Mleta uzi alihitaji kujua kwa nini J5 ya majivu na sio J4,J3 au Alhamisi? Wewe naona umetoka nje ya uzi kabisa, unaleta udini. Hapa ndipo lilipo tatizo kubwa la Watanzania.Utaongea utatoka mishipa yote kanisa Ni moja Takatifu katoliki la mitume likisema Leo Ni Kwaresma, au pasaka wote itakuea hivyo. Na ndivyo ilivyo. Hakuna calendar tofauti wamejaribu hao kina sabbato wameshindwa wamebakia wenyewe the whole world wapo na kanisa moja ambalo Ni Takatifu katoliki la Mitume
shukrani sana .Swali: "Nini maana ya nguo ya magunia na majivu?"
Jibu: Nguo ya magunia na majivu yalitumiwa katika nyakati za Agano la Kale kama ishara ya kushusha hadhi, maombolezo, na / au toba. Mtu anayetaka kuonyesha moyo wake wa kutubu mara nyingi huvaa nguo ya magunia, kukaa katika majivu, na kuweka majivu juu ya kichwa chake. Nguo ya magunia ilikuwa nyenzo isiyo laini ambayo kawaida hutengenezwa kwa nywele nyeusi za mbuzi, na kuifanya isio na raha kabisa kuivaa. Majivu yalionyesha majonzi na maangamizi.
Mtu alipopokufa, tendo la kuvaa nguo ya magunia lilionyesha huzuni kubwa kwa kupoteza mtu huyo. Tunaona mfano wa hili wakati Daudi aliomboleza kifo cha Abneri, jemadari wa jeshi la Sauli (2 Samweli 3:31). Yakobo pia alionyesha huzuni yake kwa kuvaa nguo ya magunia wakati alidhani mwanawe, Yusufu, alikuwa ameuawa (Mwanzo 37:34). Matukio haya ya maombolezo kwa wafu hutaja nguo za magunia lakini si majivu.
Mjivu yaliambatana na nguo ya magunia katika nyakati wa msiba wa kitaifa au kutubu kutoka kwa dhambi. Esta 4:1, kwa mfano, inaelezea Mordekai akirarua nguo zake, akivaa nguo ya magunia na majivu, na kuingia mjini "akilia kwa sauti kubwa na kwa uchungu." Hili ndio lilikuwa jibu la Mordekai kwa tangazo la Mfalme Ahasuero kutoa mamlaka kwa Hamani dhaifu kuharibu Wayahudi (tazama Esta 3:8-15). Mordekai sio peke yake ambaye aliomboleza. "Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu "(Esta 4:3). Wayahudi wakajibu habari haribifu kuhusu mbio zao na nguo ya magunia na majivu, kuonyesha huzuni kali sana na dhiki.
Nguo ya magunia na majivu pia hutumika kama ishara ya umma ya toba na unyenyekevu mbele ya Mungu. Wakati Yona aliwaambia watu wa Ninawi kwamba Mungu angeenda kuwaangamiza kwa sababu ya uovu wao, kila mtu kutoka kwa mfalme hadi kwa raia wa chini kabisa alijibu kwa toba, kufunga, na nguo ya magunia na majivu (Yona 3:5-7). Waliweka nguo ya magunia hata kwenye wanyama wao (mstari wa 8). Mawazo yao yalikuwa, "Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?"(mstari wa 9). Hii ni ya kushangaza kwa sababu Biblia haisemi kamwe kwamba ujumbe wa Yona unahusisha kutaja kwokwote kwa huruma ya Mungu; lakini rehema ndio waliyopokea. Ni wazi kwamba uvaaji wa nguo ya magunia na majivu kwa watu wa Ninawi haikuwa maonyesho yasio na maana. Mungu aliona mabadiliko ya kweli-mabadiliko ya unyenyekevu ya moyo yaliyowakilishwa na nguo ya magunia na majivu-na ilisababisha Yeye "kuacha" na kutoleta mpango Wake wa kuwaangamiza (Yona 3:10).
