Stendi ya Daladala Mbezi Mwisho ni chafu sana, Mbunge wetu hawezi kujua hilo ana mambo mengi

Stendi ya Daladala Mbezi Mwisho ni chafu sana, Mbunge wetu hawezi kujua hilo ana mambo mengi

Ile stendi ya mbezi mwisho tatizo sio uchafu ila imezidiwa, daladala bajaji na boda boda zimekuwa nyingi sana kaeneo kenyewe kadogo.
Huo pia ni uchafu na shisa ni saisa na pia ustarabu ni zero
 
Jana nilifuatilia mjadala ulioanzishwa na JF kuhusu maoni ya sisi Wananchi wa kawaida kwenda kwa viongozi wetu hasa Wabunge, kwanza niwapaongeze sana kwa hicho walichokifanya na ninawashauri wakiendeleza kwa kuwa kero zipo nyingi.

Acheni uvivu.Mnakichafua ninyi wenyewe na ndugu zenu wapitaji.Mjikusanye mkakisafishe!Onesheni "uzarendo"!
 
Stand ya Mbezi mwisho kweli ni chafu sana sana, wale wapiga debe wa stand ya Magufuli wanakojoa ovyo pale stand ya daladala

Machinga wanasababisha uchafu kwa bidhaa zao zilizoharibika wanatupa kwenye mitaro na kusababisha harufu mbaya ya uozo.

Hakuna utaratibu wa kupaga daladala, bajaji wala bajaji wanakaa ovyo ovyo tu.

Machinga nao ndio wanakaa kila kona ya stand wanajaa wao hata hakuna njia ya kupita watu mnapita kwa kubananaaana njia zote wameziba.

Kifupi Stand ya Mbezi inahitaji kuangaliwa upya ni kero kubwa sana.
Sasa Mbunge anahusika vipi? Akawaondoe wamachinga? Aka plant ustarabu ndani ya Wabongo?
 
Hapa ndipo ninapochoka nikiwafikiria watendaji wa wilaya. Amini usiamini itokee Mhe Rais ahoji kuhusu Suala la Uchafu wa Stand ya Mbezi au aseme Stand ya daladala mbezi imeshazidiwa uwezo, kwa kauli hiyo tu utaona jinsi viongozi na tunaomba kukiwa na mabadiliko ya wakurugenzi , watendaji na wakuu wa wilaya muikumbuke na wilaya ya Ubungo.
Tatizo sio ijengwe stendi nyingine shida ni Ushwahili wa Kitanzania
 
Jana nilifuatilia mjadala ulioanzishwa na JF kuhusu maoni ya sisi Wananchi wa kawaida kwenda kwa viongozi wetu hasa Wabunge, kwanza niwapaongeze sana kwa hicho walichokifanya na ninawashauri wakiendeleza kwa kuwa kero zipo nyingi.
TTACH=full]2479411[/ATTACH]
NI NANI ANACHAFUA?
 
Kukosa utaratibu stahiki katika vituo vyetu vya daladala kunachangia pokea kuongeza Huduma mbovu na uchafu.

Daladala nyingi hazikai katika mstari. Hakuna vitunza taka kwa abiria. Hakuna onyo kwa abiria kuhusu kutunza mazingira.
Watanzania kwa uchafu hatujambo
 
Ila wabongo wachafu sana

Inatakiwa watu wapigwe bakora

Mbona ukipita lugalo kusafi..najuwa

Jibu mnalo !

Ova
Yatakiwa wanaochafua miji wakamatwe,wapigwe faini na wafanye usafi
 
Jana nilifuatilia mjadala ulioanzishwa na JF kuhusu maoni ya sisi Wananchi wa kawaida kwenda kwa viongozi wetu hasa Wabunge, kwanza niwapaongeze sana kwa hicho walichokifanya na ninawashauri wakiendeleza kwa kuwa kero zipo nyingi.

Usafi wa hapo mbezi lous ni tatizo mm siwalaumu wasimamizi hapo maana usafi unafanyika kila siku tatizo ni stand kuwa ndogo imezidiwa sana sana.. wangeongeza na kule chini stand ya malamb iwe kubwa na pia upande wa goba kujengwe stand pia.. la sivyo hali ni ngumu pale.. watu ni wengi sana pale..

Swala la usafi ni tatizo letu binafsi sisi wabongo hatujielewi tena tuna shida uchafu ni km jadi yetu tusilaumu serikali kwa hili.

Kama mimi na wewe hatutakuwa na utaratibu wa kujizoesha kuwa wasafi basi hakuna kitachobadilika kamwe..
 
Jana nilifuatilia mjadala ulioanzishwa na JF kuhusu maoni ya sisi Wananchi wa kawaida kwenda kwa viongozi wetu hasa Wabunge, kwanza niwapaongeze sana kwa hicho walichokifanya na ninawashauri wakiendeleza kwa kuwa kero zipo nyingi.

Binafsi naamini wanasiasa ni watu wanaofuata upepo, kuna muda wanaweza kuliona jambo fulani la muhimu na wao watakiwa kulifanyia kazi, lakini kama halina mafufaa kwao au kama haliigiwi kelele wanaweza kuliacha kama lilivyo.

So, nilipoona JF wameanzisha kitu kama hiki inamaanisha kuwa ni kama tutakuwa tunawapigia kelele wakumbuke wajibu wao.

Povu langu mimi pia limfikie Mbunge wetu anayesimamia Jimbo la Ubungo ikiwezekana na viongozi wote ambao watakuwa wanahusika.

Suala la uchafu kwenye kituo cha Daladala cha Mbezi Mwisho kwa kweli ni kero na inatia kinyaa, hivi wao kwa kuwa wanatumia magari ya Serikali na hawaingii pale kituoni ndio maana wanatuchukulia poa ehh?

