Pre GE2025 Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mtulivu sana huyu mzee!anaweza pia!

Angepewa makonda ningefurahi sana nadhani angefanya ziara nchi nzima!
 
Mtu sahihi kabisa
Ni mzoefu wa siasa na strategist mzuri
Sio muumini wa fujo na vioja
 
Kuna kambi huko CCM ishanyukwa kuelekea Oct 2025
 
Uwongo mtupu, subiri jina lenyewe
 
Ni wasira.

Chuma kutoka Bunda.

Mwanamikakati wa CCM
 
Chama Cha Mapinduzi kimempendekeza Ndugu Stephen Masatu Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasilisha jina la mwanasiasa mkongwe nchini
Stephen Wassira kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM wa Taifa unaofanyika Jijini Dodoma, kwa ajili ya kupigiwa kura kuwa Makamu Mwenyemiti wa CCM Bara.

Wasira aliyezaliwa Julai Mosi, 1945 wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kwa zaidi ya nusu karne amejijengea heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.

Wasira ni miongoni mwa wana CCM waliowahi kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ni mmoja wa viongozi wakongwe wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM, ambapo tangu mwaka 2007 amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 2011.

Rekodi yake ya uongozi na uchapakazi wake, imemuweka kuwa katika nafasi nzuri ya kuonekana kama nguzo muhimu ndani ya CCM.

 
Ukome. Makamu ni Mzee Wasira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…