Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Naishi Posta.Dar
King'amuzi changu kinashika local channels vizuri ila NBA Tv ina scratch sana.Siwez ata kuangalia.Tatizo ni nini?
 
Hii hata mimi imeshanikuta sana,nalipa kifurushi cha mwezi baada ya wiki mbili wanakata hata mwezi hautimii,ebu tuambieni ni nini hiki?

Itakuwa wakati unanunua king'amuzi kilikuwa kwenye malipo ya kifurushi cha bei kubwa,wapigie uwambie wakuhamishie kwenye kifurushi cha bei unayotaka
 
Naishi Posta.Dar
King'amuzi changu kinashika local channels vizuri ila NBA Tv ina scratch sana.Siwez ata kuangalia.Tatizo ni nini?


habari naomba utupm namba yako ya Simu tutamtuma wataalamu wetu kwa msaada zaidi
 
habari yako je unaishi wapi, tafadhari tembelea maduka ya startimes utapata remote zetu kwa gharama ya Tshs 5000 tu

Naomba Magufuli apitie hapa haraka, kampuni ya ajabu kabisa, mmeleta madishi hamna lolote mara no signals, mara local channels unaambiwa not subscription!, channel haiwezi kutulia ndani yq dakika 2 lazima i kwame..Channels hazina mpangalio yaaani nyieee ipo siku yenu..
 
uzuri wa startimes mkipigiwa simu mnapokea hapohapo si kama azam ambao huwa haipokelewi kabisa simu.
 
Uzuri wa startimes mkipigiwa simu mnapokea hapohapo si kama azma simu huwa haipokelewi kabisa.
 
Nimenunua decoder ya startimes nimepewa oga ya miezi saba. Je naweza badili kifurushi nikapata kile kinacho onesha channel nyingj za mpira?
 
Channel kama TV1 na Star Tv zina scratch sana, TBC 2 stereo yake mbaya sana. Pia customer care wenu hawana lugha nzuri. Jaribuni kurekodi simu zote za wateja mtabaini tatizo kubwa.
 
Channel kama TV1 na Star Tv zina scratch sana, TBC 2 stereo yake mbaya sana. Pia customer care wenu hawana lugha nzuri. Jaribuni kurekodi simu zote za wateja mtabaini tatizo kubwa.

Mi nilipo hizo zimekata kabisa nataka niachane nao nirudi cable japo ni gharama.
 
Ni wiki 2 sasa simu yangu ya star times P 40 imezima , nimetumia kwa miezi 3, nimeenda duka la star times wananizusha tu.
 
Habari zenu wanaJamiiForums

Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie? Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi?
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

Ahsanteni sana na karibuni nyote
Mkuu nina swali. Nimeibiwa king'amuzi changu cha star times. Je, kuna uwezekano wa kukipata?
 
Back
Top Bottom