Stendi ya Daladala Mbezi Mwisho ni chafu sana, Mbunge wetu hawezi kujua hilo ana mambo mengi

Ile stendi ya mbezi mwisho tatizo sio uchafu ila imezidiwa, daladala bajaji na boda boda zimekuwa nyingi sana kaeneo kenyewe kadogo.
Huo pia ni uchafu na shisa ni saisa na pia ustarabu ni zero
 
Jana nilifuatilia mjadala ulioanzishwa na JF kuhusu maoni ya sisi Wananchi wa kawaida kwenda kwa viongozi wetu hasa Wabunge, kwanza niwapaongeze sana kwa hicho walichokifanya na ninawashauri wakiendeleza kwa kuwa kero zipo nyingi.

Acheni uvivu.Mnakichafua ninyi wenyewe na ndugu zenu wapitaji.Mjikusanye mkakisafishe!Onesheni "uzarendo"!
 
Sasa Mbunge anahusika vipi? Akawaondoe wamachinga? Aka plant ustarabu ndani ya Wabongo?
 
Tatizo sio ijengwe stendi nyingine shida ni Ushwahili wa Kitanzania
 
NI NANI ANACHAFUA?
 
Kukosa utaratibu stahiki katika vituo vyetu vya daladala kunachangia pokea kuongeza Huduma mbovu na uchafu.

Daladala nyingi hazikai katika mstari. Hakuna vitunza taka kwa abiria. Hakuna onyo kwa abiria kuhusu kutunza mazingira.
Watanzania kwa uchafu hatujambo
 
Ila wabongo wachafu sana

Inatakiwa watu wapigwe bakora

Mbona ukipita lugalo kusafi..najuwa

Jibu mnalo !

Ova
Yatakiwa wanaochafua miji wakamatwe,wapigwe faini na wafanye usafi
 
Jana nilifuatilia mjadala ulioanzishwa na JF kuhusu maoni ya sisi Wananchi wa kawaida kwenda kwa viongozi wetu hasa Wabunge, kwanza niwapaongeze sana kwa hicho walichokifanya na ninawashauri wakiendeleza kwa kuwa kero zipo nyingi.

Usafi wa hapo mbezi lous ni tatizo mm siwalaumu wasimamizi hapo maana usafi unafanyika kila siku tatizo ni stand kuwa ndogo imezidiwa sana sana.. wangeongeza na kule chini stand ya malamb iwe kubwa na pia upande wa goba kujengwe stand pia.. la sivyo hali ni ngumu pale.. watu ni wengi sana pale..

Swala la usafi ni tatizo letu binafsi sisi wabongo hatujielewi tena tuna shida uchafu ni km jadi yetu tusilaumu serikali kwa hili.

Kama mimi na wewe hatutakuwa na utaratibu wa kujizoesha kuwa wasafi basi hakuna kitachobadilika kamwe..
 
nadhani ifike wakati sasa watz wafundishwe ustaarabu,ni jambo la ajabu kuona watu wanakula vitu hovyo na kutupa uchafu chini halafu bila aibu tunataka mbunge awajibike kwa lipi?watz tustaarabike unaponunua maji,juisi,pipi nk hakikisha unatupa vifungahio vyake mahali sahihi.mtu yuko kwenye usafiri anakunywa maji halafu chupa anakirusha nje ya dirisha halafu tunahitaji mbunge asimamie.hivi watu weusi ni nani alitulaani?swala la kutupa uchafu kwenye vifaa maalumu mpaka tufundishwe?
 
Viongozi wetu wanaenda na upepo,,,sasa swala kama hilo hadi Raisi aongee ndio wafanye,,sijui ni huwa hawaoni au nimakusudi yaani hadi unashindwa elewa tuna laana gani sisi??lakini nje na hilo watz wengi ustaarabu zero,,inahitajika elimu ya kutosha kuanzia kwa watoto wetu na mashulen huko kuhusu usafi wa mazingira,,,tusisubirie Ngo's zije zitufanyie
 
Ndugu yangu athari ya kutawaliwa na Mjerumani na Muarabu walituzoesha Viboko/Fimbo ndio maana hadi leo hii bila vitisho kazi haziendi, na hii hali imekwenda hadi kwa viongozi waandamizi wenye dhamana na Mawaziri yaaani hadi Rais au Waziri Mkuu ahoji ndipo wanaanza kukimbizana na kutekeleza.

Mbezi kuna kata za Mpiji, Msumi na Makabe yaani ukifika utafikiri upo USHIROMBO. Barabara haifahamiki itawekwa LAMI mwaka gani, ukienda Maeneo hayo unaweza kufikiri labda kuna ujenzi wa Makao Makuu kutokana na Magari ya kuuza maji yanavyopishana kwa wingi barabarani, Chaajabu Bomba la Maji lilishawekwa tangu kipindi cha JPM lakini suala la kuunganishiwa maji imekuwa ni wimbo usioisha.

Lakini itokee Mhe Rais ahoji tu kuhusu Barabara na Maji katika Maeneo hayo UTAONA JINSI MAWAZIRI WA WIRAZA HUSIKA NA WATENDAJI WATAKAVYOKIMBIZANA NA KUANZA UTEKELEZAJI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…