Story ya kijana mmoja mwenye ndoto kubwa

Story ya kijana mmoja mwenye ndoto kubwa

Katabaro_EJ

Member
Joined
Jul 6, 2013
Posts
15
Reaction score
11
Kijana mmoja jina () alihitimu elimu ya chuo kikuu katika chuo kikuu kimoja mkoani Morogoro.

Baada ya kuhitimu alikuwa na viji-savings vyake akavitumia kununua kiwanja na shamba hapo hapo mkoani Morogoro.

Badae akakodi meza katika soko la Manzese (lililokuwa soko kuu la muda kupisha ujenzi wa soko kuu la mkoa wa Morogoro "Kingalu" kama linavojulikana kwa sasa).

Akaanza kuuza vitunguu maji, viazi na mafuta ya kupima (mafuta ya alizeti mabichi na korie).

Kwa mwanzo biashara ya vitunguu ilikuwa juu sana kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa kuuza vipeto viwili vya vitunguu ndani ya siku nne na anahesabu faida ya shilingi elfu themanini. kipeto ni nusu gunia la vitunguu ama viazi. Biashara ikaenda vizuri kila akipata faida anaongeza mzigo. Akaachana na kuuza viazi mbatata. Akabakia na vitunguu pamoja na mafuta.

Kimbembe kikaja, ameweka mzigo wa laki tano wa vitunguu vikashuka bei! Badala ya kuuza kilo kwa shilingi 2500/- mpaka 3000/- ikaja 700/- mpaka 900/-. Hapa biashara ikamuwia chungu. Kila meza ina vitunguu na bei iko chini yeye kanunua ikiwa juu. Wiki hajauza hata 10,000/-.

Mtaji ukashuka kutoka Tshs 500,000/- mpaka Tshs 90,000/- kumbuka hapo inabidi ale na alipe kodi. Basi biashara ikawa imefeli.

Baada ya biashara ya vitunguu kufeli akaamua kutafuta kibanda cha mabati ya kuchomelea!

Akatafuta site ya kukiweka ili aanzishe duka genge. Akafanikiwa kupata eneo katika viwanja vya CCM kata ya Uwanja wa Taifa manispaa ya Morogoro. Katibu wa CCM kata ile kwa kipindi kile wakamletea figisu ikabidi akiondoe atafute mahali pengine. Akapata na akaanza maisha ya biashara upya!

Akafanikiwa kwa kiasi kikubwa akaweza hata kujenga chumba cha kuanzia maisha! Akaweka na huduma za miamala ya simu kama MPESA na TigoPesa. Kutokana na yeye kuhamia mbali na mji akamuweka mtu wa kuwa anauza pale na kumuachia chumba alichokuwa anaishi kwa kuwa kodi ilikuwa haijaisha! Kutokana na usimamizi kuwa mdogo hiyo biashara ikawa imeyumba tena.

Mwisho wa siku akaamua kuuza kile kibanda na kupanga frame kisha akahamia kwenye biashara ya vifaa vya ujenzi! Hii biashara aliianza kwa mtaji mdogo na ikawa inakua. Nayo akawa anabeba changamoto zake lakini zikamuwia ngumu kuzibeba mara TRA, mara watu wa Manispaa, mara kodi ya frame sijui luku! Faida anabaki nayo ndogo ili mradi apate hata mlo wa mchana.

Hitimisho. Usione mtu anafanya kazi hata ndogo chini ya status yake ukamuona amekuwa hopeless! Wengine wana ndoto kubwa lakini ili wazitimize inawabidi kuvuka baadi ya vikwazo! Vikwazo njiani ni vingi. Wengi wanaamua kudhalilika ili wapate kula!
 
Mwambie aendelee kupambana Mkuu.
Ukiangalia watu watakuonaje na degree yako unakufa njaa unajiona.
Fanya chochote unachoona kitakusaidia hata watu wakuonaje Mana mwisho wa siku hawana msaada na hata wakikusaidia inafika mahali wanakuchoka afadhali wakuone unajipambania wanajua hata ukipewa msaada utautumia vizuri.
Mimi nishazoea nnachofanya na nashukuru Mungu kinanisaidia na kimenivusha.
 
hapa ndio maama na kazi yangu hii huwa naamua kuridhika.

fikiria mtu kapanga vitunguu atoboe wewe naye unakenda kuweka vitunguu uuze kama yeye wakati una uhakika wa kuishi.tuhurumiane jamani.
 
Keep up the sprit ze muse...(..) one day utafika malengo yako na ndoto zitatimia.
 
Back
Top Bottom