SUA badilikeni, achaneni na Panya imetosha

SUA ni chuo cha kilimo tafiti unazo taka wafanye azifundishi hapo chenyewe kime bezi sana na mambo ya kilimo tu mfano ni hao panya
 
Mleta mada kaandika maneno mengi lakini anachokisa ni uelewa wa hii dunia inaelekea wapi. Anadhani China wameanka asubuhi tu wakarusha chombo kwenda Mars. Nchi bado kuna familia hazina maji safi na salama, miundombinu ya uhakika, nishati na elimu bado vinasumbua jamii zetu unaongelea kurusha chombo Mars kama mfano?

Wewe umefanya utafiti gani au umechangia nini kwenye tafiti na ukachangia maarifa ya kutatua tatizo gani?

Unachojua ni kuandika tu bila uelewa wowote. Tuanze na wewe umewahi fanya utafiti upi?
 
Hii ndio ile nchi ya ahadi ambayo raisi alikufa na hakuweza kuiona nchi aliyoibomoa miaka 6 iliyopita
 
Mtoa uzi usikalili maisha,huo utafiti kuhusu panya ni ka sehemu kadogo Sana kati ya tafiti nyingi zilizofanywa/zinazofanywa na SUA.
Mtoa hoja ana hoja. Course ya Education SUA ya nini? Kijishughulishe na lengo la kuanzishwa kwake. Usipindishe hoja nyie Ma-Profesa wetu wa nadharia wakati masuala ya nchi Mhe.Msukuma, Lusinde na wengineo wanapambana nayo.TAFAKARI HOJA KWANZA ACHA NA HAO PANYA WENU[emoji38][emoji38]
 
Wanabisha bure lakini ukweli ndio huo. Mi-course ya ajabu ajabu mingi wakati vyuo vingine vinafundisha hizo courses.
 
Kweli mzee ata mimi binafsi nimechoka na hili la panya kwanza naona ni udwanzi tuu.
 
Mbawa pavlov na njiwa wa skinne!!!
We jamaa umenikumbusha hao watu.
 
Hizo tafiti zenu zimeinua wakulima? Mnashindwa na wakenya, mbegu na kemikali zimejaa mdukani kutoka kenya, hamuoni aibu?
Kubalini kukosolewa, ili mbadirike nyie ni kujitetea tu.
 
Sua wanafundisha physics watashindwaje kufanya tafiti za uranium ?
 
Mkuu Thadei!

Katika ulimwengu wa Sayansi ni kawaida kwa vyuo fulani kujikita kwenye utafiti wa vitu au kitu fulani. Kwa hili la SUA kupambana na tafiti za panya kila siku nawapa heko.

Hata mimi sipendi tafiti za panya, lakini nadhani zimewapa sifa kubwa duniani. Nadhani jambo muhimu ni kuzifanya hizo tafiti zinapotoa matokeo mazuri basi tuweze zitumia katika maisha yetu ya kawaida na hasa Tanzania.
 
Nimetumia chanjo yao mwaka jana ya magonjwa manne kwenye chanjo moja kwenye mifugo yangu
Kiukweli mpaka sasa mifugo hawajaugua
Jamaa wapo fit
Kumbe uwezo wa kutengeneza chanjo tunao
 
Kwakutumia panya kasi ya upimaji corona itakuwa kwa kasi ya 1G.
Tafiti zao jamaa karibu zote hazijawahi kuleta positive impacts katika dunia hii licha ya kuwa na na documentation mengi sana maabara.
Mambo ya kisengerema sana
 
Mbona. Kilimo hohe hahe , hizo tafiti zao zinatatua nini ?
Mpaka sasa hakuna mbegu bora za kutosha ,magonjwa mengi tu ya mimea.
Mpaja sasa wakolima wansumia na mipini, hawzna nyenzo.
Sie wengine tunalima na tunakutana na changamoto za ajabu.
Mfano SUA mpaka sasa wameshindwa kugundua njia za kudhibiti barafu mikoa ta nyanda za juu wakulima wanalia kika mwaka mazao yao kukaushwa na barafu.
Wameshindwa kugundua dawa ya homa ya nguruwe.
Wameshindwa kugundua dawa ya mdudu kantangaze wa kwenye nyanya.
Mnyauko kwenye viazi na nyanya .
Ukimwi wa mihoma.
Mnyauko wa mihogo.
Kuna siku nimetafuta mtandaoni tafiti ya chikichi iliofanywa na SUA , hakun,zipi za Wa Asia tu.
Yaani matatizo ni mengi sana.
Watafiti wa SUA wajiuzuru kama mainjinia ya wa maji, wameshindwa kazi.
Kuna mhitimu wa SUA nilimuuliza, hivi zao la kakao linastawi Kigoma, alibaki kuweweseka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…