Watu wengine Biblia inataja walivaa nguo ya magunia ni pamoja na Mfalme Hezekia (Isaya 37:1), Eliakimu (2 Wafalme 19:2), Mfalme Ahabu (1 Wafalme 21:27), wazee wa Yerusalemu (Maombolezo 2:10), Danieli (Danieli 9:3), na mashahidi wawili katika Ufunuo 11:3.
Kwa urahisi sana, nguo ya magunia na majivu yalitumiwa kama ishara ya nje ya hali ya ndani ya mtu. Ishara kama hiyo ilifanya mabadiliko ya moyo wa mtu kuonekana na kuonyesha uaminifu wa huzuni na/au toba. Haikuwa tendo la kuvaa nguo ya magunia na majivu yenyewe ambayo yalimshawishi Mungu kuingilia kati, lakini unyenyekevu kwamba hatua kama hiyo imeonyeshwa (angalia 1 Samweli 16:7). Msamaha wa Mungu kwa mjibu wa toba ya kweli husherehekewa na maneno ya Daudi: "Ulinivua nguo ya magunia, ukanivika furaha" (Zaburi 30:11).
Kwa taarifa tu yaliwahi kuwa mawili La Rome na Ufaransa. Soma historian ya kanisa.Tatizo ni pale unapotaka kutuaminisha kama hao waleta hiyo dini walivyotaka. Imani yangu ya katoliki inaniambia kuwa niamini hivi; KANISA TAKATIFU KATOLIKI LA RUMI. Hii inamaana walitaka, hata kukitokea Katholiki nyingine, tusikubaliane nalo. Tuweke imani na mafundisho yetu mahali pamoja ili tusilishwe matango pori huko.
Safi sana. Sasa soma vizuri nilichoandika. Nilisema; Tulionywa mapema kabla kuwa Endapo kutatokea Kanisa Katoliki lingine nje ya Rome; Tusilikubali. Hata wawepo mapapa 10. Papa ni mmoja tu, aliyeko pale Roma baaaasiiiiiKwa taarifa tu yaliwahi kuwa mawili La Rome na Ufaransa. Soma historian ya kanisa.
Kulikua na mapapa wawili...
Kwanini ifuatwe Amri za kabisa badala ya Amri za mungu?Lakini amri ya pili ya kanisa inasema " funga siku ya jumatano ya majivu na usile nyama siku ya ijumaa kuu" na sio kufunga kwaresma yote
Sent using Jamii Forums mobile app
Jumatano ya.majivu inatoka kitabu gani?Amri maana yake ni lazima siku hizo kufanya hivyo haimaanishi siku zilizobaki za kwaresma usifunge,kwa maana ya kwamba kama unaona huwezi kabisa kufunga kwaresma nzima basi jumatano ya majivu ujitahidi maana ni lazima.
Sent using Jamii Forums mobile app
NISAIDIE MAANA HALISI YA MANENO HAYA:Utaongea utatoka mishipa yote kanisa Ni moja Takatifu katoliki la mitume likisema Leo Ni Kwaresma, au pasaka wote itakuea hivyo. Na ndivyo ilivyo. Hakuna calendar tofauti wamejaribu hao kina sabbato wameshindwa wamebakia wenyewe the whole world wapo na kanisa moja ambalo Ni Takatifu katoliki la Mitume
Wakristo tunafunga siku 40! Sasa basi cku ya jpili huwa Hakuna kufunga kwani ni cku ya bwana! Sasa kwa wiki tunafunga cku 6 (ukitoa kila jumapili ambayo hatufunahi) ukichukua majuma 6 tunayofunga unapata siku 36! Sasa ili zikamilike cku 40 ndio unaanza j5 ya majivu mpaka jmos kuna cku 4! Sasa unajumlisha cku 36 na siku 4 ndio unapata cku 40! Lkn kama ingekuwa tunafunga mpaka jpili bc UTARATIBU UNGEBADILIKA! Hivyo ndivyo nijuavyo mimi ! Kama kuna mjuzi mwingine ajuae TOFAUTI na hivyo basi naomba ATUELIMISHE ZAIDI!
