Stephen Wassira: Watanzania wamemuelewa na kumuunga mkono Rais Samia; wanasema kiwango chao cha furaha kimeongezeka

Stephen Wassira: Watanzania wamemuelewa na kumuunga mkono Rais Samia; wanasema kiwango chao cha furaha kimeongezeka

Mzee Wasira ambaye amekuwa waziri katika serikali tangu uhuru mpaka serikali ya awamu ya nne ya JK amesema Kiwango cha furaha kwa Watanzania kimeongezeka. Ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na Azam TV. Aidha amesema baada ya masikitiko ya muda mfupi kufuatia kifo cha Magufuli nchi imerudi kwenye reli baada ya hotuba za Rais Samia Suluhu Hassan.

Kumbe furaha hii pia imetamalaki ndani ya CCM na wapambe wanafiki wa Magufuli!

===

Akizungumza Apr 9, 2021 kwenye kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na Azam TV, Mzee Wassira amesema:

"Namwambia nini Rais? Namtakia heri. Namtakia heri aongoze nchi yetu vizuri. Na kitu kimoja ambacho ningependa Rais ajue ni kwamba: kwa hotuba hizi tu, Watanzania wengi wamemuelewa na wanamuunga mkono. Wanasema kiwango chao cha furaha kimeongezeka; kwasababu tumesikitika [kufuatia kifo cha Rais Magufuli] lakini tumerudi kwenye reli."
View attachment 1748937

Kwa Lugha nyepesi tu japo amejitahidi kuficha Hisia zake, ila tunajua kuwa Mzee Wassira kama tulivyo Watanzania ( tunaojitambua tu ) tumefurahia sana Kazi iliyofanywa Kiustadi kabisa na Israeli.
 
Aisee huyu marehemu POMBE alichukiwa mno na viongozi wenzake yaani kila mmoja amefurahi Kifo chake
Ujue viongozi wengi wevi, sasa hivi wanaji position kumalizia walichobakiza kabla ya Mwenye Uhai hajasema imetosha
 
kama unamkana magufuli kipi kinafanya umkweze nyerere???

acheno unafiki nyumba ya pazia.

lissu hawawahi kumkubali nyerere hata magufuli pia maana ni waumini wa itikadi moja.
Tofauti kubwa ya Nyerere na Magufuli ni Imani: Nyerere aliamini kuwa binadamu wote ni sawa na kila mtu anastahili heshima lakini Magufuli aliamini kuwa yeye ni zaidi ya malaika na anapaswa kusujudiwa!
 
kamsome mtu anaitwa kambona utajua hujui.
 
Kwa Lugha nyepesi tu japo amejitahidi kuficha Hisia zake, ila tunajua kuwa Mzee Wassira kama tulivyo Watanzania ( tunaojitambua tu ) tumefurahia sana Kazi iliyofanywa Kiustadi kabisa na Israeli.

israel hana rafiki.

jipendekeze kwake ukadhani anafagilia shobo.
 
This is insane kabisa, yani kila mtu aweke akili yake likizo aishi kwa akili ya raisi
Ndio maana hata wasanii hawaoni tatizo. Tumekuwa kama WAcongo. Tumekuwa taifa la Uchawa yaani.

Msifie mwenye nacho ( madaraka au pesa ) uishi.
 
Ilikuwa hakuna namna zaidi ya kumnafikia ili usishi.
Ukikosoa,,,jela, unatekwa,, unaambiwa siyo raia. Watu wakaona bora kumnafikia -maisha yaendelee.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana hata wasanii hawaoni tatizo. Tumekuwa kama WAcongo. Tumekuwa taifa la Uchawa yaani.

Msifie mwenye nacho ( madaraka au pesa ) uishi.
Chawa-ism imeathiri kila mahali yani dah! Inaskitisha kuwapa dhamana viongozi ma Chawa
 
Achana na repoti ya CAG.
Kuna repoti ya uchunguzi wa matukio ya wasiojulikana.
Kamati ya bunge ya ulinzi na usalama iliyoongozwa na Mh. Adadi Rajabu, aliyekuwa mbunge wa Muheza na mkurugenzi mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) wa zamani, ilifanya uchunguzi kuhusu matukio ya kuteka, kupotezwa na kushambuliwa wanasiasa, wanaharakati, waandishi nk.

Ripoti hiyo ilipaswa kusomwa bungeni mwaka 2019, lakini ilichomolewa katika mazingira ya kutatanisha na haijawahi kuonekana tena. Adadi Rajab naye alishughulikiwa kwa kunyimwa nafasi ya ugombea ubunge wa Muheza mwaka 2020 licha ya ushindi wa kura za maoni zaidi ya 577. Badala yake nafasi ya ugombea alipewa Hamis Mwinjuma (Mwana FA) aliyepata kura 296.

Ikiwekwa hadharani, ripoti hii ndio itamzika Dikteta Magufuli na mambo yake yote, na ushetani wake wote.
 
Back
Top Bottom