Nimenunua king'amuzi dar cha 34000 nikaja nacho zenji hakioneshi channel ata moja,hakina ata mwezi mmoja na nusu na kina ofa yangu ya miezi 7.5,nilipowapigia huduma kwa wateja wakanielekeza niende kweny ofisi zao zilizopo apa zanzibar/mlandege,nilipofika wakanambia ni kweli kwa aina ya kingamuzi nlichopewa hakiwezi kuonesha zanzibar kwasababu minara yake haipo ambayo ni T2 km ckosei,nkawaomba wanibadulishie basi maana ndo utaratibu ulivo,lakini nliwashangaa walipotaka niwape na pesa ambayo ni sawa na ile ya kingamuzi kipya uku wakijidai ndo wananibadilishia.
Nilipowauliza iyo pesa yote ya nini na wakati nna warranty ya mwaka mzima wakadai eti ni ya vocha,nkawaambia mimi ctaki iyo vocha yenu ya 30000 coz icho kinhamuzi changu bafo kina ofa ya kutosha tu,kutoa elfu 30 tn ni sawa unaniuzia kingamuz kingine na sio kunibadilishia uko,mtoa huduma akanambia ndio utaratibu ulivo,nkaona huu ni utapeli tu na hii kampuni haiko makini katika kuwasaidia wateja bali kuwaibia tu,ilibidi nidai kingamuzi changu niondoke maana siku ya kwanza naenda ofisini kwao waliniomba nikiache ili waniombee cha kureplace tn waliniambia kwa tatizo langu ctotakiwa kulipia tena,but nlishangaa nliporudi tena wale vijana wamenigeukia,nusu nimrambe mtu makofi.
Wadau ebu mnaoijua hii kampuni kinagaubaga,hili langu limekaaje,mi ctaki icho kifurushi chao cha 30 elfu coz cha kwanza ni 34 elfu sas apo c bora kununua kipya tu hlf ukawa na viwili kuliko kutoa 30 elfu hlf na kile kingine unawaachia eti wamekubadilishia,apa wamebadilisha au wamekuuzia kingine?NAWASILISHA na kama wahusika mmo humu naomba muongozo.