Nimefanya research kidogo nikajikuta naumia zaidi kwa mambo mawili...
1. Jinsi tunavyodharau huu utafiti, na
2. Jinsi huko duniani utafiti huu ulivyokuwa ume-make headlines mwaka jana lakini bila kutajwa chuo husika!!!
(i) The New York Times-
Rat That Sniffs Out Land Mines Receives Award for Bravery.
Wakati Thadei na wenzake mnaona hao ni panya wanaotakiwa kuwekwa makumbusho kwa sababu ni useless na huko ughaibuni wametumika sana na hivi sasa hawana maana yoyote, The New York Times wanasem:-
Kwenye habari hiyo ya NYT, hata Tanzania haikutajwa, na labda unaweza kudhani anazungumziwa panya mwingine kabisa!!!
(ii) USToday:-
Meet Magawa, the 'hero rat' awarded a bravery medal for detecting dozens of landmines.
US Today na wenyewe wameshindwa kuitaja hata Tanzania let alone SUA lakini wanafungua habari yao kwa kusema:-
(iii) The Guardian ( UK):-
Magawa the landmine detection rat given gold medal for bravery.
Kama kwa hizo media, The Guardian nao hawaitaji SUA wala Tanzania lakini wanaukubali uwezo wa huyo panya ambao unazidi ule wa binadamu kwenye kutegua mabomu ambapo wanasema:-
(iv) NBC News:-
Rat called Magawa awarded prestigious gold medal for Cambodia landmine. detection
Kama hao wengine, NBC News inaonekana hawana ufahamu wowote kuhusu TZ na SUA kwenye uwepo wa hao panya, na matokeo yake wanaishia tu kusema:-
(v) (i) BBC -
Magawa the mine-detecting rat wins PDSA Gold Medal.
Bora hata BBC ambao angalau waliitaja Tanzania ingawaje sio kwa kuipa credit kwamba:-
Hiyo ni sehemu ndogo sana ya headlines za Panya ambao Wabongo tunataka wawekwe makumbusho kwa sababu ni "useless"!!
Sasa ikiwa sisi wenyewe tu tuna fikra kama hizi, hivi kuna mtu anaweza kuzishangaa hizo media za nchi za magharibi kutosema chochote kuhusu Tanzania, na hususani SUA ambao ni partner wakubwa wa huo mradi?
Media zote zinatoa credit kwa taasisi ya Kibelgiji inayoitwa Apopo yenye ofisi zake hapo SUA!! Ajabu, hata ukiingia kwenye website ya Apopo, huwezi kuuona ushiriki wa SUA kwa haraka! Binafsi, ilinibidi nitumie keyword tofauti ndipo nikakutana na sehemu ya hii habari:-
Ukweli ni kwamba, serikali zetu pays little attention kwenye kazi zinazofanywa na wazawa, no wonder watu kama Ngunichile wanahoji:-
Lakini ukiacha kutumia source za SUA wenyewe ambao nilichelea wasije wakawa wanajimegea, nikalazimia kutafuta credible external source ambayo inasema:-
Hayo ni maelezo kutoka tovuti ya University of California, Davis, na ukiingia website ya SUA wenyewe,
hapa utakuta mlolongo wa research projects!