JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jana nilifuatilia mjadala ulioanzishwa na JF kuhusu maoni ya sisi Wananchi wa kawaida kwenda kwa viongozi wetu hasa Wabunge, kwanza niwapaongeze sana kwa hicho walichokifanya na ninawashauri wakiendeleza kwa kuwa kero zipo nyingi.
Binafsi naamini wanasiasa ni watu wanaofuata upepo, kuna muda wanaweza kuliona jambo fulani la muhimu na wao watakiwa kulifanyia kazi, lakini kama halina mafufaa kwao au kama haliigiwi kelele wanaweza kuliacha kama lilivyo.
So, nilipoona JF wameanzisha kitu kama hiki inamaanisha kuwa ni kama tutakuwa tunawapigia kelele wakumbuke wajibu wao.
Povu langu mimi pia limfikie Mbunge wetu anayesimamia Jimbo la Ubungo ikiwezekana na viongozi wote ambao watakuwa wanahusika.
Suala la uchafu kwenye kituo cha Daladala cha Mbezi Mwisho kwa kweli ni kero na inatia kinyaa, hivi wao kwa kuwa wanatumia magari ya Serikali na hawaingii pale kituoni ndio maana wanatuchukulia poa ehh?
Kuna siku nimekuta mwanaume kasimama anakojoa katikati ya magari, na hakuna anayejali, harufu za mikojo zimesambaa, kibaya zaidi maeneo hayo ndipo ambapo kuna Watanzania wenzetu wanapanga bidhaa zao kuuza.
Hii ni hatari kwa afya, niwaambie wakati wanapambana kuwaondoa Wamachinga wajue na kufanya usafi au walizingatie hilo, kadiri siku zinavyoenda ndivyo uchafu unavyozidi kuongezeka.