Steve Nyerere ajiuzulu nafasi ya Usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania

Steve Nyerere ajiuzulu nafasi ya Usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii wa filamu na mchekeshaji, Steve Mengele maarufu Steve Nyerere, leo Ijumaa Machi 25, 2022 ametangaza kujiuzulu nafasi ya usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania(SMT).

Asema kuna mambo mengi yenye tija ambayo Taifa linapaswa kuyashughulikia badala ya kuendeleza sakata la kuteuliwa kwake.
 
Bora, awaachie wapambane wenyewe na vyeo vyao.
 
Atakayeingia sasa ana kazi kubwa ya ku-prove uwezo na matokeo, wengi wetu tulikuwa hata hatujui cheo hicho ila kuanzia sasa tutafuatilia.
 
Siasa kwenye Muziki zimefeli,huyu nadhani alienda pale kimkakati,watafute mtu mwenye weledi afanye hiyo kazi sema hata Wasanii wenyewe hawajielewi hawalipi uzito kabisa hilo shirikisho.

Hongera Steve kwa kusoma alama za nyakati ingawa umechukua uamuzi ukiwa umechelewa baada ya kung'ang'ania.
 
sanii wa filamu na mchekeshaji, Steve Mengele maarufu Steve Nyerere, leo Ijumaa Machi 25, 2022 ametangaza kujiuzulu nafasi ya usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania(SMT).

Asema kuna mambo mengi yenye tija ambayo Taifa linapaswa kuyashughulikia badala ya kuendeleza sakata la kuteuliwa kwake.
Katema ndoano. Safi sana...
 
Baada ya kupigwa stop na Basata kutekeleza majukumu yake hadi hapo aavyojulishwa, Leo hii Steve Nyerere kaamua yeye mwenyewe
ametangaza kujiuzulu nafasi ya Usemaji wa Shirikisho la Muziki, akisema kuna mambo mengi yenye tija ambayo Taifa inapaswa kuyashughulikia badala ya kuendeleza sakata la kuteuliwa kwake.

Steve amesema ataendelea kuwepo kwenye maisha ya Wasanii kwani bado ana nafasi za uongozi sehemu mbalimbali na ataendelea kuendesha matamasha yanayowahusu Wasanii.



1648200052326.png
 
Hatimaye Steve Nyerere a.k.a Steve Akeee ameamua kuachia ngazi usemaji wa shirikisho la mziki Tanzania...

Akiwa kwenye ofsi za BASATA jijini Dar es salaam , Steve Nyerere amedai nchi hii ina mambo mengi ya kufanya kuliko kuanza kuvutana kwenye nafasi ya usemaji ambayo haina hata mshahara ....

Ili kutoa nafasi Kwa mambo mengine ya msingi , ameamua kujiudhuru nafasi hiyo....

Hvi karbuni Steve Nyerere aliteuliwa na uongozi wa shirikisho la mziki Tanzania kushika nafasi ya usemaji wa shirikisho hilo , na uteuzi huo uliibua sintofahamu miongoni mwa wadau wa mziki hasa bongo fleva, na kuleta mgawanyiko mkubwa wa kimawazo kuhusu uhalali wa Steve kushika nafasi hiyo.

Untitled-1_50.jpg
 
Tivu akeeee..abaki tu kua kwenye ile kamati yake ya sikuzote
 
Bora kakubali maana wasanii wenzake walimkaa kooni mpaka akaona kiama
 
Back
Top Bottom