Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

lakini mkuu unaonaje tuishi kwa mila na desturi za Kiafrika itaondoa hii kupigania imani au dini za watu nchi zingine
Kwangu Ukristu unayo nafasi yake na Mila na desturi zetu za kiafrika zinanafasi yake pia.

Ni kanisa katoliki pekee lenye kutambua baadhi ya Mila na desturi hai wengine wote naogopa hata kusema
 
Swali: "Nini maana ya nguo ya magunia na majivu?"

Jibu:
Nguo ya magunia na majivu yalitumiwa katika nyakati za Agano la Kale kama ishara ya kushusha hadhi, maombolezo, na / au toba. Mtu anayetaka kuonyesha moyo wake wa kutubu mara nyingi huvaa nguo ya magunia, kukaa katika majivu, na kuweka majivu juu ya kichwa chake. Nguo ya magunia ilikuwa nyenzo isiyo laini ambayo kawaida hutengenezwa kwa nywele nyeusi za mbuzi, na kuifanya isio na raha kabisa kuivaa. Majivu yalionyesha majonzi na maangamizi.

Mtu alipopokufa, tendo la kuvaa nguo ya magunia lilionyesha huzuni kubwa kwa kupoteza mtu huyo. Tunaona mfano wa hili wakati Daudi aliomboleza kifo cha Abneri, jemadari wa jeshi la Sauli (2 Samweli 3:31). Yakobo pia alionyesha huzuni yake kwa kuvaa nguo ya magunia wakati alidhani mwanawe, Yusufu, alikuwa ameuawa (Mwanzo 37:34). Matukio haya ya maombolezo kwa wafu hutaja nguo za magunia lakini si majivu.

Mjivu yaliambatana na nguo ya magunia katika nyakati wa msiba wa kitaifa au kutubu kutoka kwa dhambi. Esta 4:1, kwa mfano, inaelezea Mordekai akirarua nguo zake, akivaa nguo ya magunia na majivu, na kuingia mjini "akilia kwa sauti kubwa na kwa uchungu." Hili ndio lilikuwa jibu la Mordekai kwa tangazo la Mfalme Ahasuero kutoa mamlaka kwa Hamani dhaifu kuharibu Wayahudi (tazama Esta 3:8-15). Mordekai sio peke yake ambaye aliomboleza. "Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu "(Esta 4:3). Wayahudi wakajibu habari haribifu kuhusu mbio zao na nguo ya magunia na majivu, kuonyesha huzuni kali sana na dhiki.

Nguo ya magunia na majivu pia hutumika kama ishara ya umma ya toba na unyenyekevu mbele ya Mungu. Wakati Yona aliwaambia watu wa Ninawi kwamba Mungu angeenda kuwaangamiza kwa sababu ya uovu wao, kila mtu kutoka kwa mfalme hadi kwa raia wa chini kabisa alijibu kwa toba, kufunga, na nguo ya magunia na majivu (Yona 3:5-7). Waliweka nguo ya magunia hata kwenye wanyama wao (mstari wa 8). Mawazo yao yalikuwa, "Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?"(mstari wa 9). Hii ni ya kushangaza kwa sababu Biblia haisemi kamwe kwamba ujumbe wa Yona unahusisha kutaja kwokwote kwa huruma ya Mungu; lakini rehema ndio waliyopokea. Ni wazi kwamba uvaaji wa nguo ya magunia na majivu kwa watu wa Ninawi haikuwa maonyesho yasio na maana. Mungu aliona mabadiliko ya kweli-mabadiliko ya unyenyekevu ya moyo yaliyowakilishwa na nguo ya magunia na majivu-na ilisababisha Yeye "kuacha" na kutoleta mpango Wake wa kuwaangamiza (Yona 3:10).

Watu wengine Biblia inataja walivaa nguo ya magunia ni pamoja na Mfalme Hezekia (Isaya 37:1), Eliakimu (2 Wafalme 19:2), Mfalme Ahabu (1 Wafalme 21:27), wazee wa Yerusalemu (Maombolezo 2:10), Danieli (Danieli 9:3), na mashahidi wawili katika Ufunuo 11:3.

