KERO Stendi kuu ya mabasi ya Moshi (Kilimanjaro) imejaa ujinga, upuuzi, uchafu na ushamba uliopitiliza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Duh!
 
Mwanza naona wamejitahidi sana upande wa stend waliamua kuweka pembeni ukiritimba wa maviongozi ya ccm kung'ang'ania pale mjini.
 
Moshi, Kilimanjaro
3 January 2024


Ujenzi unaendelea stendi mpya ya kimataifa Ngangamfuni International Bus Stand Terminal mjini Moshi mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Stendi hiyo itakayokuwa na ofisi, maduka, migahawa na hoteli, itakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 300 kwa siku ambayo yataingia na kutoka ambapo kati ya mabasi hayo 72 yanaweza kuegeshwa kwa wakati mmoja. Pia kutakuwa na maegesho ya ya magari binafsi 218, teksi 34 na bajaji na bodaboda 20. Soma zaidi:


10 Juni 2020
Chemchemi chini ya majengo ya stendi mpya Moshi yapasua vichwa vya wataalam


View: https://m.youtube.com/watch?v=HuJxVBQxZAESerikali mkoani Kilimanjaro imeongeza timu ya wataalam kufanya utafiti wa kina kubaini kiini cha chemchemi chini ya jengo la kituo kipya cha mabasi.

January 16th, 2019

UJENZI WA KITUO CHA MABASI CHA NGANGAMFUMUNI KUANZA RASMI​

Posted On: January 16th, 2019
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imesaini mkataba na kampuni ya ukandarasi ya kimataifa ya CRJE (EAST AFRICA LTD), kwa ajili ujenzi wa kituo cha Kimataifa cha mabasi cha Ngangamfumuni.
Ujenzi wa kituo hiki cha Kimataifa cha mabasi cha Ngangamfumuni (Ngangamfuni International Bus Stand Terminal ) utaanza rasmi Januari 17 mwaka huu mbapo hadi kukamilika mradi huu wa ujenzi utagharimu zaidi ya tsh bilioni 27.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi wa Manispaa ya
Moshi, Michael Mwandezi alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho utatekelezwa kwa awamu tatu tofauti huku ukichukua muda wa miaka miwili hadi kukamilika.

Hata hivyo Mwandezi alisema kuwa mradi huo mpya wa kituo cha mabasi utaibadilisha Manispaa hiyo katika Nyanja ya kichumi pamoja na utekelekezaji wa malengo ya Serikali kuhakikisha miradi yake inakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Moshi Rayamod Mboya alisema kuwa,ujenzi wa kituo cha Ngangamfumuni ulisubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa Manispaa ya Moshi na wadau wa usafirishaji hivyo kukamilika kwake kutaongeza hadhi pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi.

Alisema ujenzi wa kituo hicho cha mabasi utatekelezwa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni kukamilisha eneo la maegesho ili kuweza kuanza kazi ambapo awamu nyingine ni pamoja na kuanza ujenzi wa jengo la gorofa tano ambalo litakuwa na Hoteli,maduka, migahawa pamoja na ofisi mbalimbali.

Kukamilika kwa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha ngangamfumuni kutaifanya Manispaa ya kuwa mojawapo ya Manispaa zitakazokuwa na kituo ya mabasi chenye ubora zaidi nchini na ukanda wa Afrika Mashariki
 
Yote ni juhudi ya serikali sikivu ya mama yetu Suluhu
 
Kwa hichi ninachokiona stendi ya Moshi (ilivyokaa kishamba), kanda ya Ziwa (hususani Mwanza) wamewaacha mbali mnoo watu wa Moshi. Stand ya Mwanza imekaa kijanja sana, hii ya Moshi ni ushamba wa 100%
Stand anaejenga serikali au watu wa Moshi??
Mbona kama unataka kulaumu wasiohusika
 
Ni kama ulienda huko kwa ajili ya kutafuta points za kuwasuta wana Moshi.
 
Huijui ccm wewe! Ni genge la wahuni Fulani hivi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…