Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes mmekatisha huduma no channel zote hazioneshi kitu..tatueni hili tatizo kama mnanisikia.
 
Star Times Tanzania mbona katika king'amuzi chenye smart card namba 02035024318 ambacho kilikuwa hakitumiki muda mrefu sasa kimeanza kutumika lakini channel zote za Tanzania hazionekani.
Msaada please
 
Last edited by a moderator:
MOD ni heri kuifuta hii thread kuliko kuacha huu uhuni wa Startimes wa kuja kuanzisha mada kisha kuacha kujibu mashwali kama walivyo katika huduma yao kwa cistomer.ukipiga simu.
Hivi vituo vya wazalendo kama Azam, ITV nk vingefanya tafiti jinsi ya kutoa huduma safi zaidi na kwa wengi zaidi ili watu waachane na hao wezi
 
mimi nipo morogoro mjini,channel zenu za music kama vile channel 5, MTV Base na One music mziki wake hauna sterio,upo mono sana,unasikia besi tu ,mchicha husikii kabisa,nimejaribu kwenda kwenye 'audio settings' na kuweka option ya sterio hakuna kitu,wakati channel za habari kama BBC zina sterio,mnanisaidiaje mimi mpenzi wa mziki manake sipati kabisa ladha kamili ya mziki

Kitu kingine,huu ni kama ushauri tu,kiukweli mpo kizamani sana yaani kama enzi za analogia vile,unakuta mtu ukiingia katika mtandao wenu unategemea utapata taarifa fulani kuhusu vifurushi vyenu,hizipati,mfano ukitaka kujua channel zenu zilizopo ktk kila kifurushi ili ulipie hupati popote pale,n.k,badilikeni wandugu,muwe mnaweka taarifa zenu zote ktk tovuti yenu na mtu amalizie shida zake huko huko sio hadi nije huku tuanze kuclick 'keyboards'

La mwisho kabisa,naomba unitajie channel zinazopatikana katika kifurushi cha 'NYOTA' manake kila nikiingia katika mtandao wenu hakuna taarifa zozote za channel za kwenye vifurushi vyenu
 
king'amuzi cha startimes kimezima taa ya signal indicator ambayo hua green pale front panel na kusababisha kukosa channel zote.
wandugu tatizo ni nini hapo? msaada tafadhari
 
Star Times mbona simu za startimes P40 na zinginezo hazipatikani kwa mawakala wenu hapa jijini Mwanza?nahitaji kununua
 
Last edited by a moderator:
Habari,
kuanzia juzi majira ya saa 6 mchana, channel ye EATV imeondolewa kutoka kwenye king'amuzi cha STARTIMES. Tunahitaji majibu toka kwenu na mamlaka Husika TCRA. its not fair! STATIMES mna matatizo gani na hizi stations! Tumekurupuka kuingia digitali!
 
ITV,Star pia zimeondolewa,wakati huu wa uchaguzi mtaangalia TBCCM mpende msipende after all star times ina wateja wengi
 
Habari,
kuanzia juzi majira ya saa 6 mchana, channel ye EATV imeondolewa kutoka kwenye king'amuzi cha STARTIMES. tunahitaji majibu toka kwenu na mamlaka Husika TCRA. its not fair! STATIMES mna matatizo gani na hizi stations! tumekurupuka kuingia digitali!

mbona mimi naona zote ndugu ila hiyo EATV huwa sometimes inabadirika jina wewe bonyeza ile ile namba yake utaiona.
tumia ile atenna yao ya nje
 
Nimesikia Mengi ndio kaamua zitolewe. Kiukweli ni pigo kwa walalahoi ambao wengi wapo startimes.
 
mbona mimi naona zote ndugu ila hiyo EATV huwa sometimes inabadirika jina wewe bonyeza ile ile namba yake utaiona.
tumia ile atenna yao ya nje

Sijaelewa zinabadilika vipi majina.
 
labda wamegombanaaa, au hawajalipana....aucz star tv inaonesha bongo star search LOL
 
Habari,
kuanzia juzi majira ya saa 6 mchana, channel ye EATV imeondolewa kutoka kwenye king'amuzi cha STARTIMES. tunahitaji majibu toka kwenu na mamlaka Husika TCRA. its not fair! STATIMES mna matatizo gani na hizi stations! tumekurupuka kuingia digitali!
Hili tatizo ni kwa wengi ,cha kufanya jaribu kuhamisha antenna yako toka upande mmoja kwenda upande mwingine utapata hiyo eatv ila usishangae kupoteza tbc na Chanel ten.
 
Mbona zipo!? acheni mambo ya uongo, yanawasaidia nini? huenda walifanya update na antena yako haikuwa vzr, hivyo haikuandika majina ya channels. Cha kufanya ni ku scan upya channels.
 
ITV,Star pia zimeondolewa,wakati huu wa uchaguzi mtaangalia TBCCM mpende msipende after all star times ina wateja wengi

Wateja wake wengi ni wale ambao hawalipii kila mwezi,ni wanaoangalia local channels za bure
 
Nachoshangaa,hivi ving'amuzi vipya local channel hazibaki,ni lazima ulipie zote ndo uone!
Kwann?

Na kuna baadhi ya channel zipo kwenye hiki king'amuzi kipya cha zamani hakuna!mfano Emmanuel TV

Pia channel hiyo ukiwa mkoa unapata,dar hupati !
Kwann?
 
Back
Top Bottom