Nakumbuka miaka ya mwishoni 1990’s wimbi la wizi wa majumbani lilikuwa limeshamiri sana Arusha, kipindi kile walikuwa wanatembea kundi la wezi Kati ya 40-50. Sasa wakawa wamevamia nyumba za jirani sisi tukawa tumeamka dingi hakuwepo alikuwa safari, kijana mkubwa aliyekuwepo alikuwa ni baba mdogo (RIP) kipindi hicho alikuwa Anasoma kidato cha sita. sasa katika kutaharuki akawa anawasha na kuzima taa za nje kama kuwaonesha kuwa tuko macho. Hatimaye wezi walitufikia wakawa nje wanasema Tina ametuambia Deo yuko ndani kwa hiyo tufungue wamchukue Deo, walikuwa wanamaanisha antena imetuonesha ndani kuna Video (Television). Kipindi kile mama (RIP) alikuwa mgonjwa mno wa kubeba są zile purukushani tulimbeba na kumleta sebuleni, tulikuwa wengi sababu ilkuwa wakati wa likizo ya mwezi July watoto wote sita tulikuwepo na watoto wa ndugu waliokuwa wnasoma mikoa ya jirani walikuwepo tulkuwa ka 13-15 hivi wote watoto watoto. Mama akatuambia tufungue mlango sababu watavunja tu wataingia…. Mlango ulifunguliwa wakaingia bhana jamaa wa kwanza akauliza nani alikuwa anawasha taa na kuzima?? Atueleze alikuwa anawasha indicator nyumba inakata kona kuelekea wapi?? Wote tulijikuta tumecheka tukawaonesha asee alichezea kichapo, wakabeba tv, radio na wakaingia kwa chumbani kwa wazazi wakabeba mabriefcase ya mzee sijui walifkiri kuna hela…….. wakatuambia hawajatupiga wala kutukata mapanga sbb Baba yenu ni mtu mwema amenunua jezi na mipira 2 ya timu ya mtaani. Ila wamempiga Baba yetu mdg sbb ya kiherehere chake.
Mwisho wa siku tuliwahisi sababu baadhi ya sauti tulizijua na kitendo cha kujua yule ni baba yetu mdogo tulihisi sio watu wa mbali, baada ya kuondoka mama alitukataza tusiseme popote kuwa tumewajua au tumewahisi tukae kimya.
Iła mwisho wa siku life liliendelea wale tuliowahisi wengine walifariki,kufungwa nk ila yule aliekuwa anaongea bado yuko ila kachoka mno na limguu lake limevimba anatia huruma mno! Mwaka jana nlienda likizo nkakutana nae anaomba nimtoe lock nilimnunulia Kvant ndogo ila nilimchana ukweli lile dukuduku langu la miaka mingi nkalitoa