SUA badilikeni, achaneni na Panya imetosha

Kwani ni lazima SUA wafanye kila kitu? SUA wao wapo na panya, hivyo vingine fanya wewe...

Ani
Katika vyuo vinavyojitahidi kubuni na kuvumbua, SUA inajitahidi sana.
Mleta mada angepeleleza kwanza kabla ya kuja na hizi shutuma.

Sua wameweza hata kubuni mashine (kama tractor ndogo) ya kurahisisha shughuli za mkulima.
 
Ni kweli kabisa, lakini je watakuelewa, maana binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Bwana mkubwa ungelikuwa unajua sababu ya hizo kozi kuongezwa usingeandika ulichoandika,nakupa pole kwasababu Jambo usilolijua ni km usiku wa Giza,kwa upeo wako unaona kuwa anayeongeza kozi hizo ni SUA kumbe kiuhalisia sio hivyo,ngoma imeanzia juu kwa Wanasiasa wanaotoa amri kuwa hebu ongezeni kozi ili kuwa na wanafunzi wengi,Nchi hii wanaoiharibu ni Wanasiasa wataalamu wanabebeshwa msalaba usio wa kwao.
 
Ni mwaka jana tu wametengeneza chanjo ya kuku inayokinga magonjwa matatu kwa mpigo. Ni ukombozi mkubwa kwa wafugaji wadogo.
Naam,SUA iko vizuri,sema nchi yetu haisapoti ipasavyo Tafiti za Kisayansi.
 
Karibu SUA ujifunze.Usisubiri maneno ya kuambiwa.
 
Hizo tafiti zenu zimeinua wakulima? Mnashindwa na wakenya, mbegu na kemikali zimejaa mdukani kutoka kenya, hamuoni aibu?
Kubalini kukosolewa, ili mbadirike nyie ni kujitetea tu.
Kweli Mkuu ukienda mdukani madawa na mbegu nyingi sio kutoka nje ya nchi.

Elimu ya TZ ni utopolo sana basi tu.

Elimu ya Tz ni elimu ya uchuuzi na sio elimu ya kutengeza bidhaa
 
Nakuunga mkono, labda ibaki kama maonyesho lakini si kuhesabu kuwa ni mafanikio.
SUA hawataona huu ni ushauri,ni kweli kwa dunia ya leo kufanya utafiti wa panya sijui atambue nini,ni uzembe wa kiwango cha lami;
ningesikia wana-design sensors kwa ajili ya utambuzi wa magonjwa mbalimbali sawa,ila panya hapana;
Nimefanya research kidogo nikajikuta naumia zaidi kwa mambo mawili...

1. Jinsi tunavyodharau huu utafiti, na
2. Jinsi huko duniani utafiti huu ulivyokuwa ume-make headlines mwaka jana lakini bila kutajwa chuo husika!!!

(i) The New York Times- Rat That Sniffs Out Land Mines Receives Award for Bravery.

Wakati Thadei na wenzake mnaona hao ni panya wanaotakiwa kuwekwa makumbusho kwa sababu ni useless na huko ughaibuni wametumika sana na hivi sasa hawana maana yoyote, The New York Times wanasem:-
Kwenye habari hiyo ya NYT, hata Tanzania haikutajwa, na labda unaweza kudhani anazungumziwa panya mwingine kabisa!!!

(ii) USToday:- Meet Magawa, the 'hero rat' awarded a bravery medal for detecting dozens of landmines.
US Today na wenyewe wameshindwa kuitaja hata Tanzania let alone SUA lakini wanafungua habari yao kwa kusema:-
A rat is being honored with one of the highest awards in the animal world after he has potentially saved numerous lives for clearing landmines from fields in Cambodia.
(iii) The Guardian ( UK):- Magawa the landmine detection rat given gold medal for bravery.
Kama kwa hizo media, The Guardian nao hawaitaji SUA wala Tanzania lakini wanaukubali uwezo wa huyo panya ambao unazidi ule wa binadamu kwenye kutegua mabomu ambapo wanasema:-
Magawa, who is now nearing retirement age, can search the area of a tennis court in 30 minutes, something that would take a human with a metal detector up to four days.

