Steve ameweka wazi CV ya FA hana kosa.Leo katika press conference yake Steve Nyerere ambaye ni kada wa CCM alijadili Mambo mawili ya msingi na kudhibitisha kwamba Tume huru ya ya uchaguzi haipingiki.
1. Kwanza kahoji Kama mbunge wa Muheza kupitia chama Cha CCM Mh Mwinjuma alishinda kihalali.
Hili ni muhimu, Ina maana Kuna Wana CCM wanashuku Wana ccm wenzao kutoshinda kwa haki.
2. Pili, Kahoji kuhusu wabunge wa memo. Yani Kuna kiongozi alikiwa anatoa memo ya Nani awe mbunge na Nani asiwe mbunge.
Kwa hivyo wananchi hawana sauti ya mwisho Bali Memo kutoka kwa mkuu wa nchi.
Nadhani kutokana na wanaccm wenyewe kuonesha kutokubaliana na mfumo wa uchaguzi ni muda sasa tuanze mchakato wa Tume huru.