Mufti kuku The Infinity
JF-Expert Member
- Sep 21, 2019
- 6,053
- 10,032
JobTrueTrue
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh!Stendi ni ya kishenzi sana ile, nilishawahi kuona katoto ka kichagga kamechuchumaa kanakunya huku raia wakimwangalia tu, naulizia watu mama wa yule mtoto yuko wapi wakasema mama yake anafanya kazi kwenye banda lile lile alilokuwa anakunya mwanawe na hashituki ukimwambia analeta ugomvi na kuuliza unataka mwanangu akanye wapi sasa.
Kampuni ya China kukamilisha ujenzi stendi ya mabasi ya kimataifa Tanzania mwaka 2021
(GMT+08:00) 2019-07-24 10:18:40
Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam
MRADI wa ujenzi wa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Kaskazini mwa Tanzania, unaotekelezwa na kampuni ya China Railway Jianchang Engineering (CRJE) unatarajiwa kukamilika Januari mwaka 2021.
Kampuni hiyo ya China inatekekeleza mradi huo kwa kushirikiana na makanadarasi wasaidizi watano kwa gharama ya Shililingi Bilioni 28.8 za Tanzania, na kukamilika kwake kunategemea kuchochoea shughuli mbalimbali za maendeleo na uwekezaji katika mikoa ya Kaskazini mwa nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki.
Akiwa Mkoani Kilimanajaro, akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa wa mabilioni ya shilingi, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema mradi huo ni maalum na wa kimkakati kwani uko miongoni mwa miradi ambayo Serikali ya Tanzania imekuwa ikiweka utaratibu wa kupelekea fedha kwenye miradi iliyotengwa na halmashauri.
"Serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huu…ujenzi wa stendi hii unatarajiwa kukamilika Januari 2021 na unafanywa na mkandarasi mkuu ambayo ni kampuni ya CRJE ya China ikishirikiana na makandarasi wasaidizi watano," alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Stendi hiyo itakayokuwa na ofisi, maduka, migahawa na hoteli, itakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 300 kwa siku ambayo yataingia na kutoka ambapo kati ya mabasi hayo 72 yanaweza kuegeshwa kwa wakati mmoja. Pia kutakuwa na maegesho ya ya magari binafsi 218, teksi 34 na bajaji na bodaboda 20.
Waziri Mkuu Majaliwa aliongeza kuwa mradi huo umelenga kuondoa msongamano wa mabasi katikati ya mji wa Moshi lakini pia kuongeza mapato ya Manispaa.
"Baadaye hapa mtaboresha biashara zenu, kukamilika kwa stendi hii, biashara ya teksi, daladala na bodaboda zitafanyakazi kubwa, hatutaki mipango hii ikwame," alisema
Serikali kupitia Manispaa ya Moshi mkoani kilimanjaro, ulisaini mkataba wa ujenzi wa kituo kipya cha kimataifa cha mabasi Ngangamfumuni na kampuni ya ya CRJE (East Africa) Ltd ya China mwezi Januri mwaka huu, 2019.
Ujenzi wa kituo hicho cha mabasi umeanza rasmi Januari 28 mwaka huu na utadumu kwa miezi 24 na unatekelezwa na kampuni ya ukandarasi ya CRJE ya nchini China ambayo imeahidi kukamilisha kwa wakati
Stand anaejenga serikali au watu wa Moshi??Kwa hichi ninachokiona stendi ya Moshi (ilivyokaa kishamba), kanda ya Ziwa (hususani Mwanza) wamewaacha mbali mnoo watu wa Moshi. Stand ya Mwanza imekaa kijanja sana, hii ya Moshi ni ushamba wa 100%
Ni kama ulienda huko kwa ajili ya kutafuta points za kuwasuta wana Moshi.Nikiwa katika pitapita zangu za kusafiri mwishoni mwa mwaka huu wa 2023 nikajikuta mikoa ya kaskazini, nikatua Stendi kuu ya mabasi ya mikoani pale Moshi mjini na hapo nikakutana na mambo ya ajabu, yaani uchafu, ushamba na ujinga wa kiwango cha juu kupitiliza tena mamlaka za serikali zikisimamia.
Hivi inakuwaje mji wenye sifa ya usafi kuliko miji yote hapa Tanzania na pilikapilika za kitalii kuwa katika hali ile. Kwa sifa za mkoa wa Kilimanjaro na asili ya kipekee ya wenyeji wake (maendeleo na ustaarabu) nisingetegemea kuyakuta haya.
Sote tunajua, kwa mgeni mji huanzia stendi na huishia stendi, na kwa kuwa watu wengi hupenda kujifunza au kutaka kuiga ya Kilimanjaro basi nimeyaweka wazi haya ili kuwananga wahusika yamkini labda watajirekebisha.
Na hapa JF nitachambua kwa kina kila kitu cha kijinga, ushamba, upumbavu na uchafu uliopitiliza nilichokutana nacho pale stendi kuu ya mabasi Moshi mjini(Kilimanjaro).
Kwanza nikiri wazi, japokuwa hii stendi ilijengwa zamani kidogo (zaidi ya miaka 20 iliyopita) tena katikati ya mji wa Moshi lakini ubunifu wake bado unaonekana uko kisasa sana (standard bus stand design) japokuwa matumizi yake bado yako kizamani mnoo kwa Moshi. Na haya ndio kwa haraka haraka niliyoyaona;
1. Hakuna eneo rasmi la abiria kusubiria (Passenger waiting area). Yaani eneo rasmi lililojengwa kusubiria abiria limejazwa meza za ovyo za walanguzi na mawakala wa kukatia tiketi za mabasi, biashara ndogo ndogo, milingoti ya bendera za CCM nk. Yaani pamekaa kitapeli kwa 100%.