(iv) NBC News:- Rat called Magawa awarded prestigious gold medal for Cambodia landmine. detection

Kama hao wengine, NBC News inaonekana hawana ufahamu wowote kuhusu TZ na SUA kwenye uwepo wa hao panya, na matokeo yake wanaishia tu kusema:-
Wet-nosed Magawa was formally presented with his miniature medal in a virtual ceremony from London on Friday, becoming the first rat in the PDSA's 77-year history to receive the honor. Former winners include police dogs, horses, pigeons and a cat.

(v) (i) BBC - Magawa the mine-detecting rat wins PDSA Gold Medal.

Bora hata BBC ambao angalau waliitaja Tanzania ingawaje sio kwa kuipa credit kwamba:-

Hiyo ni sehemu ndogo sana ya headlines za Panya ambao Wabongo tunataka wawekwe makumbusho kwa sababu ni "useless"!!

Sasa ikiwa sisi wenyewe tu tuna fikra kama hizi, hivi kuna mtu anaweza kuzishangaa hizo media za nchi za magharibi kutosema chochote kuhusu Tanzania, na hususani SUA ambao ni partner wakubwa wa huo mradi?

Media zote zinatoa credit kwa taasisi ya Kibelgiji inayoitwa Apopo yenye ofisi zake hapo SUA!! Ajabu, hata ukiingia kwenye website ya Apopo, huwezi kuuona ushiriki wa SUA kwa haraka! Binafsi, ilinibidi nitumie keyword tofauti ndipo nikakutana na sehemu ya hii habari:-
APOPO’s innovation in landmine and tuberculosis detection using African giant pouched rats is recognized worldwide as a successful and ground-breaking collaboration with Sokoine University of Agriculture (SUA) in Morogoro.

Ukweli ni kwamba, serikali zetu pays little attention kwenye kazi zinazofanywa na wazawa, no wonder watu kama Ngunichile wanahoji:-
Kama zipo tafiti nyingine mbona hazisikikii ?? Mimi uwa nasikia panya, panya tu
Lakini ukiacha kutumia source za SUA wenyewe ambao nilichelea wasije wakawa wanajimegea, nikalazimia kutafuta credible external source ambayo inasema:-
Hayo ni maelezo kutoka tovuti ya University of California, Davis, na ukiingia website ya SUA wenyewe, hapa utakuta mlolongo wa research projects!
 
Sasa shida hizo tafiti hazina tija leo unaulizwa hao panya wanatumika wapi kusaidia wananchi je utakuwa na jibu
 
Usisahau Tanzania kuna uhaba mkubwa sana, tena sana wa Walimu wa Sayansi!!! Nakumbuka, enzi za JK walitumia njia mbalimbali kutaka kumaliza hilo tatizo, na njia hizo kwa mfuatano zilikuwa:-

1. Kuwapa mikataba wapya wastaafu waliokuwa wanafundisha masomo ya sayansi... waliopatikana hawakufika 100!

2. Wakawaita Form VI leavers waliokuwa wamemaliza masomo ya sayansi, na wapo tu mtaani! Serikali ikawaahidi kuwapa mkopo 100% and guaranteed employment ili kusomea Special Advanced Diploma (Science & Maths) pale DUCE!... Hawakutosha!

3. Offer kama #2 hapo juu ikaja kwa madogo wanaomaliza Form IV na kufaulu masomo ya sayansi ili wakasome 3 years Special Diploma ( Science & Maths) na kuahidiwa ajira moja kwa moja... hawa ndo wale ambao Magu aliwaita vilaza, na akaifuta hiyo special diploma!!

