Unawezaje kusema Mungu ni hadithi tu na hapohapo ukasema facts siyo hadithi?
Kwa sababu maelezo ya kuwepo huyo Mungu yana contradiction, facts hazina contradiction.Kitu kikiwa na contradiction, tayari ukweli wake ushakuwa challenged.
Imekuwaje Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote akaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?
Hii habari ina contradiction, unaweza kutatua contradiction hii?
Kama unaona Mungu ni hadithi na siyo facts ni kwa vipi umeelewa Mungu ni hadithi na facts siyo hadithi?
Kwa sababu habari za kuwepo Mungu zina contradiction, facts hazina contradiction.Kitu kikiwa na contradiction ukweli wake unakuwa challenged.
Unadai unataka udhibitisho wa Mungu kuwepo ni kwa vipi wewe hapo unaweza kudai siyo udhibitisho na facts za uwepo wa Mungu?
Sijataka "udhibitisho" nimetaka "uthibitisho", unaelewa tofauti?
Wewe unaweza kuniambia ni vipi mimi ni uthibitisho wa kuwapo Mungu?
Nimekuulizza swali, nimekwambia nithibitishie Mungu yupo.
Wewe unatakiwa kunijibu, kama unasema mimi ni uthibitisho wa kuwapo kwa Mungu, unanitakiwa unioneshe hatua kwa hatua mlolongo wote unaoonesha kwamba mimi ni uthibitisho wa kuwepo kwa Mungu.
Hujafanya hivyo. Umeligeuza swali kivivu kwangu, mimi nithibitishe uwepo wa Mungu kwa niaba yako wakati mimi ndiye niliyekuuliza wewe uthibitishe uwepo wa Mungu?
Huo uwepo wa Mungu unaukubali kweli? Mbona unanipa mimi nisiyeamini kuwepo Mungu kazi ya kuthibitisha kuwapo kwake, baada ya mimi kukuuliza wewe uthibitishe kuwapo kwa Mungu?
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Na kama wewe unaijua vema sayansi ambayo ndiyo unaiegemea kuhusu Mungu, dunia na mtu unadhibitisha nini juu ya dhana hii ya sayansi ambayo ni kani (gravitation) na dhana iliyomo katika mafundisho ya dini kuhusu Mungu ni nguvu inayotawala na kuendesha ulimwengu na vyote vilivyomo?
Wapi nimesema naijaua vema sayansi? Kuijua vema sayansi maana yake ni nini? Tofauti ya kuijua vema na kuijua kidogo sayansi iko wapi?
Unaweza kuthibitisha (si kudhibitisha) Mungu yupo na si hadithi tu?