KERO Stendi kuu ya mabasi ya Moshi (Kilimanjaro) imejaa ujinga, upuuzi, uchafu na ushamba uliopitiliza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwa wiki nzima nikiwa na miche miche Moshi mjini, nikisafiri, kusafirisha watu na kupokea watu fulani fulani ikiwemo watalii kadhaa.
wewe fly kecha unatakiwa ujue hii nchi ni masikini africa ni masikini pia kwaiyoo hiyoo stand ungefunge macho upite hivi. ila tupa uchafu ndo utajua hujui. happy new year
 
Hakuna stendi hapo, ni pango la walanguzi, madalali, matapeli na wazururaji tu.
 
Uliyosema 90% ni kweli! Yaan pale stand sjawahi kupelewa!

Sijuwagi tofauti ya ile stand kubwa na ile stand ndogo! Maana kwenye stand kubwa had vi hiace vya kwenda uru vimejazana huko
 
Ukishangaa ya Moshi utayaona ya Arusha, sipendi kushukia wala kupandia kwenye hizo stendi, zimejaa wahuni sjapata kuona,
 
Moshi unaionea TU kaka, njoo Huku dar Kwa Chalamila, njia zote, namaanisha zote zimewekwa kuwa masoko
 
Kwamba stendi imejengwa zamani, huo siyo utetezi.
Mimi nitetee kwani nahusika na hiyo stendi? Mi naunga mkono yote uliyosema ila nilikua najaribu kuonyesha changamoto
 
ULICHOSEMA KWA MOSHI NI KWELI

Mimi nimetokea maeneo hayo, Moshi kuna Ujinga na Ushamba katika Manispaa ya Mji, hawajali chochote cha maana zaidi ya Rushwa/ Pesa

Kingine kwa pale Moshi, kuna yale majengo ya frame pale stendi yalijengwa na baadhi ya Wananchi wenye uwezo kwa mkataba wa kupewa fremu

Sasa hao wanachojali ni kupata pesa tu na kujenga huko vijijini na maeneo mengine

Kwa Mfano kuna Mtu anaitwa NOVATUS KIMARIO, huyu pale ana maduka nane (8) ya Cosmetics matatu, ya vyakula vya kawaida kama Mini supermarket n.k. Sasa huyu Jamaa ama maduka yanayoangalia stendi kbs na pale nyuma katikati ya jengo...huyu hata Halmashauri ya Mji haimwambii chochote japo Wananchi wa chini wanamlalamikia kwa mengi

Pia wapo wengine kadhaa...yaani mji unamilikiwa na watu wachache wanaoonga viongozi wa Halmashauri

Ndio maana mpango wa stendi mpya imekwama na sio kwamba Halmashauri haiingizi pesa

UJINGA MTUPU
 
Hayo mambo uliyoyataja yanapatikana kila sehemu sio moshi tu anyway mm kinachonikwaza pale stand ni mtu unajua unapoenda lakini madalali wanavyokuganda kukufuata kama vile umepotea
Hao madalali kwani kuna sehemu nchi wanapokesekana?
 
Kwa wiki nzima nikiwa na miche miche Moshi mjini, nikisafiri, kusafirisha watu na kupokea watu fulani fulani ikiwemo watalii kadhaa.
Wee wa miche miche utakuwa mmakonde, karibu njomba ila usije na nchale huku.
 
Asante sana tutayafanyia kazi mambo haya yote.
 
Stendi ni ya kishenzi sana ile, nilishawahi kuona katoto ka kichagga kamechuchumaa kanakunya huku raia wakimwangalia tu, naulizia watu mama wa yule mtoto yuko wapi wakasema mama yake anafanya kazi kwenye banda lile lile alilokuwa anakunya mwanawe na hashituki ukimwambia analeta ugomvi na kuuliza unataka mwanangu akanye wapi sasa.
 
True, hii stendi ni chafu mno haswa wakati wa mvua utakuta vinyesi kila uchochoro tena vikiwa fresh kabisa.
 
Mateja wa Moshi wana vile vikofia vyao vimejikunja kwa mbele hivi.
[emoji16]
Sema stand ya Moshi imetulea sana. 2000s tukitoroka shule tunaenda hapo stand kula, kunyoa, na kuburn CDs pale ghorofani huku tukitafuta videmu toka shule za girls.
[emoji1]
Walevi nao walikuwa wanajinywea banana ghorofani kwenye kona.

