Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Utaongea utatoka mishipa yote kanisa Ni moja Takatifu katoliki la mitume likisema Leo Ni Kwaresma, au pasaka wote itakuea hivyo. Na ndivyo ilivyo. Hakuna calendar tofauti wamejaribu hao kina sabbato wameshindwa wamebakia wenyewe the whole world wapo na kanisa moja ambalo Ni Takatifu katoliki la Mitume
Mleta uzi alihitaji kujua kwa nini J5 ya majivu na sio J4,J3 au Alhamisi? Wewe naona umetoka nje ya uzi kabisa, unaleta udini. Hapa ndipo lilipo tatizo kubwa la Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali: "Nini maana ya nguo ya magunia na majivu?"

Jibu: Nguo ya magunia na majivu yalitumiwa katika nyakati za Agano la Kale kama ishara ya kushusha hadhi, maombolezo, na / au toba. Mtu anayetaka kuonyesha moyo wake wa kutubu mara nyingi huvaa nguo ya magunia, kukaa katika majivu, na kuweka majivu juu ya kichwa chake. Nguo ya magunia ilikuwa nyenzo isiyo laini ambayo kawaida hutengenezwa kwa nywele nyeusi za mbuzi, na kuifanya isio na raha kabisa kuivaa. Majivu yalionyesha majonzi na maangamizi.

Mtu alipopokufa, tendo la kuvaa nguo ya magunia lilionyesha huzuni kubwa kwa kupoteza mtu huyo. Tunaona mfano wa hili wakati Daudi aliomboleza kifo cha Abneri, jemadari wa jeshi la Sauli (2 Samweli 3:31). Yakobo pia alionyesha huzuni yake kwa kuvaa nguo ya magunia wakati alidhani mwanawe, Yusufu, alikuwa ameuawa (Mwanzo 37:34). Matukio haya ya maombolezo kwa wafu hutaja nguo za magunia lakini si majivu.

Mjivu yaliambatana na nguo ya magunia katika nyakati wa msiba wa kitaifa au kutubu kutoka kwa dhambi. Esta 4:1, kwa mfano, inaelezea Mordekai akirarua nguo zake, akivaa nguo ya magunia na majivu, na kuingia mjini "akilia kwa sauti kubwa na kwa uchungu." Hili ndio lilikuwa jibu la Mordekai kwa tangazo la Mfalme Ahasuero kutoa mamlaka kwa Hamani dhaifu kuharibu Wayahudi (tazama Esta 3:8-15). Mordekai sio peke yake ambaye aliomboleza. "Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu "(Esta 4:3). Wayahudi wakajibu habari haribifu kuhusu mbio zao na nguo ya magunia na majivu, kuonyesha huzuni kali sana na dhiki.

Nguo ya magunia na majivu pia hutumika kama ishara ya umma ya toba na unyenyekevu mbele ya Mungu. Wakati Yona aliwaambia watu wa Ninawi kwamba Mungu angeenda kuwaangamiza kwa sababu ya uovu wao, kila mtu kutoka kwa mfalme hadi kwa raia wa chini kabisa alijibu kwa toba, kufunga, na nguo ya magunia na majivu (Yona 3:5-7). Waliweka nguo ya magunia hata kwenye wanyama wao (mstari wa 8). Mawazo yao yalikuwa, "Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?"(mstari wa 9). Hii ni ya kushangaza kwa sababu Biblia haisemi kamwe kwamba ujumbe wa Yona unahusisha kutaja kwokwote kwa huruma ya Mungu; lakini rehema ndio waliyopokea. Ni wazi kwamba uvaaji wa nguo ya magunia na majivu kwa watu wa Ninawi haikuwa maonyesho yasio na maana. Mungu aliona mabadiliko ya kweli-mabadiliko ya unyenyekevu ya moyo yaliyowakilishwa na nguo ya magunia na majivu-na ilisababisha Yeye "kuacha" na kutoleta mpango Wake wa kuwaangamiza (Yona 3:10).

