Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Mimi natumia antenna lakini huku nilikohamia ni bondeni fulani hivi , kwa hiyo napata shida sana kupata channels. Naambiwa dish halisumbui. Mnanisaidiaje hapo!?
 
Je Star times mmeondoa huduma ya Local channels kuwa free kifurushi kikiisha?Maana siku hizi kifurushi kikikata inabaki safari chanel pekee???
 
Je Star times mmeondoa huduma ya Local channels kuwa free kifurushi kikiisha?Maana siku hizi kifurushi kikikata inabaki safari chanel pekee???
Kweli kabisa. Wameanza kujiweka juu ya sheria, eeh? Serikali inatoa maagizo wao wanafanya watakavyo? Jeuri hii wanaipata wapi?
 
Kweli kabisa. Wameanza kujiweka juu ya sheria, eeh? Serikali inatoa maagizo wao wanafanya watakavyo? Jeuri hii wanaipata wapi?
Mimi nahisi hii mikataba haina cha free local channels, ila tunafanyiwa hisani sababu ingekua hicho kitu kipo inamaanisha wamebreach contract na si mara ya kwanza kufanya hivi mpaka utasikia waziri kawafata. Sasa serikali zetu zituambie ukweli. Kesho, kesho kutwa waziri atawafata zitarudishwa baadae watatoa. Sasa kama kitu cha mkataba why hakuna penalty yeyote.
 
Hv kwanini nyie STARTIMES hasa katika upande wa kifurushi cha "MAMBO" mmeamua kutuzingua katika ile tamthiria ya "KUMKUM BHAGYA? Maana ilikuwa inaenda fresh kabisa tatizo limeanzia katika kubadili muda. Hadi sasa Kumkum BHAGYA imeanza upya...nini SHIDA?
 
Hivi nyinyi wahuni itv na eatv mmezipeleka wapi mbona hazipo hata nikizitafuta sizipati
 
Je naweza kupata king'amuzi ambacho sio lazima nitoe antenna nje au kuweka dish?
 
Back
Top Bottom