Kuna siku nimekuta mwanaume kasimama anakojoa katikati ya magari, na hakuna anayejali, harufu za mikojo zimesambaa, kibaya zaidi maeneo hayo ndipo ambapo kuna Watanzania wenzetu wanapanga bidhaa zao kuuza.

Hii ni hatari kwa afya, niwaambie wakati wanapambana kuwaondoa Wamachinga wajue na kufanya usafi au walizingatie hilo, kadiri siku zinavyoenda ndivyo uchafu unavyozidi kuongezeka.


nadhani ifike wakati sasa watz wafundishwe ustaarabu,ni jambo la ajabu kuona watu wanakula vitu hovyo na kutupa uchafu chini halafu bila aibu tunataka mbunge awajibike kwa lipi?watz tustaarabike unaponunua maji,juisi,pipi nk hakikisha unatupa vifungahio vyake mahali sahihi.mtu yuko kwenye usafiri anakunywa maji halafu chupa anakirusha nje ya dirisha halafu tunahitaji mbunge asimamie.hivi watu weusi ni nani alitulaani?swala la kutupa uchafu kwenye vifaa maalumu mpaka tufundishwe?
 
Hapa ndipo ninapochoka nikiwafikiria watendaji wa wilaya. Amini usiamini itokee Mhe Rais ahoji kuhusu Suala la Uchafu wa Stand ya Mbezi au aseme Stand ya daladala mbezi imeshazidiwa uwezo, kwa kauli hiyo tu utaona jinsi viongozi na watendaji wa wilaya watakavyoanza kukimbizana na suala litapatiwa ufumbuzi faster tu.

Hii inamaanisha kwamba viongozi wengi na watendaji ngazi za kati na chini Serikalini hasa Mikoa na Wilaya sio wawajibikaji kabisa, Kiongozi mzuri ni yule anayewajibika pasipo kutishiwa au kusukumwa au kuhojiwa na Mkubwa wake.

Binafisi natamani sana Mheshimiwa Rais awaondoe hawa watu. Hivi kweli suala la uchafu wa Stand ni mpaka Mheshimiwa Rais au Waziri Mkuu alitolee tamko!!

hivi kweli suala la Machinga kurudi Stand nyakati za jioni na usiku ni hadi wakuu wa Kitaifa watoe maelekezo kwa viongozi wa Wilaya.

Hivi Kweli Kuzidiwa kwa Stand ya daladala mbezi mwisho ni hadi viongozi wa Kitaifa waumize vichwa wakati kuna viongozi na watendaji wa Wilaya na Mkoa.

Unapokuwa kiongozi wa ofisini ni dhahiri kuna mengi hutayapata. Viongozi wilayani na mkoa wakiwa ni watu wakutoka wangekuwa wanapata mengi sana . Pia wangepata maoni ya wadau/wananchi namna ya kutatua au kupunguza baadhi ya changamoto.

Mfano, iwapo kungejengwa Stand ndogo upande wa juu yaani pale njia ya Goba kungepunguza msongamano kwenye Stand ya Sasa ya daladala kwani abiria wa msakuzi, msumi na wale wanaopanda gari za kwenda Mwenge na Tegeta kupitia Goba wangepandia hapo.

Mhe. Rais wangu Mpendwa na Mhe. Waziri Mkuu tunaomba kukiwa na mabadiliko ya wakurugenzi , watendaji na wakuu wa wilaya muikumbuke na wilaya ya Ubungo.
Viongozi wetu wanaenda na upepo,,,sasa swala kama hilo hadi Raisi aongee ndio wafanye,,sijui ni huwa hawaoni au nimakusudi yaani hadi unashindwa elewa tuna laana gani sisi??lakini nje na hilo watz wengi ustaarabu zero,,inahitajika elimu ya kutosha kuanzia kwa watoto wetu na mashulen huko kuhusu usafi wa mazingira,,,tusisubirie Ngo's zije zitufanyie
 
Viongozi wetu wanaenda na upepo,,,sasa swala kama hilo hadi Raisi aongee ndio wafanye,,sijui ni huwa hawaoni au nimakusudi yaani hadi unashindwa elewa tuna laana gani sisi??lakini nje na hilo watz wengi ustaarabu zero,,inahitajika elimu ya kutosha kuanzia kwa watoto wetu na mashulen huko kuhusu usafi wa mazingira,,,tusisubirie Ngo's zije zitufanyie
Ndugu yangu athari ya kutawaliwa na Mjerumani na Muarabu walituzoesha Viboko/Fimbo ndio maana hadi leo hii bila vitisho kazi haziendi, na hii hali imekwenda hadi kwa viongozi waandamizi wenye dhamana na Mawaziri yaaani hadi Rais au Waziri Mkuu ahoji ndipo wanaanza kukimbizana na kutekeleza.

Mbezi kuna kata za Mpiji, Msumi na Makabe yaani ukifika utafikiri upo USHIROMBO. Barabara haifahamiki itawekwa LAMI mwaka gani, ukienda Maeneo hayo unaweza kufikiri labda kuna ujenzi wa Makao Makuu kutokana na Magari ya kuuza maji yanavyopishana kwa wingi barabarani, Chaajabu Bomba la Maji lilishawekwa tangu kipindi cha JPM lakini suala la kuunganishiwa maji imekuwa ni wimbo usioisha.

Lakini itokee Mhe Rais ahoji tu kuhusu Barabara na Maji katika Maeneo hayo UTAONA JINSI MAWAZIRI WA WIRAZA HUSIKA NA WATENDAJI WATAKAVYOKIMBIZANA NA KUANZA UTEKELEZAJI.
 
Back
Top Bottom