Stendi mpya ya mabasi ya Nyegezi jijini Mwanza imeanza kazi rasmi leo tarehe 5/6/2023 huku uzuri wake ukiwaacha hoi wananchi na kusema iko vizuri zaidi ya viwanja vingi vya ndege.
Ikumbukwe jiwe la msingi la ujenzi wa stendi hii liliwekwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Magufuli, hivyo wananchi wamemlilia tena kwenye uzinduzi wa stendi hii na kusema bila Magufuli kuwa Rais huenda ingewachukua miaka 50 kwa jiji la Mwanza kujengewa stendi nzuri kiasi hiki.
Uzuri wa stand siyo jengo pekee yake bali ni sustainability yake ya shughuli za stand.
Ikumbukwe kwamba jiji la Mwanza lina watu wengi sana, na ndilo linaloongoza kwa ongezeko la watu kuzidi miji yote ya Afrika Mashariki.
Lakini cha kushangaza, eneo la stand hii ya Nyegezi ni dogo sana, na baada ya miaka mitano, wataanza kuongelea kupata eneo jingine jipya la stand kwa sababu hili halitafaa kutokana na udogo wake..
Matatizo haya yapo karibia kila mji, na wala hatujifunzi. Mipango yetu ni ya muda mfupi mno.
Dar tulianza na Mnazi mmoja, watu wakaona panafaa sana. Baadaye pakawa finyu. Wakasema limepatikana eneo kubwa Ubungo. Ikajengwa stand Ubungo. Baadaye eneo likawa dogo, stand imepelekwa Mbezi, si ajabu baadaye ukasikia inapelekwa Kibaha.
Ni sehemu moja tu, ndiyo niliona watu wana mipango ya muda mrefu, yaani zaidi ya miaka 50. Nayo ni Njombe. Wao wana eneo kubwa sana la stand, kwenye sehemu waliojenga, inayotumika haifiki hata 50%, lakini eneo hilo lililojengwa halifiki hata 20% ya eneo lote lililotengwa kwaajili ya stand. Hivyo wana enwo kubwa limehifadhiwa kwaajili ya upanuzi kwa miaka ya mbeleni. Halafu ni mji usio na ongezeko kubwa la watu kama ilivyo Mwanza au Dar. Na nilipozungumza na mwenyekiti wao wa Halmashauri ya mji, akaeleza wazi kuwa wao hawaangalii miaka 10 au 20 bali miaka 100 mbeleni.
Zinapojengwa stand au hata huduma nyingine kama hospitali au shule, ni lazima wafanya mipango wajiulize, hiki tunachokijenga kitaendelea kufaa kwa muda gani, na baada ya huo muda, tutakapotaka kuongeza, eneo liko wapi?
Kati ya maeneo yaliyopangwa kwa kufikiria sana miaka ya mbeleni ni UDSM, nadhani hata UDOM, husikii wakiongelea kukosa maeneo ya upanuzi.