Tetesi: SUA: Prof Mstaafu afariki kwa tatizo la kushindwa kupumua! Ni Prof wa tatu kufariki ndani ya miezi miwili kwa tatizo kama hilo

Huu uzi ufungwe na mleta hii post aonywe
 
Nasikia na Meneja wa Banki ya NMB Geita,nae amefariki usiku wa leo kwa changamoto ya kupumua.
 
Nimeleta habari ambayo ni tetesi. Wenye habari kamili watatuhabarisha. Hii ni JF,tetesi nayo ni habari na inaruhusiwa.
 
Ukishafariki hata kama ulikua na sifa gani, u sawa na mbuzi aliekufa porini tu.

Kwani akitangazwa ndio atafufuka, nashangaa sana watu wanaoweka ufahari makaburini kwenye mwili unaooza
 
Hii changamoto ya kupumua itakuwa inaendelea kutafuna taratibu hasa kwa wenye umri mkubwa, over 60 yrs...
 
Kama tunavyoshindwa kuchagua siku ya kuzaliwa, hatuwezi kuchagua siku ya kufa.
 
Ukishafariki hata kama ulikua na sifa gani, u sawa na mbuzi aliekufa porini tu.

Kwani akitangazwa ndio atafufuka, nashangaa sana watu wanaoweka ufahari makaburini kwenye mwili unaooza
Ni desturi yetu. Endapo Mangwea na Kanumba hadi Ikulu ilishiriki kuwaaga na hukutoa hoja kama hiyo ila kwa Profesa unaona kawaida! Ni nini kimetupata sisi Watz?
 
Inatamkwa imepungua sana haisemwi imekwisha na ndio sababu tunasisitizwa tuendelee kuchukua tahadhari
Korona ipo usidanganywe na wanasiasa kwamba imekwisha fuatilia taarifa za kimataifa ndio utajua kuwa Kumi na Kenda anazidi kupuyanga China wenyewe wameshapata maambukizi tena yaani FUTA limerudi CHINA.
 
Inatamkwa imepungua sana haisemwi imekwisha na ndio sababu tunasisitizwa tuendelee kuchukua tahadhari
Imepungua kutoka ngapi hadi ngapi? Watu hawapimwi lakini wanasema imepungua mara imekwisha mara tuna wagonjwa 66 yaani hawaeleweki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…