Hizi mada tangu zianze humu,hazijawahi toa mshindi
Mimi siku zote huwa naamini MUNGU yupo kwa swali moja tu,ambalo kwa vyovyote vile lina jibu moja tu
Tuchukulie mfano mdogo tu,Jicho! lina lens kwa ajiri wa kukusanya Mwanga na Retina kwa ajiri ya kutengeneza image,halafu kuna mfumo unaofanya hio taswira iliyoundwa kutafasiriwa na ubongo
Jicho lina mapungufu mengi sana.
Haliwezi kuona nyuma ya kichwa, haliwezi kuona beyond visible light (gamma rays, ultraviolet rays etc)
Jicho hili lenye mapungufu yote haya haliwezi kuwa limeumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
Lingekuwa limeumbwa na Mungu huyo, lisingekuwa na mapungufu, huyo Mungu si Mungu wa mapungufu.
Swali la kujiuliza hivi ni Nani aliyewaza kabla kuwa Jicho inabidi liwe katika muundo huo ili lifanye kazi,au lens inabidi ikae hapa na Retina ikae hivi ili jicho lifanye kazi sawasawa
Ukishaanza kuuliza kwa minajili ya "nani" na "aliwaza" tayari ushajipa jibu kabla hata hujamaliza kuuliza swali, unejilengesha kwenye jibu unalolitaka, kwa kujua ama kutojua. Swali lenye maana zaidi ni "nini kilifanya hivyo" si "nani aliwaza".
Ni kama vile umekuta jani la muembe mlangoni mwako, badala ya kuuliza "ni nini kimelifanya jani hili la muembe liwe hapa mlangoni mwangu" unauliza "ni nani kalileta jani hili la muembe mlangoni mwangu". Ikiwa jani limepeperushwa na upepo, swali lako la kutafuta "nani" litakuwa limeanza katika msingi potofu.
Sasa tuna nadharia 2,moja inadai hakuna sababu yoyote iliyofanya jicho liwe katika muundo huo,bali imetokea tu by mere chance and series of random mutations ndani ya mda mrefuuuuu
Hivi kweli hakuna sababu kwanini Jicho liwe na kope?kope hazina kazi?
Kama zina kazi,lazima kuwe na sababu ya kope kuwepo
Na kama kuna sababu,lazima kuwe na yule aliyeifikiria hio sababu mwanzoni kabisa
Hata kama kuna sababu, sababu hiyo si lazima iwe Mungu. Kimsingi unapinga evolution, kitu ambacho sina hakika unakielewa, lakini hata ukifanikiwa kupinga kwa ukamilifu evolution, hilo halithibitishi Mungu yupo. Hili si suala la mutual exclusivity kwamba if its not evolution, then it is creation by God.
It is possible that the answer is neither evolution nor creation by God.
Kama kuna betri kwenye smartphone yako,na kuna sababu ya betri kuwepo,basi lazima kuwe na mtu aliyeiona hio sababu kabla hajaweka hio betri
Unaelewa kwamba hii argument inaonesha Mungu hayupo, haioneshi Mungu yupo?
Kimsingi unasema complex systems lazima ziwe na designer, haziwezi kuwepo tu bila ya designer.
Mungu naye ni very complex, hivyo, naye atahitaji designer.
Mungu akishahitaji designer si Mungu huyo.
Na designer wake atahitaji designer, ad nauseum, ad infinity.
Kwa hiyo habari yako inayosema complex systems zinahitaji designer inaonesha Mungu hayupo, haioneshi Mungu yupo.
Point ni kwamba haijalishi Jicho limetokea vipi,by evolutionary process au by design lazima kuwe na sababu kwanini jicho linatakiwa kua katika muundu huu,na sababu(reasoning) ni sifa ya intelligent mind
Have you ever heard of the anthropic principle?
So we have to affirm the existence of intelligent mind(or mechanism) otherwise our eyes have no purpose(a proposition which is utterly absurd)
Kama unasema kwamba huwezi kupata complexity bila ya kuwa na intelligent design, unaelewa kwamba umekubali Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ambaye hana muumba hawezi kuwepo?
Mwisho,Kuamini Evolution as mindless process unahitaji a lot of assumptions zaidi kuliko kuamini kuwa Evolution iliyotokea kwa msaada wa intelligent agent(s)
Mtu hahitaji kuamini evolution ili kuona kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
The problem of evil does not need evolution to validate its successful critique of the God idea.
Na kulingana na Occam's razor,ni sahihi kwa mtu mwenye busara kukataa Darwinism
Hata ukikataa Darwinism, kukataa huko haku prove Mungu yupo. Hili si swali la mutual exclusivity kwamba kuna majibu mawili tu, Darwinism na Mungu, inawezekana kabisa vyote viwili vikawa vina makosa na jibu likawa si Darwinism wala Mungu.
Nikikutaka u prove Mungu yupo, hilo si sawa na ku disprove Darwinism. Unaweza ku disprove Darwinism lakini ukawa huja prove Mungu yupo, katika ulimwengu ambao Darwinism na Mungu vyote ni makosa.
Unaweza ku prove Mungu yupo?
Habari zako zote juu zina faulty logic, logical non sequitur (unaunganisha mambo ambayo hayana muungano), ukiona jicho liko complex una conclude limeumbw ana Mungu, wakati actually ukisema hakuna complexity ambayo inatokea bila kuumbwa unasema Mungu hawezi kuwepo.
Unaelewa kwamba kusema complexity lazima iwe na muumbaji ni kusema Mungu hayupo, si kusema Mungu yupo?