Sasa katika harakati hizo hizo za kupunguza uhaba wa walimu wa sayansi, ndipo SUA napo zikaanzishwa various BSc Educations courses za sayansi kama vile BS Ed ( Chemistry & Physics), Physics & Maths, Chemistry & Biology, Chemistry & Maths, etc!!

Sasa hivi kweli unaweza kuponda hilo suala?!
 
Sasa shida hizo tafiti hazina tija leo unaulizwa hao panya wanatumika wapi kusaidia wananchi je utakuwa na jibu
Kwenye tija hapo ndio shida. Lakini nadhani hii miradi haikuanzishwa na Watanzania, ililetwa na wafadhili ambao yamkini kwao ina tija. Serikali sasa idumishe ufadhili wa tafiti zenye tija kwa watanzania.
 
Panya wetu wamefanya nini mpaka sasa
 
Hatujashindwa mkuu hamjaweka hela mezani ndo tatizo. Au unataka professa achukue 4m zake anazo lipwa kwa mwezi ndo afanyie tafiti?

Watu wanafanya tafiti ambazo zinakua funded na donors, na hao donors wako interested na projects ambazo hata bongo hazina tija , ila ndo wana weka hela huko, na ma professa wana fanya hizo research.

Narudia tena, shida haiko SUA, shida iko kwenye serikali na vipaumbele vyake.As long as mtaendelea kupanga mipango ya miaka mitano ya uchaguzi, sahau kuhusu tafiti zenye tija, sahau kabisa.

Mm nakuambia hata kupata chanjo ya korona, inawezekana. Wekeni pesa watu wajifungie maabara, matokeo mtayaona. Lasivyo mtaendelea kupiga makelelw tyu.

[emoji112][emoji112]

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Sasa shida hizo tafiti hazina tija leo unaulizwa hao panya wanatumika wapi kusaidia wananchi je utakuwa na jibu
Ushaambiwa panya wanatumika kutegua mabomu sehemu ambapo kuna mabomu ya ardhini huelewi.

Hao panya wana letewa sampuli kwa ajili ya kupima wagonjwa wa TB kwa haraka zaidi, sampuli zitakazo onyesha positive results zonpelekwa maabara for confirmation. Hii inaongeza speed ya kupima TB.

Pitia kwenye website ya Apopo utaona mpaka sasa, wametegua mabomu mangapi na wame weza ku diagnose sampuli ngapi za TB.



Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
1. Una HOJA lakini haikidhi kujibu hoja ya mtoa hoja.

2. Hizo digrii za ualimu katika masomo ya sayansi kama ulivyotanabaisha zinafundishwa katika Vyuo mbalimbali hapa nchini.

3. Tatizo linaloleta maswali ni lengo/malengo ya chuo kikuu cha kilimo pekee hapa nchini ku-diverge kwenye mambo ya kilimo kuwa na mwelekeo wa kutoa digrii za elimu?

4. Hivi hizo digrii za elimu zinafundishwa na Ma- Profesa Mahoo (ana zaidi ya miaka 30 hapo SUA) Msanya au kuna wengine waliletwa?Wahadhiri wa UDSM, DUCE,TUMAINI,SAUTI,N.K warafundisha nini kwenye vitivo vyao vya Elimu?

5. Hebu wasomi wetu tuwe na mawazo chanya kuendana na dunia ya sasa ili kuiletea nchi yetu maendeleo pamoja na kumsaidia Mhe.Rais wetu Mama SSH ili tupate matokeo chanya.

6. Huoni kuna ukakasi katika malengo ya uanzishwaji wa SUA miaka hiyo na uanzishwaji wa digrii za Elimu SUA miaka ya hivi karibuni?

7. Tutafakari zaidi na hao PANYA WENU. Inaonekana hawana tija kwa Taifa na isiwe kama Chaka la kuomba misaada ya fedha kutoka kwa wafadhili.

KARIBU TUTAFAKARI PAMOJA!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…