Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Misimamo yetu ya kuwepo Mungu au kutokuwepo ni zaidi ya sababu tunazotumia hapa kubishania,watu tumegawanyika makundi tofauti wapo wenye elimu na wasiokuwa na elimu na wengineo ila wote kila mmoja ana msimamo wake juu ya suala la Mungu na
kila mmoja anajaribu kutetea msimamo wake.
Msimamo kila mtu anao, hilo halina ubishi.

Ila fact ni moja tu.

Sasa unaijuaje fact?

Kwa uchunguzi, kwa uthibitisho, si kwa imani.

Sasa mbona watu wanataka kujua fact ya kuwepo Mungu kwa imani badala ya uchunguzi na uthibitisho?
 
Wewe mwenyewe una kazi ya kuaminisha watu humu kuwa hakuna Mungu halafu unasema hautaki kuamini,huko pakodaiwa kuwepo Mungu wewe unajua kuwa hayupo au unaamini tu kuwa hatakuwepo?
Wapi naaminisha watu? Na inakuwaje mtu mmoja akamuaminisha mwingine?

Aanayeaminisha inakuwaje asisitize uchunguzi na uthibitisho badala ya imani?
 
Ndugu kiranga
Maswali yangu kwako
1: kipi kilikufanya ukathani hakuna Mungu?

2:Je kabla ya kutokuamini Mungu yupo kwanini ulikuwa unaamini?
Shukrani maswali yangu ndiyo hayo mkuu
 
1. Nilipokuwa na mika 19 nilisoma hiki kitabu nilicho attach kinaitwa "Philosophy of Religion: An Anthology", mwanzo mpaka mwisho. Sehemu iliyonionesha Mungu hayupo ni hapo PART IV The Problem of Evil 276.

Kama unaweza kusoma na una wasaa kipitie, ni kitabu kizuri sana kwa sababu kina point zote za wanaosema Mungu yupo na wanaopinga kuwepo kwa Mungu, halafu ni anthology imekusanya maandishi ya wasomi wa miaka na miaka.

2. Kwa sababu nilikuwa mdogo sana, sina ujuzi sana, sijasoma sana, nilifuata dini ya wazazi wangu tu.
 
Attachments

Nimeshakipakua na kuanza kukisoma, shukrani kwa kukiweka hapa tuongeze maarifa.

Kwa maoni yako, kila anayekisoma atahitimisha kwamba hakuna Mungu?
 
Hapana, sina uwezo wa kujua mawazo ya kila anayekisoma yataishaje.

In fact, kitabu kina arguments nyingi sana na nzuri sana za kutetea uwepo wa Mungu.

Moja ya kitu ambacho ningependa ni kuona watetezi wa uwepo wa Mungu wanatetea kwa arguments zilizosheheni usomi, sasa hivi naona wanapwaya wanakuja kiubishi wa Simba na Yanga zaidi.

Ni kama kipo nusu kwa nusu, kimeelezea mpaka habari za pantheism na aina nyingi sana za imani za Mungu/ miungu ambazo hapa hatujapata hata nafasi ya kuzijadili, kwa sababu ya upeo mdogo wa wengi wetu.

Soma vizuri tu, ni anthology nzuri sana, yani ukimaliza kitabu hiki kama umekisoma vizuri, ni sawa na umefanya graduate school level course katika comparative religion.
 
Unayoyasema ni kweli, kwa kuperuzi haraka haraka nakubaliana na maneno yako. Pia nimependa ulivyojibu kwa busara kwamba maamuzi ya mwisho baada ya kusoma na kuelewa hichi kitabu yatakuaje. Ni kweli, kuna wengine itawafanya waelewe zaidi hoja zao juu ya uwepo wa Mungu, na kuna wengine itawaimarisha juu ya kutokuamini kwao kwamba Mungu hayupo na kuna kundi la mwisho litachanganywa kabisa likose pakusimamia.

Hata chuo au darasani, wote mnasoma mtaala mmoja, waalimu wale wale, mtihani ule ule lakini bado hamfaulu kwa kiwango sawa, na mnatofautiana sana namna mtakavyoelewa na kutumia hiyo elimu na ujuzi baada ya shule.

Wanaochukulia mjadala kama ushabiki na ushindani ni wakuvumiliwa tu, ilimradi wasikie kiwango cha kufanya hasira zishindwe kuzuilika na kuharibu mjadala.

Msamaria
 
Kujadiliana na mtu kama wewe sioni tabu kabisa.
Kwa sababu unaweza ku reason.

Kuna watu wana reason, hata kama hukubaliani nao, mnapingana kabisa, lakini mazungumzo yanawajenga wote mnabadilishana mawazo, mnapeana changamoto kuongeza wigo wa mawazo.