Hopefully, stand mpya itakamilika, mambo yatakuwa poa.
 
Hakuna Stendi Pale Ni Eneo La Ajabu Sana Labda Watakapohamia Stendi Mpya Chini Ya Moshi Pazuri
 
I wish mamlaka zingesoma hili bandiko na kuanzia hapa, yaani hii ni starting point nzuri sana. Hongera kwa kuibua changamoto.
 
Binafsi nikusifu na nikushukuru kwa maono na hasa kwa kufikiri kiasi cha kuona na kujua mahali pa kuiandika hii kero,

haya yoote uliyaandika yana ukweli kwa 100% .

hivyo ni bora umejitokeza ukaliandika hili ambalo umeliona ili wahusika walifanyie kazi

mimi ninavyoona shida inaanzia pale nia za wahusika ama mamlaka ambao ndiyo wenye kupaswa kusimamia majukumu wanaposhindwa kuutambua wajibu wao na wapi wanapaswa kusimamia yapi

Kwa kuanzia tu ni kwamba mji kama moshi ina ofisi ya manispaa na ama halmashauri ama jiji kuna ofisi za mkurugenzi,meya maafisa mipango miji,afisa biashara kunao madiwani hawa woote hawafahamu ama hawajitambui wajibu wao

Nasema hivyo kwa sababu jengo la stand ya moshi wakati linajengwa hata kama ni miaka mingi huko nyuma lakini ramani na ujenzi wake ulipangwa vizuri sana hivyo ilipaswa tu kufanyiwa matumizi sahihi kama ilivyojengwa yaani sehemu ya kuweka ofisi za mabasi ibakie itumike katika uhalisia wa ramani ya ujenzi I kuwepo eneo la kupumzika wasafiri na sehemu chache za maduka ya huduma ambazo ni muhimu na za msingi kwa ajili ya mahitaji ya wasafiri ikiwepo kama biashara yenye kuhusiana na ubadilishaji wa fedha na maswala mengine yenye kuhusiana na fedha,air line ofisi,snacks shop,pharmas,ofisa usalama kwa rais(polisi),ofisi inayohusika na usimamizi wa kituo kwa ujumla,ofisi ya maulizo na maelekezo kwa wageni na mambo kama hayo hizi ni kwa uchache ila ni baadhi ya huduma ambazo ni muhimu kuwepo na siyo lazima kuwepo na maduka mia moja ama elfu kwa sababu hii siyo shopping mall bazaar bali hii ni stand ama bus terminal hivyo ni makosa kufikiria kwamba wakiondolewa wale wanaofanya biashara pale wataenda wapi na kama tunahitaji kuwa na standards lazima sasa tusiwaangalie wanaofanya biashara pale ila tukishakamilisha ofisi ambazo ni muhimu kuwepo basi kama kuna maeneo ya ziada yaliyobakia na ambayo yapo kwenye utaratibu wa ramani ya mjenzi yatolewe kwa maelekezo ya biashara gani zinahitajika kuwepo na siyo mpangaji kujiamlia kuweka biashara anayohitaji yeye bali tangu mwanzo ofisi ya afisa biashara ianishe biashara zinazohitajika na na zipi za kupewa kipaumbele

na kuwepo na ubao wenye kuelekeza huduma zinazopatikana ndani ya kituo
isiruhusiwe kuweka meza maeneo ambayo ramani haioneshi kama ilipaswa kupangwa meza na wala kusiwepo na kuweka miamvuli inayoonekana kama uchafu ama vichaka wapiga debe wapigwe marufuku kwa maana kutakuwepo na information desks moja ama zaidi kama kutahitajika
kuhusiana matoroli inawezekana kuweka ama kuruhusu kampuni yenye kueleweka ikafanya hiyo kazi kwa kuwekewa utaratibu wa kuvaa sare na vitambulisho na hapa utaona maana na uzuri wa stand ya mabasi

Hivyo haya yote yanawezekana iwapo tu watendaji wa mamlaka zenye kuhusika watajiondoa na kuacha kushiriki katika shughuli za kupangisha ama kujimilikisha biashara kwenye eneo la stand na ikiwa pia mipango ya stand itaachwa ipangwe na mamlaka bila kuingiza siasa ndani yake
zitangazwe tenda pale penye kuhitajika ili kusiwepo na upendeleo kwa afisa biashara ama kiongozi kutoka ofisi ya serkali ama chama cha siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…