Stendi mpya ya mabasi Nyegezi yaanza kazi, ni zaidi ya Airport

Stendi mpya ya mabasi Nyegezi yaanza kazi, ni zaidi ya Airport

Isijeishia kuchakaa bila kutoa huduma stahii kama Ile ya Dom! Swala sio uzuriswala ni ipo kimkakati??
 
Stendi mpya ya mabasi ya Nyegezi jijini Mwanza imeanza kazi rasmi leo tarehe 5/6/2023 huku uzuri wake ukiwaacha hoi wananchi na kusema iko vizuri zaidi ya viwanja vingi vya ndege.

Ikumbukwe jiwe la msingi la ujenzi wa stendi hii liliwekwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Magufuli, hivyo wananchi wamemlilia tena kwenye uzinduzi wa stendi hii na kusema bila Magufuli kuwa Rais huenda ingewachukua miaka 50 kwa jiji la Mwanza kujengewa stendi nzuri kiasi hiki.

Legacy ya chuma
 
Hizi si ni kazi za manispaa/halmashauri husika.Naona sifa zibaenda kwa watendaji wa serikali kuu
 
Airport inakuaje katikati ya mji? Hiyo haina miaka 10 mbele itakuwa ya daladala. Mnasifia vitu kwa kuangalia rangi ,za majengo. Waliojenga hii ni akina nani wapi? Na huu nao ni uzalendo?
Kwani ikiwa stendi ya daladala kuna ubaya gani?
 
Wewe huna akili nadhani,hivi unaijua Stend ya Nyamongolo au unaisikia? kamuulize mkurugenzi wa Ilemela akueleze namna mapato yalivoongezeka baada ya kuanza kazi stend.Mwaka jana walikusanya b 9 + mwaka huu wanaweka malengo ya kukusanya b 13 hadi kufikia robo ya 3 mwezi march walikuwa walikusanya b 12. Usipende kuongea vitu usivojua Nyamongolo ni uti wa mgongo wa mapato ya Ilemela kwa sasa pamoja na Soko la kimataifa la dagaa na samaki pale Mwaloni.

Sent from my D6503 using JamiiForums mobile app
Uko sahihi sana
 
Ukweli hii stendi ni nzuri hebu fikiria nilipanda bus hapo mwaka jana 2022, Novemba nikisafiri kwenda Musoma na kushuka stendi mpya ya Musoma vitu viwili tofauti lakini zote zipo nchi moja.
Bukoba wao walishajikatia tamaa kitambo....

Magufuli aliwaambia walikosea kuchagua upinzani miaka ile...

Sasa kuna mbunge wa CCM lakin leo tupo 2023 nothing new

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Wewe huna akili nadhani,hivi unaijua Stend ya Nyamongolo au unaisikia? kamuulize mkurugenzi wa Ilemela akueleze namna mapato yalivoongezeka baada ya kuanza kazi stend.Mwaka jana walikusanya b 9 + mwaka huu wanaweka malengo ya kukusanya b 13 hadi kufikia robo ya 3 mwezi march walikuwa walikusanya b 12. Usipende kuongea vitu usivojua Nyamongolo ni uti wa mgongo wa mapato ya Ilemela kwa sasa pamoja na Soko la kimataifa la dagaa na samaki pale Mwaloni.

Sent from my D6503 using JamiiForums mobile app
Hicho unachosema ni matazamio ya huyo mkurugenzi wako! Mimi kila siku napita hapo kwa maana nasafirisha abiria ndo kazi yangu! Kwa sasa mkurugenz wako anapanga kurudisha magari madogo ya magu na sumve yaanzie buzuruga halaf unajifanya unajua kumbe hujui! Abiria wanakwepa tozo ya tsh 200 za pale terminal wanakimbilia kisesa! Tata nyingi zinaanzia kisesa.
 
Nasema kwamba Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kujivunia na kuiheshimu Sana,Ni zawadi tuliyopewa na Mwenyezi MUNGU kwa makusudi maalumu,Ni zawadi ipendezayo ndani ya Taifa letu, Ni zawadi ambayo yeyote ikiitazama lazima apate matumaini,faraja,furaha ,amani na Tabasamu Katika moyo wake.

Viongozi aina ya Rais Samia hujankwa nadra Sana hapa Duniani ,hawazaliwi kila siku na hawapatikani kila mahali.

Hakuna mradi utakaoshindikana au ambao hautamalizwa au kutekelezwa katika uongozi wa Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania,faraja ya wanyonge, Tumaini la waliokata Tamaa na nuru kwa waliogizani mh mama Samia suluhu Hassani mzalendo wa kweli,Jasiri muongoza njia,mama wa shoka,kiongozi shupavu na madhubuti.
Wewe ulitumbuliwa Sasa unataka mama akurudishe , umefeli na utasugua bench mpaka matako yaote sugu[emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom