Stella Fiyao: Sheria ya Ulinzi wa Data Binafsi ni muarobaini wa wananchi kuingiliwa akaunti zao

Stella Fiyao: Sheria ya Ulinzi wa Data Binafsi ni muarobaini wa wananchi kuingiliwa akaunti zao

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1667315288010.png

Mbunge CHADEMA Songwe Viti Maalum, Stella Fiyao akichangia hoja yake katika mjadala wa Muswada wa ulinzi wa taarifa binafsi anabainisha kuwa mswaada huu ni muhimu na utakwenda kutatua changamoto ya mamlaka kuingilia kwenye akaunti za watu mbalimbali.

Akifafanua hoja yake anasema kuwa Muswada huu utakwenda kuwa muarubaini wa wananchi kuingiliwa katika akaunti zao. Miaka milili mitatu iliyopita kuna watu waliingiliwa kwenye akaunti zao, wakasachiwa wakakutwa na kiasi cha pesa kisha wakafilisiwa.

zaidi ya hayo, Stella Fiyao anaweka bayana kwamba Muswada wa Ulinzi wa taarifa binafsi utaenda kuongeza uwekezaji ndani ya taifa letu kwa sababu kuna maeneo tumekosa uwekezaji kwa sababu ya kukosa sheri ya ulinzi wa taarifa binafsi. Bunge hili likipitisha sheria hii tutaenda kupata wawekezaji wa nje na ndani ya nchi.

Aidha, Stella Fiyao ameshauri kuwa kwenye muswada huu ni muhimu likaongezwa neno falagha ili kuipa uzito sheria husika.
 
How much do people want to bet it will do the opposite!
 
Back
Top Bottom