Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Mimi wanakata channel zote nikilipa baada ya wiki mbili wanakat tena..jana nimelipa wamenifungulia channel 3 tu.. hawa ni wezi wakubwa
 
Habari, naomba msaada wenu, nikiweka smart card kwene decoder, ujumbe unatokea wa No acces and Not subscribed, je nifanyaje?
 
Naweza kubadilisha king'amuzi cha zamani ili nipate kipya??nina kile cha zamani boksi la pembe nne..sasa nahitaji kipya hivi vidogo...utaratibu ukoje??pia channel zinasumbua sana..nipo mgeninani kata ya kijichi..
 
Hivi hawa muda nyota wamo humu?wakiacha utoto naomba wanijibu kwa nini sisi wa nchi jirani ya Zanzibar tuna vifurushi viwili tu vya mambo na uhuru hatuna cha Kili?
 
Habari zenu wanaJamiiForums

Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie? Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi?
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

Ahsanteni sana na karibuni nyote

Mimi nina tatizo ambalo na shindwa kuelewa kwa nini local channels haipatikani zaidi ya TBC... Ilhali king'amuzi nilichokuwa nacho Dom kulikuwa kinaonesha. Maana wengine TBC ni kama mam mkwe
 
Nauliza wakulima kuwa na leseni ni sawa kwani leo sehemu ya babati Mkoa wa Manyara gari zangu zimezuiliwa na afisa TRA Mohamed Karume kwa madai ya leseni ya mazao ya mtama mimi nilikuwa napeleka Arusha kuuza nikitokea Shinyanga hivi ni wakulima wote au mimi pekee yangu naomba kufahamishwa
 
habari yako

tunaving'amuzi vya aina mbili, vinavyotumia antenna na vinavyotumia Dish

vinavyotumia Antena viko vya aina mbili

kuna vile ukinunua unafurahia chanel zaidi ya 75 mwezi mmoja kinauzwa tshs 59000
na kuna vile ukinunua unapata chanel 17 kwa muda wa miezi 7.5 vinauzwa tsh 34000 (kingamuzi na malipo humo humo)

vingamuzi vinavyotumia Dish

hivi vinauzwa TSHS 139000 pamoja na ufundi unapata na dishi lake
kama unadishi kinauzwa Tshs 96000

Ahsante
Mlisema localchanel bure sasa mi napata Tbc peke yake tu jamani au ndo mpo kitapeli zaidi msitufanyie ivyo jamani.
 
Mie nililipia hio 4000 ilikaa siku 6 tuuu hebu nijibuni na mimi inakuaje
 
Ijumaa iliyopita nimelipia kifurushi cha Mambo. Mmeweka channel nyingi amabzo hazipatikani Arusha ila DSM tuu, mfano cctv news,CTN,Tumain tv, Mlimani tv, Clouds tv. Kwanini msizitoe hizo Channel maana inakuwa ni utapeli una market kitu usichokuwa nacho kwa eneo husika, na wala ukitaka kulipia hauambiwi kama hazipo
 
Nilifuta chanel zote za kibongo nisaidieni jinsi ya kuzirudisha maana niliambiwa kuna namba unaziweka je ni kwl na n nambaga gan #startimes
 
kwenye vipeperushi vyenu. Mmeonyesha kuna vifirushi 2 vya michezo. Kimoja ni 5,000 na kingine ni 14,000

Swali:
je! Katika hivyo vifurushi 2 ukilipia 5,000/= Au 14,000/= utapatatu hivyovifurushi vya mpira bila kupata station nyingine?

Maana wengi wetu tunaweza kupenda kulipia hizo station za michezotu tusitake station nyingine.

Swali jingine:
je! Sisi wenye vingamuzi vya zamani, tunawezaje kujiunga kupata hizo station za vifurushi vya michezo peke yake?
 
Mlisema localchanel bure sasa mi napata Tbc peke yake tu jamani au ndo mpo kitapeli zaidi msitufanyie ivyo jamani.
hili labda niwasaidie startimes kuwajibia. Ni hivi hivi vingamuzi vya promotion. Ukinunua ni vyakulipia kila mwezi.

Kama unataka hambacho hakilipiwi mwisho wa mwezi nadhani wanaviuza kuanzia elf 60 kama sikosei.

Sasa watu wengi wanapenda vya elf 22 bila kujua kila mwisho wa mwezi itawagharimu kulipia.
 
Startimes mbona nimelipia kifurushi cha uhuru malipo ya mwezi kimekaa wiki mbili kifurushi kimeisha?
 
Habari zenu wanaJamiiForums

Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie? Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi?
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

Ahsanteni sana na karibuni nyote
Napenda kuuliza kuhusu simu zenu za startimes kutokua na memory card. mi NAP G GHAYO .NAMBA YANGU NI 0676754632
 
Startimes nyinyi kuna mda mnanikera hadi natamani kuuza king'amuzi ila basi. Boresheni basi channeli mnazoonyesha kwa vifurushi hvi vya cheap. Sio kwakua ni elfu4 ndo mtupatie machanel ya ajabu. Akhsante
 
Channel za bongo mbona hazionekani zaidi ya tbc 1?? Au nazo zinalipiwa??
 
nilitaka kuhamia huku kumbe kote shida
 
Back
Top Bottom