Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Unawezaje kusema Mungu ni hadithi tu na hapohapo ukasema facts siyo hadithi?
Kama unaona Mungu ni hadithi na siyo facts ni kwa vipi umeelewa Mungu ni hadithi na facts siyo hadithi?
Unadai unataka udhibitisho wa Mungu kuwepo ni kwa vipi wewe hapo unaweza kudai siyo udhibitisho na facts za uwepo wa Mungu?
Na kama wewe unaijua vema sayansi ambayo ndiyo unaiegemea kuhusu Mungu, dunia na mtu unadhibitisha nini juu ya dhana hii ya sayansi ambayo ni kani (gravitation) na dhana iliyomo katika mafundisho ya dini kuhusu Mungu ni nguvu inayotawala na kuendesha ulimwengu na vyote vilivyomo?
 
Uko kama binti alieumizwa moyo alafu anabakia na wazo hapa duniani hakuna mapenzi ya kweli. Wayahudi baada ya Hitler kuua wengi wao wakati wa vita kuu ya pili , wengi walikuja na wazo kuwa hakuna Mungu. Waliamini kama angekuwepo asingekubali yatokee hayo yaliotokea. Wewe Kiranga utakuwa umeathirika kisaikologia baada ya machungu yaliokupata ukakosa majibu sio kosa lako . You need help brother !! There are many ways to prove GOD exists and he loves you very much . There is no true friend like him , just call him and he will come to you in ways you can not understand with your human mind.
 
Unawezaje kusema Mungu ni hadithi tu na hapohapo ukasema facts siyo hadithi?

Kwa sababu maelezo ya kuwepo huyo Mungu yana contradiction, facts hazina contradiction.Kitu kikiwa na contradiction, tayari ukweli wake ushakuwa challenged.

Imekuwaje Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote akaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?

Hii habari ina contradiction, unaweza kutatua contradiction hii?

Kama unaona Mungu ni hadithi na siyo facts ni kwa vipi umeelewa Mungu ni hadithi na facts siyo hadithi?

Kwa sababu habari za kuwepo Mungu zina contradiction, facts hazina contradiction.Kitu kikiwa na contradiction ukweli wake unakuwa challenged.

Unadai unataka udhibitisho wa Mungu kuwepo ni kwa vipi wewe hapo unaweza kudai siyo udhibitisho na facts za uwepo wa Mungu?

Sijataka "udhibitisho" nimetaka "uthibitisho", unaelewa tofauti?

Wewe unaweza kuniambia ni vipi mimi ni uthibitisho wa kuwapo Mungu?

Nimekuulizza swali, nimekwambia nithibitishie Mungu yupo.

Wewe unatakiwa kunijibu, kama unasema mimi ni uthibitisho wa kuwapo kwa Mungu, unanitakiwa unioneshe hatua kwa hatua mlolongo wote unaoonesha kwamba mimi ni uthibitisho wa kuwepo kwa Mungu.

Hujafanya hivyo. Umeligeuza swali kivivu kwangu, mimi nithibitishe uwepo wa Mungu kwa niaba yako wakati mimi ndiye niliyekuuliza wewe uthibitishe uwepo wa Mungu?

Huo uwepo wa Mungu unaukubali kweli? Mbona unanipa mimi nisiyeamini kuwepo Mungu kazi ya kuthibitisha kuwapo kwake, baada ya mimi kukuuliza wewe uthibitishe kuwapo kwa Mungu?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Na kama wewe unaijua vema sayansi ambayo ndiyo unaiegemea kuhusu Mungu, dunia na mtu unadhibitisha nini juu ya dhana hii ya sayansi ambayo ni kani (gravitation) na dhana iliyomo katika mafundisho ya dini kuhusu Mungu ni nguvu inayotawala na kuendesha ulimwengu na vyote vilivyomo?

Wapi nimesema naijaua vema sayansi? Kuijua vema sayansi maana yake ni nini? Tofauti ya kuijua vema na kuijua kidogo sayansi iko wapi?

Unaweza kuthibitisha (si kudhibitisha) Mungu yupo na si hadithi tu?
 
Uko kama binti alieumizwa moyo alafu anabakia na wazo hapa duniani hakuna mapenzi ya kweli. Wayahudi baada ya Hitler kuua wengi wao wakati wa vita kuu ya pili , wengi walikuja na wazo kuwa hakuna Mungu. Waliamini kama angekuwepo asingekubali yatokee hayo yaliotokea. Wewe Kiranga utakuwa umeathirika kisaikologia baada ya machungu yaliokupata ukakosa majibu sio kosa lako . You need help brother !! There are many ways to prove GOD exists and he loves you very much . There is no true friend like him , just call him and he will come to you in ways you can not understand with your human mind.
Hujathibitisha Mungu yupo. Thibitisha Mungu yupo.

