Starlink yawasilisha maombi ya leseni kwa TCRA. Je, safari hii watatoboa? Ushindani wa gharama na ubora wa internet utakuwaje?

Starlink yawasilisha maombi ya leseni kwa TCRA. Je, safari hii watatoboa? Ushindani wa gharama na ubora wa internet utakuwaje?

Niliona crdb pale kigamboni wameweka hii sema walikuwa wanatumia kwa Siri sana😃😀😀😀😀
We Umewachoma Wazi 🤣🤣
Huoni kama Utawafanya Washitakiwe kwa Matumizi ya Bidhaa zilizokatazwa 🤣🤣🤣

Maana Mpaka Sasa Bado haziruhusiwa Kuna Wale watu walikula Mvua na Wazungu wao kwa matunzi ya Hizo starlink...
Utawacosts 🤣🤣🤣
 
Naunga mkono hoja mkuu 😀 😃
20241115_081743.jpg

Hawa wajinga wametutesa sanaaa
 
Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo?

Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga,

View attachment 3152628
Meanwhile hivi ndivyo voda na wenzake walivyo sasa hivi​


=====

Baada ya muda mrefu wa Watanzania kuhoji kwanini Tanzania hatujaruhusu uwepo wa Internet ya Starlink kutoka kwa tajiri Elon Musk, hatimaye leo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo kuonesha Kampuni hiyo imeomba kupatiwa leseni ya Kitaifa ya Miundombinu na Leseni ya Kitaifa ya Huduma ya Mifumo Tumizi.


Kwa muda mrefu Wananchi wamekuwa wakihoji kwanini Tanzania hatuna huduma hii na hasa ukizingatia kwa wenzetu majirani wanayo; Je, kwanini Tanzania hatupati huduma ya starlink nini shida?

Wakati hapa kwetu kumekuwa na kususua kupokea huduma hii wananchi wakihoji kwanini: Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?

Katika moja ya fafanuzi zake, aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti, hivyo ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.

Na haya yalikuwa majibu ya Nape, kuwa serikali haikuwa imeweka vikwazo vyovyote ila bwana Elon hakuwa na mpango wa kuanzicha huduma hiyo nchini: Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania

Hata hivyo, Februari mwaka huu, akiwa bado Waziri, Nape Nnauye alisema Kampuni hiyo inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa huduma nchini. Aliongeza kuwa ikishatimiza taratibu zote itaanza kutoa huduma na kwamba Serikali inasubiri wakamilishe tu taratibu hizo.

Sasa hivi Kampuni hiyo imeomba leseni tena na TCRA kwa sasa imeweka wazi kabisa uombaji huo tofauti na awali ambapo haikuwa wazi. Sasa maswali ya kujiuliza ni

  1. Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo? Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga
  2. Je, sasa hivi amekubali kujenga ofisi au ile ilikuwa janja janja ya kipindi kile?
Serikali ya CCM wanapenda kuona watanzania wakiteseka ndio maana hawataki kumuachia Musk aje kushusha gharama za internet na kuboresha huduma. Watawala wa nchi wana mambo ya kiquma sana
 
Haina shida leseni washapewa kaka 😀😃😃😃😃😃

kwani lesseni Tayari Wamepewa starlink??

Ila hata kama Serkali ikiamua Kukusagia kunguni Kisheria wao walianza Matumizi Kabla ya Leseni kutoka..
So wanahesabika Ni makosa..

Maana tunaanza kuhesabu lini Wameanza kutumia Na Lini leseni imeanza Kutumika
 
kwani lesseni Tayari Wamepewa starlink??

Ila hata kama Serkali ikiamua Kukusagia kunguni Kisheria wao walianza Matumizi Kabla ya Leseni kutoka..
So wanahesabika Ni makosa..

Maana tunaanza kuhesabu lini Wameanza kutumia Na Lini leseni imeanza Kutumika
Nakumbuka Kuna wachina walibebwa aisee 😀😃😃😃 hivi ulisikia nao Qatar airways wamefungwa kwenye ndege zao hizi starlink
 
Tatizo watu hawajui Bei ya Bundle inatokana na nini..., Sio kweli kwamba waliopo ndio wanasababisha bei kuwa juu.. HAPANA Serikali na TCRA waliweka bei elekezi hence kuondoa ushindani na wote kuchezea kwenye Bei elekezi

Huoni kwamba kwa mitandao kuona hilo sasa hivi wanapush watu wanunua router (wireless) yenye unlimited kwa kupitia mgongo kwamba ni Biashara... Kwahio kikulacho ki nguoni mwako (hata akija malaika na Internet) kama TCRA ameweka bei elekezi basi bei itachezea palepale..., Kuna wakati enzi za ushindani mitandao ilikuwa inatoa bundle bure (kama motisha) let alone bei ya juu

 
Back
Top Bottom