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa Yesu hakuteswa enzi za pontio pirato aliteswa enzi za pontio pilatoWarumi wana nguvu kubwa duniani...hawa hawa ndiyo walimtesa Yesu zamani za pontio pirato na hawa hawa ndiyo wanarudi kutupangia ratiba. Mkumbuke wakati ule wa pontio pirato warumi ndiyo walikuwa watawala.
Safi sana. Sasa soma vizuri nilichoandika. Nilisema; Tulionywa mapema kabla kuwa Endapo kutatokea Kanisa Katoliki lingine nje ya Rome; Tusilikubali. Hata wawepo mapapa 10. Papa ni mmoja tu, aliyeko pale Roma baaaasiiiii
Umejuaje mkuu kama sio mtaliano ?Na hapo we sio mzungu wala mtaliano au mvatican ni mtu 1 mweusi mwenye hisia kali kuliko wenye dini yao
Acha kusikia mapokeo ya mababa, soma maandiko matakatifu Biblia. Wasome waliokuwa wanafunga toka Ibrahim mpaka mitume. Hakuna kuchagua cha kufunga.Nimekuelewa mkuu ndio maana zamani mzee alikuwa anatuambia tuchague cha kufunga kama ni wali au ugali au nyama.....ni mpka kwaresma iishe
Sent using Jamii Forums mobile app
Katika siku za Agano la Kale na pia katika Agano Jipya, kama tulivyosikia katika Maandiko Matakatifu ya kuwa ikiwa mtu alikuwa ametenda dhambi, alivaa nguo za magunia na kujipaka majivu katika mwili wake (Rej. Yer 6:26). Tendo hili tunalofanya leo la kupakwa majivu, linatokana na desturi hiyo ya kiroho ya kufanya toba. Katika ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au uduni (Rej. Ayubu 2:8, 30:19; Zab 102:10). Baadaye utamaduni huu wa kupakana majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama alama ya toba.
Huo ujinga wako huo sidhani ka kuna mtu aliye nao zaidi ya weye. U seem to be very very seditious and mbaguzi saanaA blackman ana pledge allegiance to Romans religious dominance...
Eti "kanisa la roma"......gross!
Huo ujinga wako huo sidhani ka kuna mtu aliye nao zaidi ya weye. U seem to be very very seditious and mbaguzi saana
Kwani Wasabato ni Wakristo!!?Sema wakristo wakatoliki. Sio wakristo wote maana kuna wasabato nadhani haya mambo wala hawayajui, kuna walokole, kuna mashahidi wa yehova, mormons nk. Usipende kauli jumlishi, ni dalili za ujinga.
Mm sibishan njoo hapa na maandiko unioneshe maagizo ya kujipaka majivuWe msabato nakuonaga sana ukibishana na watu Jf kwenye nyuzi mbali mbali... Ngojea kwanza niende kanisani nitarudi kukujibu.
Acheni bla blaa ,hiv unajua ibada ya majivu ilivyoaanza kanisa la Roma,? Au unaburuzwa tu,Katika siku za Agano la Kale na pia katika Agano Jipya, kama tulivyosikia katika Maandiko Matakatifu ya kuwa ikiwa mtu alikuwa ametenda dhambi, alivaa nguo za magunia na kujipaka majivu katika mwili wake (Rej. Yer 6:26). Tendo hili tunalofanya leo la kupakwa majivu, linatokana na desturi hiyo ya kiroho ya kufanya toba. Katika ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au uduni (Rej. Ayubu 2:8, 30:19; Zab 102:10). Baadaye utamaduni huu wa kupakana majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama alama ya toba.
Dini yenyewe kaletewa na wakoloni ila alivyoshupaa kuliko hata wenye dini yaoMleta uzi alihitaji kujua kwa nini J5 ya majivu na sio J4,J3 au Alhamisi? Wewe naona umetoka nje ya uzi kabisa, unaleta udini. Hapa ndipo lilipo tatizo kubwa la Watanzania.
Sent using Jamii Forums mobile app