Watu wengine Biblia inataja walivaa nguo ya magunia ni pamoja na Mfalme Hezekia (Isaya 37:1), Eliakimu (2 Wafalme 19:2), Mfalme Ahabu (1 Wafalme 21:27), wazee wa Yerusalemu (Maombolezo 2:10), Danieli (Danieli 9:3), na mashahidi wawili katika Ufunuo 11:3.

Kwa urahisi sana, nguo ya magunia na majivu yalitumiwa kama ishara ya nje ya hali ya ndani ya mtu. Ishara kama hiyo ilifanya mabadiliko ya moyo wa mtu kuonekana na kuonyesha uaminifu wa huzuni na/au toba. Haikuwa tendo la kuvaa nguo ya magunia na majivu yenyewe ambayo yalimshawishi Mungu kuingilia kati, lakini unyenyekevu kwamba hatua kama hiyo imeonyeshwa (angalia 1 Samweli 16:7). Msamaha wa Mungu kwa mjibu wa toba ya kweli husherehekewa na maneno ya Daudi: "Ulinivua nguo ya magunia, ukanivika furaha" (Zaburi 30:11).
shukrani sana .
 
Tatizo ni pale unapotaka kutuaminisha kama hao waleta hiyo dini walivyotaka. Imani yangu ya katoliki inaniambia kuwa niamini hivi; KANISA TAKATIFU KATOLIKI LA RUMI. Hii inamaana walitaka, hata kukitokea Katholiki nyingine, tusikubaliane nalo. Tuweke imani na mafundisho yetu mahali pamoja ili tusilishwe matango pori huko.
Kwa taarifa tu yaliwahi kuwa mawili La Rome na Ufaransa. Soma historian ya kanisa.

Kulikua na mapapa wawili...
 
Mimi Wala sikua najibu hoja ya mleta
Mada Soma vizuri, Bali mpuuzi mmoja ametoa kashfa ya kipuuzi nami nikamjibu kisabato
 
Kwa taarifa tu yaliwahi kuwa mawili La Rome na Ufaransa. Soma historian ya kanisa.

Kulikua na mapapa wawili...
Safi sana. Sasa soma vizuri nilichoandika. Nilisema; Tulionywa mapema kabla kuwa Endapo kutatokea Kanisa Katoliki lingine nje ya Rome; Tusilikubali. Hata wawepo mapapa 10. Papa ni mmoja tu, aliyeko pale Roma baaaasiiiii
 
Utaongea utatoka mishipa yote kanisa Ni moja Takatifu katoliki la mitume likisema Leo Ni Kwaresma, au pasaka wote itakuea hivyo. Na ndivyo ilivyo. Hakuna calendar tofauti wamejaribu hao kina sabbato wameshindwa wamebakia wenyewe the whole world wapo na kanisa moja ambalo Ni Takatifu katoliki la Mitume
NISAIDIE MAANA HALISI YA MANENO HAYA:
1, utakatifu
2, kisha nieleze utakatifu wa kabisa katoriki ni nini na ni upi.
3, Ni nani aliyelipasisha kabisa katoliki? Nipe maandiko toka Biblia. Hebu tuanzie hapo
2,U

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakristo tunafunga siku 40! Sasa basi cku ya jpili huwa Hakuna kufunga kwani ni cku ya bwana! Sasa kwa wiki tunafunga cku 6 (ukitoa kila jumapili ambayo hatufunahi) ukichukua majuma 6 tunayofunga unapata siku 36! Sasa ili zikamilike cku 40 ndio unaanza j5 ya majivu mpaka jmos kuna cku 4! Sasa unajumlisha cku 36 na siku 4 ndio unapata cku 40! Lkn kama ingekuwa tunafunga mpaka jpili bc UTARATIBU UNGEBADILIKA! Hivyo ndivyo nijuavyo mimi ! Kama kuna mjuzi mwingine ajuae TOFAUTI na hivyo basi naomba ATUELIMISHE ZAIDI!

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii ina tofauti gani na SUPERSTITION?

Because they do the same routine like movie actors with movie roles!

Dini ni political set up first and foremost to control motherfuckers!
 