2. Hakuna ofisi rasmi hata moja ya makampuni ya mabasi ndani ya stendi. Vyumba vyote vimepangishwa biashara zingine zisizohusiana na usafirishaji. (Baada ya kudodosa sana nikaelezwa fremu karibu zote za chini ndani ya hiyo stendi ni miradi rasmi binafsi ya wakubwa ndani ya Manispaa ya Moshi na baadhi ya vigogo wa CCM mkoa, wamejimilikisha hizo fremu kifisadi na kuwapangisha watu vile wanavyojisikia na ndio kikwazo cha kuzuia kukamilika ujenzi wa stendi mpya maeneo ya Majengo)
3. Stendi imegeuzwa kuwa ni soko rasmi la wamachinga. Kila biashara ya uchuuzi, ulanguzi mdogo mdogo, mama lishe, shoe shine, kupaka rangi kucha, utapeli, udangaji nk unaikuta ndani ya stendi. Yaani ile sio stendi bali ni soko holela.
4. Hakuna sehemu rasmi za kutupia takataka ndogo ndogo za mikononi, ni kama hakuna dustbin kabisa. Takataka unaweza kutupa popote na hakuna yoyote wa kukukataza.
5. Hakuna taa zinazowaka usiku eneo la parking za mabasi, kumebakia magofu ya milingoti ya chuma na mabaki ya taa chakavu zilizokufa.
6. Miundo mbinu ya kudumu imechakaa kupitiliza. Kingo za kuta kuzunguka stendi zimebomoka na kupauka, barabara za ndani zimejaa mashimo balaa. Ni kama mahandaki ya kule Gaza.
7. Eneo lote la stendi limezungukwa na utitiri wa vibanda holela, vya ovyo ovyo ambavyo kila mtu anajiwekea atakavyo.
8. Kwa zaidi ya asilimia 80 ya eneo la stendi kumejaa magari ya Noah, Hiace na Coaster za kwenda maeneo ya karibu karibu ndani ya Kilimanjaro na machache ya Arusha badala ya mabasi ya masafa marefu ndani na nje ya nchi.
9. Stendi imepakana na kuunganika na na dampo dogo la takataka. Yaani kunanuna na taka taka kuzagaa mara kwa mara huku baadhi ya watu wakienda haja ndogo za papo kwa papo.
10. Kuna vyoo vya kulipia vinavyotoa harufu kali kuelekea nje huku utitiri wa biashara zingine (zikiwemo za vyakula) zikizunguka maeneo hayo hayo. Huhitaji kuuliza vyoo viko wapi, harufu ya vyoo inakuelekeza vilipo.
11. Hakuna alama zozote au vibao vyenye kueleza na kuelekeza maeneo mbalimbali (ukiondoa vyooni). Yaani pamekaa kienyeji mnoo, utadhani watu wote ni wenyeji wanaoishi ndani ya stendi hiyo siku zote.
12. Hakuna eneo/ofisi ya maulizo (Customer enquiry). Ukipata shida au changamoto hujui uanzia wapi, uulize wapi, ulalamike wapi au umuulize nani.
13. Mazingira ya kiusalama ni sifuri. Emergency Assemble point hakuna, hakuna ofisi rasmi za polisi (kuna trafiki wanaokaa kaa njia ya kutokea mabasi muda fulani) nk.
14. Hakuna wabeba mizigo rasmi wala toroli rasmi za kubeba mizigo ya wasafiri. Kumejaa mateja na wapiga debe wanaomvamia msafiri yoyote mwenye mizigo na kumbabaisha.
15. Nyakati za usiku mara nyingi stendi hufungwa kabisa. Hivyo mabasi kulazimika kushushia abiria nje ya stendi.
16. Kumejaa kelele za muziki kutoka kwenye maduka, vibanda, baa uchwara na vispika vya matangazo ya biashara. Yaani pako vururu vururu.
17. Sehemu kubwa ya juu ghorofani ni kama haitumiki kabisa, sijui bado inajengwa! Ama imekosa wapangaji? Pamekaa kama gofu la kale.
18. Ndani ya jengo la stendi kuna vibanda umiza kwa ajili ya kuonyesha video, mpira, kuchoma CD, kudanga na kucheza kamari (betting).
19. Kumejaa takataka zilizozagaa balaa. Haijarishi ni muda gani, iwe asubuhi, mchana au usiku, ni machupa ya maji, vifungashio vya plastiki mpaka maganda ya matunda.
20. Parking ya magari binafsi na tax haileweki, kila mara huzaa migongano na mizozo. Hakuna tofauti kati ya tax rasmi, tax bubu na gari binafsi. Eneo la parking za magari lipo lakini utaratibu hauleweki na usalama ni duni. (Japokuwa kuwa kuna eneo rasmi, safi na bora la parking/stendi ya pikipiki).
21. Miundo mbinu ya kunawa mikono imebakia magofu ndani ya stendi, haifanyi kazi na bado ipo ndani ya stendi kama kumbukumbu ya kudumu!. Yaani usafi wa kunawa mikono uliletwa Moshi na Covid na ukafa baada ya covid kufifia.
Kwa leo niishie hapo, ni mengi nimejionea lakini kwa uhakika hayo ndio nimeweza kuandika, kama huamini siku moja pita pale na kushuhudia mwenyewe.
Huijui ccm wewe! Ni genge la wahuni Fulani hivi!Nikiwa katika pitapita zangu za kusafiri mwishoni mwa mwaka huu wa 2023 nikajikuta mikoa ya kaskazini, nikatua Stendi kuu ya mabasi ya mikoani pale Moshi mjini na hapo nikakutana na mambo ya ajabu, yaani uchafu, ushamba na ujinga wa kiwango cha juu kupitiliza tena mamlaka za serikali zikisimamia.