Ndugu Kiranga, sio kwamba hauna hoja, unayo. Mimi naelewa hasa kinachokutatiza.
Kuna masuala kadhaa usiyo yaelewa bado. Kuna elimu hizi: saikolojia, falsafa na teolojia bado huzielewi na kwa sababu hiyo huelewi pia sayansi. Ni kutoelewa, kwasababu unawezaje kukataa wewe siyo uthibitisho wa kuwepo Mungu lakini ukakubali hadumi inathibisha uwepo wa vimelea au viumbe vingine tusivyoviona kwa macho?
Bado ni tatizo hilohilo la kutoelewa, kama sayansi inathibisha kwamba DNA hutawala maisha ya mtu daima, lakini ukakataa dini inaposema roho ndiyo hutawala maisha ya mtu. Hii ni kwa sababu huelewi kipi unakiegemea na kukifuata na kipi inakithibitisha.
Madai yako yote yanaonyesha kwamba bado hujaelewa Mungu ni nani na nini? Uliza au jielimishe! Kwa sababu huelewi na humjui Mungu ndiyo maana unalalamika kwanini alishindwa kuumba ulimwengu usiyo na matatizo badala yake akaumba ulimwengu huu wenye matatizo na kila aina ya uovu; na hivyo unaelewa hakuna uthibitisho wa Mungu kwa sababu tu ya dunia ilivyo. Yaani hata dunia yenyewe ilivyo kando na matatizo yaliyomo, bado akili yako haitambui? Sasa kama jambo dogo kama hilo huelewi, utawezaje kujijua na kuelewe wewe mwenyewe? Na kama wewe mwenyewe hujijuwi na kujielewa, unawezaje kujua na kuelewa Mungu?
Huwezi kudai matatizo hayawezi kudhibitisha jambo jema. Yaani hivi: kwa vile kuna matatizo, basi hakuna mema. Kama unashindwa kuuthibisha ukweli kwenye matatizo huwezi kuona uzuri kwenye wema.
Unaposhindwa kuelewa zaidi ni pale unapofikiri Mungu ni contradiction lakini wewe ni facts and not contradiction! Wewe huoni kama ni fact ya Mungu, lakini unaona Mungu ni contradictions wakati huohuo wewe ni facts, lakini hujioni kama ni contradiction s!
Ndugu Kiranga uthibitisho wa Mungu uko ndani yako na siyo sehemu nyingine yeyote. Hiki kilichopo nje unachokiona ni uthibitisho ya kile kidogo kilichomo ndani yako. Kama hukioni hiki kidogo kilichopo nje maana yake hauna sayansi-hauna uthibitisho hivyo, unakataa hicho kilichomo ndani yako, ambacho kwa chenyewe, hiki kinachoonekana nje kinatokana na hicho kilichomo ndani yako, ndiyo Mungu.
Katika msingi huo, sayansi kwa maana nyingine ni uthibisho unaomthibisha Mungu, ambae yuko ndani yako anaejithibisha na kujidhihirisha kwa maarifa ya sayansi kadiri ya wakati.
Sasa unaposema unataka uthibitisho wa Mungu: sijui ni uthibitisho gani zaidi ya huu wa: wewe mwenyewe ndani yako, ndiyo roho, wewe mwenyewe kama umbo la kuonekana, ndiyo mwili; dunia na vitu vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyooneka, maarifa kama tulivyonayo, ndiyo sayansi, saikolojia, falsafa na teolojia?