Hizo nyingine kelele tu.
 
Tunapinga uwepo wa Mungu kwa sababu sifa zake ---'-zinazo muelezea hazina mantiki. ....

Kwani kilicho umba huu ulimwengu lazima kiwe/awe mungu ambaye hawezi kuthibitika uwepo wake? ...

Yaani hapo inaonyesha wazi kuwa Unaamini uwepo wa huyo mungu kwakuwa unatokea katika jamii iliyo karilishwa kuhusu uwepo wake

Unataka Mungu athibitishwe kwa namna gani labda? Maana ukiambiwa kwamba uumbaji wote ni kazi ya Mungu bado unabisha. Chanzo cha haya yote dunia jua nyota na mpangilio wote wa maisha ya kila kiumbe ni uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Huwa nashangaa sana wanasayansi wanashindwa vipi kujua kwamba kuna Mungu. Angalia kitu kama DNA, jicho, brain nk nk, ni vitu complex sana na viko well arranged kwa ajili ya kusapoti maisha na kubeba taarifa husika za viumbe. Angalia namna ambavyo mimba inatunvwa na kiumbe kinavyo develop ndani ya uterus ya mwanamke. Kila kitu kiko planned, organized.

Nani au nini ni organizer? The planner?
 
Thibitisha kuwa Mungu yupo ' hizo zote unazopiga ni mboyoyo

Thibitisha Mungu yupo kwa njia 8nayoweza kuhakikiwa na kuonesha yupo na ambayo haina contradi tion.

Kwa mfano. Umisema "Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, kwa sababu yeye ndiye kaumba ulimwengu huu" unatakiwa.

1. Uthibitishe ulimwengu umeumbwa na Mungu na haujatokea kwa namna nyingine yoyote.
2. Uondoe contradiction ya problem of evil inayoleta swali la, kama Mungu yupo, ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wotw, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?
 
Hujathibitisha Mungu yupo. Thibitisha Mungu yupo.

Hizo nyingine kelele tu.
Nathibitisha umeumizwa na dunia hizo zingine ni kelele tu. Pole sana.Unaweza thibitisha kwamba bacteria wapo bila microscope.
 
Nathibitisha umeumizwa na dunia hizo zingine ni kelele tu. Pole sana.Unaweza thibitisha kwamba bacteria wapo bila microscope.
Hujathibitisha Mungu yupo. Thibitisha Mungu yupo.

Hizo nyingine kelele tu.
 
Ni rahisi sana kumuelewa prof hawking kuliko kiranga,nadhani kama ningekua naongea na prof mwenyewe tungeelewana zaidi maana binafsi hua naona kiranga anafanya mambo kua magumu bila sababu.

Siyo kufanya mambo kuwa magumu bali uwezo wake wa kufikiri beyond ya pale aliposhikilia umefikia kikomo na anajiona yeye ni yard stick na standard measure ambaye watu wote tujipime kwake kiakili na kifikra.

Yupo kama chura kisimani huku akijidai kuwa hakuna bahari kubwa kuliko maji yaliyomo kisimani--, yeye anataka mambo yatii fikra zake (preconceived ideas) na siyo fikra zake zitii mambo yalivyo, kama ingalikuwa ni hivyo basi Newton asingeweza kukokotoa kanuni ya "universal gravitation" kwa sababu yeye ali formulate jinsi nguvu ya uvutano inavyofanya kazi na siyo jinsi akili yake inavyotaka nguvu hiyo ifanye kazi.

Jambo jingine, watu wanaopinga uwepo wa Mungu wapo radhi kuongopa ili kutetea madai yao ya ya kupinga uwepo wa Mungu na wala hawajali kuhusu "repercussions" za uongo wao zitakuwa vipi dhidi yao kwa sababu wamekosa akili hata kidogo ya kutambua hilo, kwa hali hiyo akili ya kutambua uwepo wa Mungu watatoa wapi?!. Wao wanaona watu wote ni mazwazwa kama wao.
 
Kweli mkuu kwenye Qur'an hakuna andiko linalosema kuwa jua huwa linazama kwenye matope,kama wewe umeliona andiko hilo liweke.
Sasa kama hamna mbona ulikua unadai kua lipo ila nimelielewa vibaya?
 
