Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

stand ya ubungo ina ekari ngapi hadi hiyo ya mbezi kuwa ekari 24?? kwa Tz ya sasa ekari 24 hazitoshi maana kila. cku hali inabadilika na watu wanaongezeka wangetenga hata ekari 100 baadae zingepata matumizi maana sio. kila cku kulipa fidia tuu
 
 
Hakuna mahali nilipotetea ila nimeunga mkono stend kutolewa pale magar yangeendelea kuharibika hata tukipiga kelele sioni serikali ya ccm ikichukua hatua
Kusema ni "mipango ya Mungu" ni utetezi
 
Kufuatia ujenzi wa kituao hicho cha kisasa ktk eneo la mbezi mwisho ni

fursa kwa maeneo ya mbezi, kibamba, kiluvya nk, hoteli za kisasa zitahitajika, mall, Viwanja vya burudani n.k .
Wawekezaji changamkieni fursa hiyo,kwani stendi hiyo sio tu itahudumia mabasi ya mikoani bali pia mataifa mbalimbali.
Pongezi serikali ya mkoa
 
Wazo la kuhamisha Stand y'a mabasi toka Ubungo kwenda Mbezi Luis ni jema n'a kina faida nyingi, ikiwemo kupunguza msongamano/foleni kubwa hasa saa za asubuhi n'a jioni. Ushauri wangu Eneo la ujenzi wa kituo jipya mbezi Luis uzingatie mradi wa upanuzi wa barabara y'a Morogoro rd kwenda njia sita.
 
Mwanadamu sio Mungu ni jambo jema kuhamishia kituo cha mwendokasi ubungo ili stendi ya ubungo iende mbezi luis
WEWE WACHA KUTETEA UFUJAJI WA PESA. MIJI MIKONGWE KAMA LONDON KUNA VICTORIA STATION IMESIMULIWA KTK MAVITABU NA MAIGIZO HAIJAWAHI KUHAMISHWA SABABU YA KUWA KATIKATI YA JIJI HILO. IKO ZAIDI YA MIAKA 100. MWANZO ILIPOKUWA KISUTU ENEO LIKAWA DOGO NA KUHAMISHIA UBUNGO NDIO SAWA. sasa kuhamisha kwa sababu imekuwa katikakati ya jiji si sawa kwa vile baada ya jiji kufika kibaha hapi mbezi itakUWA KATIKATI YA JIJI TENA. TUFIKIRIE ZAIDI. MNAONA RAHISI KUCHUKUA PESA NA KUZITUMIA BILA UCHUNGU. WAULIZE WA LONDONI WAMEFANYAJE NA MJICWAO UNA WAKAZI MILLIONI 20. ENEO LA UBUNGO LINATOSHA KWA MAGARI YOTE YA UDART NA MIKOANI KWA MIAKA ZAIDI YA 100 IJAYO. NI AFADHALI KUNUNUA ENEO LINALOZUNGUKA STENDI MAANA HAKUNA HATA MGOROFA MENGI MUONGEZEE ENEO. HIYO FLYOVER ITASAIDIA MAGARI KUINGIA NA KUTOKA NA STENDI TAYARI IPI KUBWA YA UDART
 
Wataalam round ya kwanza hawakuliona hili!?.. Mbona tunachezea sana hela.
Wote wale waliofanya upembuzi yakinifu kuhusu huo mradi wajibu hizi tuhuma za uzembe uliokithiri na wafunguliwe jarada huko TAKUKURU kwa matumizi mabaya ya fedha za Umma.
 
Toka wanasema wanatengeneza hapo jangwani niliwaona hawana akili
 
Umeniacha hoiii!!!!

London haina watu milioni 20 mkuu!!! Yaani wasema theluthi wa idadi ya watu UK wanaishi London?

Hayo mengine nakubaliana nayo!


 
Serikali imewavunjia nyumba waliojenga mabondeni na kila siku wanawa lalamikia waliojenga mabondeni.
Halafu serikali hiyohiyo imeruhusu ujenzi wa karakana kuu ya mradi wake wa mabasi ya mwendo kasi hapohapo bondeni na kusababisha hasara ya mabilioni na imeamua kuicha hiyo karakana kuu iliyojengwa kwa mabilioni na kuhamia ubungo naitatumia mabilioni mengine kuirakabati iwe ya kisasa kukidhi vigezo
 
Siku ya uzinduzi wa ujenzi wa Kituo hicho cha Jangwani yeye JPM akiwa waziri mwenye dhamana na JK walikuwepo pale wote.Badala ya kushughulika na mandari ya mkondo wa maji kilikokuwa kinajengwa kituo, Wao walihangaika kumtumbua aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa DART wakati ule Bwana Cosmas Peter Takule.Kumbe hakuna mapana yasiyokuwa na ncha,Leo tunajionea madhara yenyewe.
Hata hivyo lini ulimsikia JPM akiongelea swala la Mwendokasi ?Mwenye nayo UDART mwamjua?Si yule aliyenunua UDA ?Tena ana kashfa za kuuza majineri huko Mwanza na Geita ? Na mwekezaji mwenza si yule alimkingia kifua kwa dhamana za serikali(Treasury Bills) kupata mkopo NMB kununulia mabasi ?Kama vile hamuoni kuna ukimya fulani umetawala mahali fulani....Fungukeni mpaze sauti huduma hii ni mkanganyiko wa kufa mtu mwanzo mwisho,Nasema tena haiwezi kutengemaa hadi Yesu arudi....
 
Tokea mwanzo humu humu Jf watu walisema jangwani hapafai
Ki ukweli wataalamu watanzania akili za zinawatosha wenyewe na familia zao......harafu VODA wakileta CEO kutoka nje mnapiga keleleleee!!!!!
 
Enviromental Impact Assessment vs Political WILL
 
Hawa watu siku zote hawafikiri vizuri na hawajawahi kujali maslahi ya watu. Hivi Ubungo terminal inatakiwa kubaki hapo ilipo ili kunusuru biashara na uwekezaji waliofanya watu au kama itawalipa fidia wenye hotel, guest na biashara.
Mwendo kasi ndio uende mbezi huko ndio watu wanauhitaji zaidi kuliko jangwani.
Mbezi mshavunjia watu hizo fidia watamlipa nani sasa
 
Tanzania haiwezi kubadilika hata siku moja. Hatufanyi kitu kuangalia mbele, kila mtu anafanya kitu kwa kuangalia muda akiwa ofisini, pale jangwani watu waliondolewa kupisha mkondo wa bahari, iweje tena serikali nao wakajenga? Leo tena wahamie Ubungo kwahiyo ile gharama iliyotumika Jangwani itatumika tena Ubungo. Teh teh sijawahi kuona hawa wasomi wetu
 
Unaweza kujenga kitu sehemu sahihi lakin natural calamities huwez kuzikwepa kama ikitokea zikaja tofaut hata huko ma mbele wanahangaika na haya majanga
Pale waliubana mto what will be happen
 

Tena UDART yenyewe imeshaanza kupooza mara magari yameharibika mengi. Mara wanaburuzana mahakamani. Siombei mabaya katikati ya mazuri tuliyotegemea but hawa UDART wanatoa huduma zilizofubaa, huduma zimezeeka na kutia kichefuchefu. Yale magari ile milango yake siku siyo nyingi wataajiri makonda wa kufunga na kufungua.

Wakazi wa Mbezi/kimara wameshapata adhabu ya kutosha kabisa kabla hata hayo magari hayajaoga mafuriko ilikuwa shida na utumbo mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…