Safi sana. Sasa soma vizuri nilichoandika. Nilisema; Tulionywa mapema kabla kuwa Endapo kutatokea Kanisa Katoliki lingine nje ya Rome; Tusilikubali. Hata wawepo mapapa 10. Papa ni mmoja tu, aliyeko pale Roma baaaasiiiii

A blackman ana pledge allegiance to Romans religious dominance...

Eti "kanisa la roma"......gross!
 
Nimekuelewa mkuu ndio maana zamani mzee alikuwa anatuambia tuchague cha kufunga kama ni wali au ugali au nyama.....ni mpka kwaresma iishe

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kusikia mapokeo ya mababa, soma maandiko matakatifu Biblia. Wasome waliokuwa wanafunga toka Ibrahim mpaka mitume. Hakuna kuchagua cha kufunga.

Tumeamliwa kufunga kula na kunywa. kadiri ya Uwezo wako wa kustahimili njaa na kiu. Hii hufanyika kwa mtu anayetafuta kuwa karibu na mungu kwa kutubu makosa yake,au kuomba jambo fulani lililo jema kwa mungu atendewe yeye au mwingine. Kufunga ni kuutesa mwili ili mungu aone kweli umejutia kosa ulilofanya,au kitu unachoomba kina umuhimu sana.

TENDO HILI MUNGU ULIFURAHIA SANA KWAKUWA ANAONA HAKUNA UNACHOKITEGEMEA ZAIDI YA YEYE. HUTEKELEZA HARAKA SANA.Msifuate mikumbo tu ati askofu kusema,padri kusema,eti mchungaji kasema.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
vipi kuhusu kuvaa nguo za magunia, mbona hatuvai leo?
Katika siku za Agano la Kale na pia katika Agano Jipya, kama tulivyosikia katika Maandiko Matakatifu ya kuwa ikiwa mtu alikuwa ametenda dhambi, alivaa nguo za magunia na kujipaka majivu katika mwili wake (Rej. Yer 6:26). Tendo hili tunalofanya leo la kupakwa majivu, linatokana na desturi hiyo ya kiroho ya kufanya toba. Katika ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au uduni (Rej. Ayubu 2:8, 30:19; Zab 102:10). Baadaye utamaduni huu wa kupakana majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama alama ya toba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ujinga wako huo sidhani ka kuna mtu aliye nao zaidi ya weye. U seem to be very very seditious and mbaguzi saana

Mbaguzi wa nini?

It is only right to be mbaguzi kwenye ujinga!

Umetoa general statement tu,nenda kwenye specifics,ufanye counter ya hoja zangu,sio unaishia kwenye "wewe mjinga sana" And then basi....

Ulisomaje shule hujui kujibu maswali wewe?

Na unajua maana ya seditious au una kunya kunya tu?
 
We msabato nakuonaga sana ukibishana na watu Jf kwenye nyuzi mbali mbali... Ngojea kwanza niende kanisani nitarudi kukujibu.
Mm sibishan njoo hapa na maandiko unioneshe maagizo ya kujipaka majivu

Nami nitakupa historia hadi papa aliyeanzisha huo upagani na aliutoa wapi

Maana ushadanganywa , kuabudu Masanamu, kusali rozali, kuasi amri za Mungu ,umeaminishwa ndio ukristo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika siku za Agano la Kale na pia katika Agano Jipya, kama tulivyosikia katika Maandiko Matakatifu ya kuwa ikiwa mtu alikuwa ametenda dhambi, alivaa nguo za magunia na kujipaka majivu katika mwili wake (Rej. Yer 6:26). Tendo hili tunalofanya leo la kupakwa majivu, linatokana na desturi hiyo ya kiroho ya kufanya toba. Katika ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au uduni (Rej. Ayubu 2:8, 30:19; Zab 102:10). Baadaye utamaduni huu wa kupakana majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama alama ya toba.
Acheni bla blaa ,hiv unajua ibada ya majivu ilivyoaanza kanisa la Roma,? Au unaburuzwa tu,

Nakuja kukufundisha ,ngoja ninywe uji kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom