SUA badilikeni, achaneni na Panya imetosha

SUA badilikeni, achaneni na Panya imetosha

SUA ni chuo cha kilimo tafiti unazo taka wafanye azifundishi hapo chenyewe kime bezi sana na mambo ya kilimo tu mfano ni hao panya
 
Mleta mada kaandika maneno mengi lakini anachokisa ni uelewa wa hii dunia inaelekea wapi. Anadhani China wameanka asubuhi tu wakarusha chombo kwenda Mars. Nchi bado kuna familia hazina maji safi na salama, miundombinu ya uhakika, nishati na elimu bado vinasumbua jamii zetu unaongelea kurusha chombo Mars kama mfano?

Wewe umefanya utafiti gani au umechangia nini kwenye tafiti na ukachangia maarifa ya kutatua tatizo gani?

Unachojua ni kuandika tu bila uelewa wowote. Tuanze na wewe umewahi fanya utafiti upi?
 
Hii ndio ile nchi ya ahadi ambayo raisi alikufa na hakuweza kuiona nchi aliyoibomoa miaka 6 iliyopita
 
Mtoa uzi usikalili maisha,huo utafiti kuhusu panya ni ka sehemu kadogo Sana kati ya tafiti nyingi zilizofanywa/zinazofanywa na SUA.
Mtoa hoja ana hoja. Course ya Education SUA ya nini? Kijishughulishe na lengo la kuanzishwa kwake. Usipindishe hoja nyie Ma-Profesa wetu wa nadharia wakati masuala ya nchi Mhe.Msukuma, Lusinde na wengineo wanapambana nayo.TAFAKARI HOJA KWANZA ACHA NA HAO PANYA WENU[emoji38][emoji38]
 
nakukumbusha kwa sasa lile jina "chuo cha kilimo " ni jina tu ila yaliyo ndani sio kilimo,na kuthibitisha hili tafuta mtu yuko SUA muulize kwanini kuna ualimu,na baadhi ya kozi zisizoeleweka pale kama shahada ya utalii ndio utajua uhalisia nadhani wanataka kuongeza na shahada ya rasilimali watu ambayo wanajua kabisa kuna vyuo vingi vinatoa hadi sasa na ajira hazipo;
hivyo kama mnavyomkosoa mleta mada kuwa hajui alichosema,naona baadhi yenu mmeanza kuchangia msivyovijua pia;
katika uhalisia SUA ni kati ya vyuo ambavyo vina kozi nyingi zisizo na ajira nchi hii,na hakijafanya hata lile lengo lake la kuzalisha wataalamu wa kilimo nchi hii;
Wanabisha bure lakini ukweli ndio huo. Mi-course ya ajabu ajabu mingi wakati vyuo vingine vinafundisha hizo courses.
 
Kweli mzee ata mimi binafsi nimechoka na hili la panya kwanza naona ni udwanzi tuu.
 
Na Thadei Ole Mushi.

SUA wamekuja na panya wa Kupima Corona... Mimi nshaanza kuchoka na hawa panya wa SUA.

Sayansi hii ya kufundisha wanyama kunusa (Sniffing) kwa wenzetu ilianza muda mrefu sana. Ni mojawapo ya Technolojia ya kizamani kabisa. Huko Cuba Panya wameanza kutumika toka 1954 kunusa maeneo yenye madini, mobomu nk. Kwa sasa haitumiki Sana kwa kuwa njia za kisasa zaidi zimeendelea kugundilika kila kukicha.

Ni wakati sasa wa kuwaambia SUA badala ya kutrain Panya zaidi ambao hatuwatumii popote wajikite kwenye kugundua mabomu ambayo tutayauza au wajikite kwenye kufanya tafiti tunawezaje kutumia uranium iliyopo kule Dodoma kuzalisha nguvu za Nyuklia. Au wajikite kutengeneza Chanjo ya Corona ambayo tutaiuza.

Waliwahi kuja na panya wa kutambua TB lakini hakuna Hospital hata Moja inayotumia Panya kunusa makohozi. Bado njia za kisasa za kupima TB ndizo zinazoendelea Kutumika mahospitalini.

Hata hii ya kutegua Mabomu kwa kunusa ni ya zamani Sana. Majeshi ya wenzetu hawatumii Tena sniffing technology Sana nadhani tunapaswa kuanza kufikiria kubadilika.

Sio kwamba wenzetu hawawezi ku train Panya kufanya sniffing. Wanaweza Sana Ila ni technolojia ya Zamani mno watu walishahama huko wanaitumia technolojia hii mara Chache Sana.

Yaani Maabara za Dunia zipo busy kutengeneza Chanjo na Makampuni yanashindana kwenye kutengeneza Chanjo sisi tunamuwaza panya tu atusaidie kunusa watu wenye Corona.

Tuwekeze kwenye tafiti zitakazoleta faida na uvumbuzi wenye tija kwa Taifa na Dunia. Naona SUA wao kila kitu ni kuwaza Panya wao tu. Tumekuwa kama tumesimama mahali pamoja wenzetu wanakwenda mars na kurudi sisi tunalisha Panya Pumba tu hapo SUA. Na wameona hakuna Cha maana wanachofanya wameamua kuanzishwa course za Education. Jamani nafikiri hivi vyuo kila kimoja ki-save purpose yake.

Je kitu Wanachokiweza SUA ni Kutumia panya Kunusa Tu? Vyuo vikuu vingine wao kwani wanasemaje? Muhimbili pale kile kijumba Cha kujifukiza bado kipo?

Tunakwama wapi? Leo Tarehe 15/5/2021 asubuhi hii China imefanikiwa kurusha kifaa kwenda Sayari ya Mars na kimetua vizuri na kitakaa huko Miezi 3 kutafiti kama Kuna uwezekano wa maisha kwenye Sayari hiyo. Huko Sua Profesa anaamka na Box la Panya anaenda kuwachungulia na anatokea hadharani anasema amevumbua kitu.

Tubadilike... Dunia inakimbia sisi tumekaa kabisa na tumeanza kulala.

Ole Mushi.
0712702602

View attachment 1785585
Mbawa pavlov na njiwa wa skinne!!!
We jamaa umenikumbusha hao watu.
 
Kwa taarifa yako:
1. Sua wanafanya tafiti nyingi sana, hiyo ya panya ni ndogo tu.
2. Hujui sua wametengeneza chanjo za magonjwa mengi ya wanyama ikiwemo kuku? Wiraza zenu izinaendelea kuabudu chanjo kutoka nje. Sio kosa la sua
3. Vipi vipaumbele vya taifa kuhusu maendeleo? Je wametenga bajeti kiasi gani na sua wakashindwa kuomba na kutekeleza? Umeelewa?
4. Training kubwa ya MSC na PhD sehemu kubwa tumeachia wafadhili, wakija na ajenda za panya wasiombe fund?
Yako mengi nadhani mleta mada anaufinyu mkubwa wa uelewa kuhusu hali za vyuo vyetu. Afanye tafiti kabla ya kukurupuka kuandika
Naishia hapo
Hizo tafiti zenu zimeinua wakulima? Mnashindwa na wakenya, mbegu na kemikali zimejaa mdukani kutoka kenya, hamuoni aibu?
Kubalini kukosolewa, ili mbadirike nyie ni kujitetea tu.
 
How comes SUA wafanye tafiti za nishati za uranium wakati ni chuo cha Kilimo na mifugo kwa specialization. Wenzako wanatumia panya sababu mifugo ndio sehemu ya specialization yao hivyo watatumia resources, knowledge walizonazo katika kufanya tafiti.

Mfano kuna tafiti za madawa ya kilimo mengi ambayo SUA wamefanya na kugundua dawa ambazo zinatumika kwa wingi kwa wakulima, Pia kuna mbegu za mazao pamoja na wanyama ambao SUA wamegundua na kuwauzia wakulima ila serkali yako ndo imeshindwa kupigia promo na kutoa motisha kwa wazalishaji wa ndani hivyo acha kulahumu.
Sua wanafundisha physics watashindwaje kufanya tafiti za uranium ?
 
Na Thadei Ole Mushi.

SUA wamekuja na panya wa Kupima Corona... Mimi nshaanza kuchoka na hawa panya wa SUA.

Sayansi hii ya kufundisha wanyama kunusa (Sniffing) kwa wenzetu ilianza muda mrefu sana. Ni mojawapo ya Technolojia ya kizamani kabisa. Huko Cuba Panya wameanza kutumika toka 1954 kunusa maeneo yenye madini, mobomu nk. Kwa sasa haitumiki Sana kwa kuwa njia za kisasa zaidi zimeendelea kugundilika kila kukicha.

Ni wakati sasa wa kuwaambia SUA badala ya kutrain Panya zaidi ambao hatuwatumii popote wajikite kwenye kugundua mabomu ambayo tutayauza au wajikite kwenye kufanya tafiti tunawezaje kutumia uranium iliyopo kule Dodoma kuzalisha nguvu za Nyuklia. Au wajikite kutengeneza Chanjo ya Corona ambayo tutaiuza.

Waliwahi kuja na panya wa kutambua TB lakini hakuna Hospital hata Moja inayotumia Panya kunusa makohozi. Bado njia za kisasa za kupima TB ndizo zinazoendelea Kutumika mahospitalini.

Hata hii ya kutegua Mabomu kwa kunusa ni ya zamani Sana. Majeshi ya wenzetu hawatumii Tena sniffing technology Sana nadhani tunapaswa kuanza kufikiria kubadilika.

Sio kwamba wenzetu hawawezi ku train Panya kufanya sniffing. Wanaweza Sana Ila ni technolojia ya Zamani mno watu walishahama huko wanaitumia technolojia hii mara Chache Sana.

Yaani Maabara za Dunia zipo busy kutengeneza Chanjo na Makampuni yanashindana kwenye kutengeneza Chanjo sisi tunamuwaza panya tu atusaidie kunusa watu wenye Corona.

Tuwekeze kwenye tafiti zitakazoleta faida na uvumbuzi wenye tija kwa Taifa na Dunia. Naona SUA wao kila kitu ni kuwaza Panya wao tu. Tumekuwa kama tumesimama mahali pamoja wenzetu wanakwenda mars na kurudi sisi tunalisha Panya Pumba tu hapo SUA. Na wameona hakuna Cha maana wanachofanya wameamua kuanzishwa course za Education. Jamani nafikiri hivi vyuo kila kimoja ki-save purpose yake.

Je kitu Wanachokiweza SUA ni Kutumia panya Kunusa Tu? Vyuo vikuu vingine wao kwani wanasemaje? Muhimbili pale kile kijumba Cha kujifukiza bado kipo?

Tunakwama wapi? Leo Tarehe 15/5/2021 asubuhi hii China imefanikiwa kurusha kifaa kwenda Sayari ya Mars na kimetua vizuri na kitakaa huko Miezi 3 kutafiti kama Kuna uwezekano wa maisha kwenye Sayari hiyo. Huko Sua Profesa anaamka na Box la Panya anaenda kuwachungulia na anatokea hadharani anasema amevumbua kitu.

Tubadilike... Dunia inakimbia sisi tumekaa kabisa na tumeanza kulala.

Ole Mushi.
0712702602

View attachment 1785585
Mkuu Thadei!

Katika ulimwengu wa Sayansi ni kawaida kwa vyuo fulani kujikita kwenye utafiti wa vitu au kitu fulani. Kwa hili la SUA kupambana na tafiti za panya kila siku nawapa heko.

Hata mimi sipendi tafiti za panya, lakini nadhani zimewapa sifa kubwa duniani. Nadhani jambo muhimu ni kuzifanya hizo tafiti zinapotoa matokeo mazuri basi tuweze zitumia katika maisha yetu ya kawaida na hasa Tanzania.
 
Nimetumia chanjo yao mwaka jana ya magonjwa manne kwenye chanjo moja kwenye mifugo yangu
Kiukweli mpaka sasa mifugo hawajaugua
Jamaa wapo fit
Kumbe uwezo wa kutengeneza chanjo tunao
 
Kwakutumia panya kasi ya upimaji corona itakuwa kwa kasi ya 1G.
Tafiti zao jamaa karibu zote hazijawahi kuleta positive impacts katika dunia hii licha ya kuwa na na documentation mengi sana maabara.
Mambo ya kisengerema sana
 
Hakijui hiki chuo!
Nafikiri ndiyo chuo kinachoheshimika zaidi Tanzania hata huko ulimwenguni kwa tafiti.
Wana maabara kubwa ya tafiti za mbegu na wanajenga maabara kubwa na BORA zaidi Africa.
SUA ukisikie tu mitaani ila ni chuo chenye tafiti nyingi zaidi ya panya.

Everyday is Saturday.............................. 😎
Mbona. Kilimo hohe hahe , hizo tafiti zao zinatatua nini ?
Mpaka sasa hakuna mbegu bora za kutosha ,magonjwa mengi tu ya mimea.
Mpaja sasa wakolima wansumia na mipini, hawzna nyenzo.
Sie wengine tunalima na tunakutana na changamoto za ajabu.
Mfano SUA mpaka sasa wameshindwa kugundua njia za kudhibiti barafu mikoa ta nyanda za juu wakulima wanalia kika mwaka mazao yao kukaushwa na barafu.
Wameshindwa kugundua dawa ya homa ya nguruwe.
Wameshindwa kugundua dawa ya mdudu kantangaze wa kwenye nyanya.
Mnyauko kwenye viazi na nyanya .
Ukimwi wa mihoma.
Mnyauko wa mihogo.
Kuna siku nimetafuta mtandaoni tafiti ya chikichi iliofanywa na SUA , hakun,zipi za Wa Asia tu.
Yaani matatizo ni mengi sana.
Watafiti wa SUA wajiuzuru kama mainjinia ya wa maji, wameshindwa kazi.
Kuna mhitimu wa SUA nilimuuliza, hivi zao la kakao linastawi Kigoma, alibaki kuweweseka tu.
 
Back
Top Bottom