Kwa urahisi sana, nguo ya magunia na majivu yalitumiwa kama ishara ya nje ya hali ya ndani ya mtu. Ishara kama hiyo ilifanya mabadiliko ya moyo wa mtu kuonekana na kuonyesha uaminifu wa huzuni na/au toba. Haikuwa tendo la kuvaa nguo ya magunia na majivu yenyewe ambayo yalimshawishi Mungu kuingilia kati, lakini unyenyekevu kwamba hatua kama hiyo imeonyeshwa (angalia 1 Samweli 16:7). Msamaha wa Mungu kwa mjibu wa toba ya kweli husherehekewa na maneno ya Daudi: "Ulinivua nguo ya magunia, ukanivika furaha" (Zaburi 30:11).
 
Ungekuwa mstaarabu ungeishia kwenye sentensi ya kwanza. Hukuwa na ulazima wa kuandika kwa shari kama ulikuwa na lengo la kumrekebisha mwenzako. Kama wewe ni mkristu basi wapaswa kujua mstari wa Bibilia unaosema Tendaneni kwa upendo.
Sema wakristo wakatoliki. Sio wakristo wote maana kuna wasabato nadhani haya mambo wala hawayajui, kuna walokole, kuna mashahidi wa yehova, mormons nk. Usipende kauli jumlishi, ni dalili za ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi warumi ndio walimtesa Yesu au Wayahudi? Maana navyojua mambo ya Dini yalikuwa chini ya Wayahudi wenyewe na hawakuingiliwa na wafalme wa Warumi
Warumi wana nguvu kubwa duniani...hawa hawa ndiyo walimtesa Yesu zamani za pontio pirato na hawa hawa ndiyo wanarudi kutupangia ratiba. Mkumbuke wakati ule wa pontio pirato warumi ndiyo walikuwa watawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika siku za Agano la Kale na pia katika Agano Jipya, kama tulivyosikia katika Maandiko Matakatifu ya kuwa ikiwa mtu alikuwa ametenda dhambi, alivaa nguo za magunia na kujipaka majivu katika mwili wake (Rej. Yer 6:26). Tendo hili tunalofanya leo la kupakwa majivu, linatokana na desturi hiyo ya kiroho ya kufanya toba. Katika ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au uduni (Rej. Ayubu 2:8, 30:19; Zab 102:10). Baadaye utamaduni huu wa kupakana majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama alama ya toba.
Si nyie huwa mnalipinga agano la kale lakini mnadai lilikuwa kwa ajili ya waisraeli leo kwenye majivu mnalikubali ha ha hebu leta aya kwenye agano jipya watu wanajipaka majivu, na kwanini hamvai magunia leo na kujipaka majivu mwili mzima mnapaka usoni tu? Pakeni mwili mzima acheni usharo nyie
 
wangekufafanulia pia nini maana halisi ya kufunga? kwamba unafunga masaa mangapi kwa siku? unaruhusiwa kunywa maji maziwa ama juice ikifika mchana? Je ni kweli kwamba unafunga vitu ambavyo mwili unavipenda zaidi ?
Kufunga kamili

Kitabu cha mtaguso kinaelezea kuwa kufunga ni masaa 18 kati ya masaa 24 ya siku. Unamaliza kula saa sita usiku na kufungua saa 12:00 jioni. Na
Ukiwa umefunga unatakiwa kusali ikiwemo njia ya msalaba kujiunganisha na mateso ya Yesu.
 