Watu kama wewe nikiwapata kujibizana nao nitaweza hata kuelewa mengi zaidi.

Lakini hawa wanaong;ang'ania "lazima nishinde mjadala nimuoneshe huyu Kiranga mimi ni zaidi yake" au "Mungu wangu ni mkuu w amajeshi hashindwi kitu, hata akishindwa, ushindi ndio unageuka kusinda" kujadiliana nao ni tabu sana.
 
Niliwahi kukuandikia faragha kukushukuru kwamba licha ya kutofautiana kwenye baadhi ya misimamo na imani, umekua msaada mkubwa sana kwangu kujifunza mambo mengi, nimeona ijulikane hapa kwamba kutokukubaliana jambo na mtu haileti uadui au ubishani usio na tija, vinginevyo tutamlazimisha profesa wa watu aseme huo hata sio ujinga. Naomba nikushukuru kwa hilo mkuu.

Staha, uvumulivu na kujadili kwa hoja kunaonyesha kiwango cha ukomavu, sijafikia huko lakini nakushukuru umenisaidia kuianza hiyo safari.

.
 
Kwenye jangwa kubwa lisilo na maji, kuona chemchemi ya maji safi kunafurahisha roho kama kuona uandishi wa aina yako hapa JF.

Ni rahisi kumfurahia mtu mnayekubaliana naye.

Ukiona namfurahia hivi mtu ambaye sijakubaliana naye maana yake ni kwamba hata katika kutokubaliana kumeonekana uwezo mkubwa wa kupambanua mambo.
 
Hizi mada tangu zianze humu,hazijawahi toa mshindi

Hilo mimi nishalisema mara kadhaa humu.

Hizi mada huwa zinajirudia rudia sana.

Kimsingi, kama huwa kuna tofauti, basi tofauti hiyo/ hizo huwa ni kwenye kichwa cha mada tu lakini maudhui huwa ni yale yale tu.

Na kwangu huwa siziangalii hizi mada kutumia mzani wa kushinda na/ au kushindwa.

Kilicho muhimu zaidi kwangi ni nani au ni upande upi unaoweza kunionyesha ushahidi utaonishawishi kuhusu uwepo au kutokuwepo.

Ahsante nawe kwa kuona kama nionavyo mimi.
 
Ukitaka kutopata hitimisho kwa jambo lolote, hata uwepo wako wewe mwenyewe kama ni kweli upo au si kweli, unaweza kutopata hitimisho.

Absolutely everything is built on some assumptions, mostly axiomatic.

So it is a matter of shifting the framework.Dig to the assumption.

Oh, so two parallel lines don't meet? Forever? Forever ever? Have you tried to test for forever ever?

So the question then becomes, how do you decide anything is true?
 
Dunia ingekuwa na perfection unayoidhania ingekuwa very boring. Changamoto zilizopo zinatupa sababu ya kutaka kuishi

Actually, ukitaka kwenda kwenye physics ya themodynamics na enropy, the only perfection is nothingness.

Lakini hilo, na ulilosema wewe, havisemi lolote kuhusu Mungu kuwepo.

Inawezekana kabisa ukawa umesema kweli - in fact your assertion is even more shocking than you posited-

Ulimwengu ungekuwa na perfection, usingekuwepo.

Kwa sababu, hali pekee yenye perfect entropy ni nothingness, ukianza kuweka chochote, kuondoka kwenye hiyo nothingness, unaharibu perfection.

Kwa physics.

Lakini hilo halimaanishi Mungu yupo.

Na kwa kweli, linatupa swali.

Kama Mungu yupo, ameshindwa kuumba ulimwengu ambao una perfection, lakini si nothingness?

Kuna kitabu cha Jim Holt "Why Does The World Exist: Aan Existential Detective Story" kinaelezea hili.

Nakitafuta, nitakiweka hapa. Nataka kuwa najibu maswali kwa vitabu zaidi ili tulingane na wengi kwenye majadiliano.

Hii hapa ni TED Talk yake on the subject, sijaiona hi video bado hata mimi.Nimesoma vitabu vyake..

Msimamo kila mtu anao, hilo halina ubishi.

Ila fact ni moja tu.

Sasa unaijuaje fact?

Kwa uchunguzi, kwa uthibitisho, si kwa imani.

Sasa mbona watu wanataka kujua fact ya kuwepo Mungu kwa imani badala ya uchunguzi na uthibitisho?
Ni uchunguzi gani uliyofanyika wa kwenda kumsaka Mungu na majibu yakawa hayupo? Maana huku kusema Mungu angekuwepo ingekuwa hivi sijui isingekuwa vile haiwezi kuwa fact.

Sasa wewe umetumia nini kusema hayupo?
 
Back
Top Bottom