hiyo inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa huduma nchini. Aliongeza kuwa ikishatimiza taratibu zote itaanza kutoa huduma na kwamba Serikali inasubiri wakamilishe tu taratibu hizo.

Sasa hivi Kampuni hiyo imeomba leseni tena na TCRA kwa sasa imeweka wazi kabisa uombaji huo tofauti na awali ambapo haikuwa wazi. Sasa maswali ya kujiuliza ni

  1. Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo? Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga
  2. Je, sasa hivi amekubali kujenga ofisi au ile ilikuwa janja janja ya kipindi kile?
Sasa Hivi bila Kupata baraka za Elon huongei na Trump, mama Samia kaona asiponzwe kuja kukosa misaada kisa kumkazia Elon...Elon is unstoppable force kwa sasa 🤫
 
Starlink ni speed ya 5G, ni zaidi ya 100Mbps..
Ambayo hiyo Mbs ni sawa na zile zinazo andikwa kwenye simu kama hiyo M/s? Nikimaanisha 100Mbps itasomeka gapo kwenye mshale?
Screenshot_20241115-100048.png
 
Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo?

Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga,

View attachment 3152628
Meanwhile hivi ndivyo voda na wenzake walivyo sasa hivi​

=====

Baada ya muda mrefu wa Watanzania kuhoji kwanini Tanzania hatujaruhusu uwepo wa Internet ya Starlink kutoka kwa tajiri Elon Musk, hatimaye leo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo kuonesha Kampuni hiyo imeomba kupatiwa leseni ya Kitaifa ya Miundombinu na Leseni ya Kitaifa ya Huduma ya Mifumo Tumizi.

Kwa muda mrefu Wananchi wamekuwa wakihoji kwanini Tanzania hatuna huduma hii na hasa ukizingatia kwa wenzetu majirani wanayo; Je, kwanini Tanzania hatupati huduma ya starlink nini shida?

Wakati hapa kwetu kumekuwa na kususua kupokea huduma hii wananchi wakihoji kwanini: Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?

Katika moja ya fafanuzi zake, aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti, hivyo ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.

Na haya yalikuwa majibu ya Nape, kuwa serikali haikuwa imeweka vikwazo vyovyote ila bwana Elon hakuwa na mpango wa kuanzicha huduma hiyo nchini: Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania

Hata hivyo, Februari mwaka huu, akiwa bado Waziri, Nape Nnauye alisema Kampuni hiyo inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa huduma nchini. Aliongeza kuwa ikishatimiza taratibu zote itaanza kutoa huduma na kwamba Serikali inasubiri wakamilishe tu taratibu hizo.

Sasa hivi Kampuni hiyo imeomba leseni tena na TCRA kwa sasa imeweka wazi kabisa uombaji huo tofauti na awali ambapo haikuwa wazi. Sasa maswali ya kujiuliza ni

  1. Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo? Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga
  2. Je, sasa hivi amekubali kujenga ofisi au ile ilikuwa janja janja ya kipindi kile?
Woyowoyowoyawoyo!
 
Mwanzo kipindi starlink inaingia kenya mapokeo yalikua makubwa kwa vile price ya vifurushi ilikua cheap ukilinganisha na internet service provider wengine

Competition ikawa kubwa baina ya starlink na safaricom ( router) . Hali iliofanya wateja kuihama safrcom. Ndipo safaricom ikaingia ubia na starlink sahvi ndo distributor wakubwa wa hizo device kupitia mawakala wao
 
Watatoboa kwa sababu musk kwa sasa ni sehemu ya serikali huko Amerika,
Nani mwenye mbavu za kumpa vikwazo kwenye biashara yake na akiangalia mnawategemea kwa mambo kibao
Nadhani ameomba tena kwa mara nyingine makusudi tu ili aone huwenda kuna dharau zilionyeshwa
 
Back
Top Bottom