Mkuu mistari yote Hio hujasoma? Yeremia 6.26,
nimesoma mbona hamkuvaa magunia? nimekutana nao leo wamechorewa tu misalaba ya majivu kwenye vipaji vya nyuso zao karibu niseme alama ya mnyama nini. ila hakuna aliyevaa magunia hata moja hii imekaaje ukurejea mafungu uliyoyaandika
 
Si nyie huwa mnalipinga agano la kale lakini mnadai lilikuwa kwa ajili ya waisraeli leo kwenye majivu mnalikubali ha ha hebu leta aya kwenye agano jipya watu wanajipaka majivu, na kwanini hamvai magunia leo na kujipaka majivu mwili mzima mnapaka usoni tu? Pakeni mwili mzima acheni usharo nyie
Ha ha ha Biblia yote ni Neno la Mungu Mkuu;TOBA ina namna nyingi za kufanya, ni bora kufanya kuliko kutofanya kabisa
 
nimesoma mbona hamkuvaa magunia? nimekutana nao leo wamechorewa tu misalaba ya majivu kwenye vipaji vyao karibu niseme alama ya mnyama nini. ila hakuna aliyevaa magunia hata moja hii imekaaje
Mkuu unakaribishwa pia kuvaa hayo magunia ya TOBA na Kupaka Majivu mwili Mzima
 
Ungekuwa mstaarabu ungeishia kwenye sentensi ya kwanza. Hukuwa na ulazima wa kuandika kwa shari kama ulikuwa na lengo la kumrekebisha mwenzako. Kama wewe ni mkristu basi wapaswa kujua mstari wa Bibilia unaosema Tendaneni kwa upendo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati mwingine kenge hua haelewi ila hadi aone damu. Kuna wakati unatamiwa kumfundisha mtu kwa njia ngumu
 
Ha ha ha Biblia yote ni Neno la Mungu Mkuu;TOBA ina namna nyingi za kufanya, ni bora kufanya kidogo kuliko kutofanya kabisa
kwanini usifanye kabisa kwani kwenye kupaka majivu mwili mzima na kuvaa magunia huelewi kitu gani hasa,au ndo uofisa na uheshimiwa wakubatizwa maji kidogo kichwani badala ya ubatizo alioufundisha Yesu kuzamishwa kwenye maji mengi,acheni kuigiza mambo ya Mungu
 
Utaongea utatoka mishipa yote kanisa Ni moja Takatifu katoliki la mitume likisema Leo Ni Kwaresma, au pasaka wote itakuea hivyo. Na ndivyo ilivyo. Hakuna calendar tofauti wamejaribu hao kina sabbato wameshindwa wamebakia wenyewe the whole world wapo na kanisa moja ambalo Ni Takatifu katoliki la Mitume
Hapa tuna kanisa la mitume lisilofuata maagizo ya Bwana Yesu na mitume wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha Biblia yote ni Neno la Mungu Mkuu;TOBA ina namna nyingi za kufanya, ni bora kufanya kuliko kutofanya kabisa
Mbona maelekezo ya hiyo toba hamyatekelezi kama ipasavyo kwa mujibu wa maandiko yasemavyo mvae magunia na kujipaka mwili mzima majivu?
 
Katika siku za Agano la Kale na pia katika Agano Jipya, kama tulivyosikia katika Maandiko Matakatifu ya kuwa ikiwa mtu alikuwa ametenda dhambi, alivaa nguo za magunia na kujipaka majivu katika mwili wake (Rej. Yer 6:26). Tendo hili tunalofanya leo la kupakwa majivu, linatokana na desturi hiyo ya kiroho ya kufanya toba. Katika ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au uduni (Rej. Ayubu 2:8, 30:19; Zab 102:10). Baadaye utamaduni huu wa kupakana majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama alama ya toba.
asante mkuu
 
Utaongea utatoka mishipa yote kanisa Ni moja Takatifu katoliki la mitume likisema Leo Ni Kwaresma, au pasaka wote itakuea hivyo. Na ndivyo ilivyo. Hakuna calendar tofauti wamejaribu hao kina sabbato wameshindwa wamebakia wenyewe the whole world wapo na kanisa moja ambalo Ni Takatifu katoliki la Mitume
Tatizo ni pale unapotaka kutuaminisha kama hao waleta hiyo dini walivyotaka. Imani yangu ya katoliki inaniambia kuwa niamini hivi; KANISA TAKATIFU KATOLIKI LA RUMI. Hii inamaana walitaka, hata kukitokea Katholiki nyingine, tusikubaliane nalo.

Tuweke imani na mafundisho yetu mahali pamoja ili tusilishwe matango pori huko.
 
Back
Top Bottom