Sasa kama hamna mbona ulikua unadai kua lipo ila nimelielewa vibaya?
Napita kuangalia kama kuna mtu kathibitisha Mungu yupo tu.

Naona bado.

Mtu akiweza kuthibitisha Mungu yupo naomba nistue.
 
"'(hivi hii inaingia akilini kweli? Unajua kabisa kuwa hii nyumba nayo jenga kesho itaungua moto halafu unaweka wanao wakae humo mpaka mwakani '" Mantiki ya ujuzi wake wa yote -upendo kwa wote iko wapi hapo. ...?"

Tukijaribu kutoa mifano sie mnasema tunalinganisha Mungu na hivyo vitu ila nyie mkitoa mifano ndio sahihi,sasa wewe hapo ulikuwa unamlinganisha Mungu na nani?wakati mwengine huwa mnafurahisha tu.
Mkuu mtu anayepinga uwepo wa mungu ana haki ya kutumia mifano hii kwasababu wanatoa mapungufu yake, kitu ambacho kipo duniani. Lakini kwa wewe unayemuamini huyo mungu huwezi kumlinganisha na vitu vilivyokuwa na mapungufu kwasababu unaamini mungu ni mkamilifu na mjuzi wa kila kitu na hivyo basi kufanya hivyo ni kumshushia thamani huyo mungu wako ambaye ni nyali na mjuvi wa mambo yote..
 
Brilliant and clear explanation.

Mtu anakwambia Mungu ana nguvu zote.

Halafu anazifananisha nguvu za Mungu huyo na nguvu za serikali ya Marekani!

Kama vile serikali ya Marekani ina nguvu zote.
 
Brilliant and clear explanation.

Mtu anakwambia Mungu ana nguvu zote.

Halafu anazifananisha nguvu za Mungu huyo na nguvu za serikali ya Marekani!

Kama vile serikali ya Marekani ina nguvu zote.
Wanashangaza mkuu.. They are shooting themselves in the foot, and sadly enough they seem totally unaware of it..
 
If you haven't read Hawking, and you are interested "A Brief History of Time: From The Big Bang To Black Holes" (attached) is a good start.

We should always remind ourselves that science at a large extent deals with theories and and facts at a small extent compared to theories. Therefore science is also an ignorant field on its own as it can not explain the spiritual side of things, according to science the spiritual does not exist but to many it does. How to will explain satanism in every sphere of life, witchcraft, freemansory, miracles. Conclusively Hawking was equally an ignorant person on the other side like anybody else, right now there are other scientist who proving the existence of God in the universe.
 
What is "spiritual"?

Your diction is jumbled and hardly comprehensible.

Fix your English, or write in Swahili.
 
Watu ambao wame limit akili zao katika kufikiri mara nyingi huwa wanakurupuka kuokoteza vijihoja huko na huko wakidhani vinaweza kuwasaidia kutetea uongo wao wa kupinga uwepo wa Mungu.

Pfof, Hawkins alikuwa na udhuru (an excuse) kutokana na ugonjwa wake uliomsababishia "sonona" (depression) and I was sorry about him, kwa hiyo vyote alivyovisema au kuandika kipindi hicho lazima vichuliwe kwa tafakuri na siyo kukurupuka.

Ukiangalia maneno ya Hawkins hapo juu kabisa ambapo anasema; "------ it is impossible for God to exist in our universe ---"

👆🏻Hapo anakiri uwepo wa Mungu lakini anapinga uwepo wake katika huu ulimwengu wetu (in our universe). Hivyo ukitumia akili kidogo tu utaona anachopinga Hawkins ni uwepo wa Mungu katika hii universe yetu lakini hapingi kwamba Mungu hayupo kabisa.

Sasa mada inakuwa hivi;- "je Mungu yupo katika universe yetu au yupo mahali pengine wapi?."

Kama Hawkins angesema; "--God does not exist anywhere--" hapo ndio ingekuwa hoja ya kujadili uwepo wake.

Wanasayansi (theoretical physicists) waliokuwa Brilliant kuliko prof, Hawkins wanakiri kuwepo kwa Mungu mfano Isaac Newton , Albert Einstein, Abdus Salam, hao wawili Einstein na Salam ni Nobel winners-- Huyo salam alikuwa anaitwa WRANGLER huko University of Cambridge toka akiwa mwanafunzi hadi akiwa profesa wa mahesabu na physics, ka theorise lots of theories at the Cambridge which needs to be proved right now -- wote hao na wengineo wanakiri uwepo wa Mungu, je hamkuwaona au kusikia habari zao zinazohusu Mungu??.
 
Back
Top Bottom