Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Mimi nawapa ushauri tu kwa nini msibuni ving'amuzi vya kwenye magari?
 
habari yako, pole kwa usumbufu, ukishafanya malipo katika king'amuzi chetu, inakupasa usubiri si zaidi ya dk 15 kabla chaneli hazijaanza kuonyesha, endapo itachelewa basi kunakuwa na matatizo katika mifumo yetu, na tunakushauri ikitokea hivyo wasiliana na watoa huduma wetu moja kwa moja wafanye 'manual authorizations'
No zenu za dharura ni zipi? Hii nayo ni changamoto
 
habari yako, chanel hii ni local na huwa zinapatikana bure, isipokuwa pale tu kama ulinunua kile chenye bei maalum ambacho pia unaweza kubadilisha kadi na ukapata chanel zote za nyumbani bure
Hapo kweny kubadli kad utaratbu na gharama zipoje?
 
Mnacho bore ni hiki, Bollywood wanatoa movie nzuri sana kila siiku. Lakini nyie mnakomaa na movie zile zile,mara chamku,mara sikupendi mara hii unasema hii ya mwezi uliopita,nyingine ukiiona tu unasonya na kubadili chanel. Mnakera sana tena sana,tunalipia lakini matufanya sisi mazuzu

habari yako, tunashukuru kwa maoni tutajitahidi kuboresha zaidi
 
Naomba kujua kuna kifurushi cha Week cha elfu moja?? [HASHTAG]#startimes[/HASHTAG]


habari yako, gharama inategemea na aina ya kingamuzi ulicho nacho kama ni cha dish au cha antena! lakini gharama zetu ni

upload_2017-9-28_9-59-41.png
 
Mimi nawapa ushauri tu kwa nini msibuni ving'amuzi vya kwenye magari?


habari yako, hapo awali 2014 na 2015 tulikuwa na aina hii ya huduma Dar es Salaam na arusha, tulikuwa na car tv, GPS 7, G 501, Lakini mwitikio haukuwa mzuri kabla hatujasitisha huduma hii, tunashukuru kwa maoni tutafikisha kwa idara husika
 
Huku kwetu Tandale ving'amuzi vya anttena havitoi sauti TBC1 wala TBC2

Bahatu siyo ITV maana mngeua soko lenu
 
Huku kwetu Tandale ving'amuzi vya anttena havitoi sauti TBC1 wala TBC2

Bahatu siyo ITV maana mngeua soko lenu

Habari yako, tafadhari nyaya za sauti nyuma ya king'amuzi chako zi 'exchange' kama nyeupe umechomeka kwa nyeupe na nyekundu kwa nyekundu badilisha nyeupe chomeka kwa nyekundu na nyekundu kwa nyeupe!
 
ni miongoni mwa ving'amuzi vya kipuuzi sana mfano mimi ninatumia dish kifurushi cha chini cha mwezi nalipa sh 9000 ninachomzidi mwenye antena ni clouds tv tu.

ila mwenye antena kifurushi cha bei ya chini cha mwezi analipia sh 6000 ila tofauti ni yeye kifurushi chake kikiisha anapata free tv1 na tbc 1 pia faida nyingine ya king'amuzi cha antena kwa hiyo gharama ndogo ya 6000 anaongezewa tv sibuka na tv iman tofauti na mimi mwenye dish hata nilipe 100000 siwezi pata hizo channels huo ni upuuzi wa king'amuzi cha star times Tanzania ukipiga simu wanakujibu kunya kwanza vifurushi vinakata kabla ya kumaliza mwezi ukienda kwenye ofisi yao ya mkoa wafanyakazi wao wapo bussy na kuchezea komputer na simu [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] natafuta mpunga tu hapa nihame king'amuzi kingine huu ni uhuni wa kiwango cha rami.
 
Habari zenu wanaJamiiForums

Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie. Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi.

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

kumbuka namba zetu za huduma kwa wateja ni 0764700800 au 0677700800

Ahsanteni sana na karibuni nyote.

Habari! Naombeni msaada juu ya hili king'amuzi changu cha startimes kuanzia juma tatu ya tarehe 2 mwezi huu jioni kinasoma channel tatu tu Stv guide, Tbc1 na Tv1 na wakati hapo awali kilikuwa kinaonyesha hizi channel TBC1, TV1, TVE, CLOUDS TV, ITV,EATV,TV IMANI, TABIBU TV tangu nimenunua mwaka 2011 naombeni msaada tafadhari maana litakuwa tena ni kopo tu na wakati nilikuwa napata hizi channel bure

Nipo Dar.ahsanteh
 
Habari yako, tafadhari nyaya za sauti nyuma ya king'amuzi chako zi 'exchange' kama nyeupe umechomeka kwa nyeupe na nyekundu kwa nyekundu badilisha nyeupe chomeka kwa nyekundu na nyekundu kwa nyeupe!
Habari! Naombeni msaada juu ya hili king'amuzi changu cha startimes kuanzia juma tatu ya tarehe 2 mwezi huu jioni kinasoma channel tatu tu Stv guide,Tbc1 na Tv1 na wakati hapo awali kilikuwa kinaonyesha hizi channel TBC1,TV1,TVE,CLOUDS TV,ITV,EATV,TV IMANI,TABIBU TV tangu nimenunua mwaka 2011 naombeni msaada tafadhari maana litakuwa tena ni kopo tu na wakati nilikuwa napata hizi channel bure,
Nipo Dar.ahsanteh
 
Back
Top Bottom